ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
44 : 24

يُقَلِّبُ ٱللَّهُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ

Mwenyezi Mungu hubadilisha usiku na mchana. Hakika katika hayo yapo mazingatio kwa wenye kuona. info

Mwenyezi Mungu huzigeuza hali za usiku na mchana kwa urefu na ufupi, na kwa kuanzia na kumalizikia, kwa mizunguko ya falaki. Hakika katika hayo pana mazingatio kwa wenye akili zilio nzima zenye busara, na kwa njia hiyo wakamuamini Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
45 : 24

وَٱللَّهُ خَلَقَ كُلَّ دَآبَّةٖ مِّن مَّآءٖۖ فَمِنۡهُم مَّن يَمۡشِي عَلَىٰ بَطۡنِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن يَمۡشِي عَلَىٰ رِجۡلَيۡنِ وَمِنۡهُم مَّن يَمۡشِي عَلَىٰٓ أَرۡبَعٖۚ يَخۡلُقُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na Mwenyezi Mungu ameumba kila kinyama kutokana na maji. Wengine katika wao huenda kwa matumbo yao, na wengine huenda kwa miguu miwili, na wengine huenda kwa miguu mine. Mwenyezi Mungu huumba ayatakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. info

Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na ndiye aliye anzisha kila kitu kwa kupenda kwake. Na akaumba kila kilicho hai kutokana na asili moja ya shirika, nayo ni maji. Na kwa hivyo kila kihai hakiachi kuwa na maji. Kisha zinawakhitalifisha khitilafu nyengine kwa namna, na uwezo, na sura, na kadhaalika. Katika wanyama wapo wanao tambaa kwa matumbo yao, kama samaki, na nyoka. Na wapo wanao kwenda kwa miguu miwili kama wanaadamu na ndege. Na wapo wanao kwenda kwa miguu mine kama mahayawani wengi wa kufugwa na wa mwituni. Mwenyezi Mungu huumba apendavyo kwa njia mbali mbali, kuonyesha uwezo wake na ujuzi wake. Kwani ni Mwenye kutaka atakacho, na Mwenye kukhitari apendacho. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu. "Na Mwenyezi Mungu ameumba kila kinyama kutokana na maji. Wengine katika wao huenda kwa matumbo yao, na wengine huenda kwa miguu miwili, na wengine huenda kwa miguu mine. Mwenyezi Mungu huumba ayatakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." Maji katika Aya hii tukufu ni maji ya uzazi, yaani vinyama vinavyo toa manii. Na Aya hii si kama imetangulia msafara wa sayansi katika kubainisha kuzalikana mtu kutokana na tone la manii, kama ilivyo kuja katika kauli yake Aliye tukuka: "Hebu naajitazame mtu, ameummbwa kwa kitu gani? Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa." (Sura Att'ariq 5,6), bali imetangulia pia katika kubainisha kwamba kila kinyama kinacho kwenda kwenye ardhi kimeumbwa kwa njia ya kuzalikana na vinyama vya manii, na vinga khitalifiana hivyo vinyama vya manii na sifa zao katika kila namna mnamo hizo namna za vinyama. Katika maana za kisayansi ambazo zaweza kuwa nazo hii Aya ni kuwa maji ni msingi wa kila kiumbe kilicho hai. Kwa mfano mwili wa mtu umekusanya 70% ya uzito wake kuwa ni maji. Yaani mtu mwenye uzito wa kilo 70, kiasi kilo 50 ni maji. Na kabla ya kuteremka Qur'ani haya hayakuwa yakijuulikana kabisa ya kuwa mtu ana sehemu hii kubwa ya mwili wake kuwa ni maji. Na maji ndio chakula cha dharura kabisa kwa mwanaadamu. Kwani hali mtu yamkini aishi siku 60 bila ya kula chakula chochote, hawezi kuishi bila ya maji kwa zaidi kuliko siku 3 mpaka 10 mwisho wake. Na maji ndio msingi wa kufanyika damu, na maji ya limfo, na ya katika ubongo wa mifupa, vimwagavyo na mwili, kama mkojo, na jasho, na machozi, na mate, na nyongo, na maziwa, na maji yanayo patikana katika viungo, na ambayo ndiyo sababu ya ulaini wa mwili. Na yakikosekana 20% ya maji yake basi mwanaadamu hukabiliwa na mauti. Na maji huyayusha vyakula vikasahilika kufyonzeka. Na kadhaalika huyayusha makombo yenye asili ya vilivyo hai au maadini katika mkojo na jasho. Na kwa namna hii maji yana sehemu kubwa zaidi na muhimu kabisa katika kuumbwa kwa mwili. Na kwa hivyo yamkini kusema kwamba kila kiumbe kilicho hai kimeumbwa kutokana na maji.

التفاسير:

external-link copy
46 : 24

لَّقَدۡ أَنزَلۡنَآ ءَايَٰتٖ مُّبَيِّنَٰتٖۚ وَٱللَّهُ يَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Kwa yakini tumeteremsha Ishara zinazo bainisha. Na Mwenyezi Mungu hummwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka. info

Na hakika Sisi tumeteremsha kwa wahyi Aya zilizo wazi za kubainisha hukumu na mawaidha, na zinazo piga mifano. Na Mwenyezi Mungu humwezesha kwenye kheri ampendaye katika waja wake ambao wapo tayari kuziangalia na kufaidika nazo.

التفاسير:

external-link copy
47 : 24

وَيَقُولُونَ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلرَّسُولِ وَأَطَعۡنَا ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٞ مِّنۡهُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۚ وَمَآ أُوْلَٰٓئِكَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na wanasema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume, na tumet'ii. Kisha kikundi katika hao hugeuka baada ya hayo. Wala hao si wenye kuamini. info

Na wanaafiki husema kwa ndimi zao: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume, na tunazifuata amri zao. Na wanapo tiwa mtihanini kikundi kati yao hukataa kushirikiana na Waislamu katika kazi ya kheri, kama Jihadi na nyenginezo, baada ya kauli yao hii. Na watu hawa si Waumini wa kweli, wala hawastahiki kutumiliwa jina la Waumini kwao.

التفاسير:

external-link copy
48 : 24

وَإِذَا دُعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ إِذَا فَرِيقٞ مِّنۡهُم مُّعۡرِضُونَ

Na wanapo itwa kumuendea Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, kipo kikundi katika wao kinakataa. info

Na katika hali zao ni kuwa wakitakiwa kuhukumiwa mbele ya Mtume kwa jambo alilo literemsha Mwenyezi Mungu, unaafiki wa baadhi yao hudhihiri, na wao hukataa kuhukumiwa wakijua kuwa haki ni ya wale makhasimu zao.

التفاسير:

external-link copy
49 : 24

وَإِن يَكُن لَّهُمُ ٱلۡحَقُّ يَأۡتُوٓاْ إِلَيۡهِ مُذۡعِنِينَ

Na ikiwa haki ni yao, wanamjia kwa kut'ii. info

Ama wakijua kuwa haki iko upande wao basi humjia Mtume mbio mbio ili awahukumu baina yao na makhasimu zao.

التفاسير:

external-link copy
50 : 24

أَفِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَمِ ٱرۡتَابُوٓاْ أَمۡ يَخَافُونَ أَن يَحِيفَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَرَسُولُهُۥۚ بَلۡ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Je! Wana maradhi katika nyoyo zao, au wanaona shaka, au wanaogopa ya kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake watawadhulumu? Bali hao ndio madhaalimu. info

Na kwa nini wanasimama msimamo huu katika kushitakiana mbele ya Mtume? Ni kwa sababu nafsi zao zimesibiwa na maradhi ya upofu, na kwa hivyo haziridhiki na hukumu yako ya haki? Au ni kwa kuwa wao wanatilia shaka uadilifu wa Muhammad s.a.w. katika kuhukumu? Si lolote katika hayo kabisa. Lakini hao ni madhaalimu walio dhulumu nafsi zao na wengineo kwa sababu ya ukafiri wao na unaafiki wao na kuiacha kwao haki.

التفاسير:

external-link copy
51 : 24

إِنَّمَا كَانَ قَوۡلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذَا دُعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ أَن يَقُولُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Haiwi kauli ya Waumini wanapo itwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila ni kusema: Tumesikia, na tumet'ii! Na hao ndio wenye kufanikiwa. info

Hakika kauli ya haki ifaayo kwa Waumini wa kweli wanapo itwa wahukumiwe kwa mujibu wa yaliyo kuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ni kuwa waseme kwa kukubali na kunyenyekea: Tumesikia wito wako, ewe Muhammad! Na tumeridhia hukumu yako. Na hao ndio watao kuwa watu wa kufanikiwa katika dunia yao na Akhera yao.

التفاسير:

external-link copy
52 : 24

وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَخۡشَ ٱللَّهَ وَيَتَّقۡهِ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَآئِزُونَ

Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu. info

Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na kuridhia anayo yaamrisha Mtume s.a.w. na wakaiogopa dhati ya Mwenyezi Mungu Tukufu, na wakaukumbuka Utukufu wake, na wakaikhofu ghadhabu yake, hao ndio watakao pata radhi ya Mwenyezi Mungu na mapenzi yake, na neema za Pepo, na ndio wenye kupata kheri tupu.

التفاسير:

external-link copy
53 : 24

۞ وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَئِنۡ أَمَرۡتَهُمۡ لَيَخۡرُجُنَّۖ قُل لَّا تُقۡسِمُواْۖ طَاعَةٞ مَّعۡرُوفَةٌۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kiapo chao ya kwamba ukiwaamrisha kwa yakini watatoka. Sema: Msiape! Ut'iifu unajuulikana. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. info

Na wanaafiki wanaapa kwa ukomo wa nguvu za viapo vyao, kwamba wewe, Muhammad, ukiwaamrisha watoke nawe kwenda vitani watakut'ii. Waambie: Msiape! Kwani mambo yatakikanayo kwenu mnayajua, hapana hata mmoja wenu asiye yajua. Wala yamini zenu za uwongo haziondoi ujuzi huo. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua baraabara kila linalo tokana nanyi, na Yeye atakulipeni kwayo.

التفاسير: