ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
32 : 15

قَالَ يَٰٓإِبۡلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ

(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu? info

Hapo basi Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Ewe Iblisi! Kitu gani kilicho kupelekea hata ukaasi na usiwe pamoja na wanyenyekevu walio sujudu?

التفاسير:

external-link copy
33 : 15

قَالَ لَمۡ أَكُن لِّأَسۡجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقۡتَهُۥ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ

Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unaotoa sauti, unao tokana na matope yenye sura. info

Iblisi akasema: Si shani yangu mimi kumsujudia mtu uliye muumba kwa udongo mkavu, wenye kutoa sauti ukigongwa, nao umegeuka rangi, wenye kutiwa sura.

التفاسير:

external-link copy
34 : 15

قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٞ

(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! info

Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Ukiwa wewe umekuwa a'asi, umetokana na ut'iifu wangu, basi tokelea mbali kwenye Bustani hii! Kwani hakika wewe umefukuzwa kwenye rehema yangu pahala pa hishima.

التفاسير:

external-link copy
35 : 15

وَإِنَّ عَلَيۡكَ ٱللَّعۡنَةَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo. info

Na Mimi nimekwisha kuhukumia ubaidike na rehema na utukufu mpaka Siku ya Kiyama, Siku ya Hisabu na Malipo. Na hapo ndipo utapo pata adhabu, wewe na wanao kufuata .

التفاسير:

external-link copy
36 : 15

قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapofufuliwa. info

Iblisi akasema, hali naye kesha kuwa ni mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu: Ewe Muumba wangu! Nipe muhula, nibakishe usinitwae mpaka Siku ya Kiyama, Siku watapo fufuliwa watu wakawa hai baada ya kufa kwao.

التفاسير:

external-link copy
37 : 15

قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ

(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula info

Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Wewe utabakishwa, umepewa muhula,

التفاسير:

external-link copy
38 : 15

إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ

Mpaka siku ya wakati maalumu. info

Mpaka wakati niliyo ukadiria, ninao ujua Mimi. Na kama utavyo kuwa mrefu una kikomo.

التفاسير:

external-link copy
39 : 15

قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote, info

Akasema Iblisi, mkhalifu, a'asi: Ewe Muumba wangu unaye nibakisha! Umenitakia upotofu, nami nikatumbukia ndani yake. Basi kwa sababu hiyo nahakikisha kuwa nitawapambia wanaadamu maovu wayaone mazuri, na nitafanya kila juhudi kuwapotoa wote!

التفاسير:

external-link copy
40 : 15

إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ

Ila waja wako walio safika. info

Wala hawatoepukana na upotovu wangu ila wale waja wako walio kufanyia ikhlasi Wewe na nisio weza kuzimiliki nyoyo zao kwa zilivyo kuwa imara kwa kukumbuka Wewe.

التفاسير:

external-link copy
41 : 15

قَالَ هَٰذَا صِرَٰطٌ عَلَيَّ مُسۡتَقِيمٌ

Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka. info

Hakika usafi wa waja walio isafia niya Dini yao ndio Njia Iliyo Nyooka, na haki yangu nisiikiuke, kwani hao siwezi kuwapotoa. (Tafsiri hii yaonyesha maneno hayo ni ya Iblisi. Lakini Tafsiri nyengine zinasema maneno hayo ni ya Mwenyezi Mungu, kwa mfano ya Abdulla Saleh, Abdulla Yusuf, Pickthall, Razi, Baidhawi, Qurtubi, Zamakhshari, Ibn Kathir, Assad.)

التفاسير:

external-link copy
42 : 15

إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ

Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata. info

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Hakika waja wangu walio nisafia Mimi Dini yao wewe huna uwezo wa kuwapoteza. Lakini wapotovu, walio zama katika upotovu, walio kufuata wewe, basi hao ndio unayo madaraka juu ya nyoyo zao.

التفاسير:

external-link copy
43 : 15

وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote. info

Na hakika Moto mkali mno ndio wameahidiwa hao wote kuwa ndiyo adhabu ya kutia uchungu.

التفاسير:

external-link copy
44 : 15

لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٰبٖ لِّكُلِّ بَابٖ مِّنۡهُمۡ جُزۡءٞ مَّقۡسُومٌ

Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa. info

Wala huo Moto mkali hauna mlango mmoja tu, bali una milango saba kwa ajili ya wingi wanao stahiki kuingia humo. Na kila mlango una kundi lake makhsusi. Na kila kundi una cheo chake maalumu cha kulingana na uovu wake.

التفاسير:

external-link copy
45 : 15

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ

Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. info

Haya ni malipo ya wanao mfuata Shetani. Ama wale ambao Shetani kashindwa kuwapotoa, kwa kuwa wameweka kinga baina yake na nyoyo zao, hao watapata Mabustani yaliyo bora, na chemchem zinazo pita .

التفاسير:

external-link copy
46 : 15

ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ

(Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani. info

Mola wao Mlezi atawaambia: Ingieni katika Bustani hizi kwa utulivu na amani. Kwani hapana khofu juu yenu, hamhuzunikii nyakati zenu.

التفاسير:

external-link copy
47 : 15

وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلٍّ إِخۡوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ

Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana. info

Na hakika watu wa Imani wataishi katika kheri hii na nafsi zao zimetua. Kwani tumezitoa chuki zilizo kuwamo katika nafsi hizo. Wote hao watakuwa ndugu waketi juu ya viti vya enzi zikitazamana nyuso zao kwa furaha na mahaba, wala hawawi mmoja nyuma ya mwenzie wakichunguliana visogoni.

التفاسير:

external-link copy
48 : 15

لَا يَمَسُّهُمۡ فِيهَا نَصَبٞ وَمَا هُم مِّنۡهَا بِمُخۡرَجِينَ

Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo. info

Hawapatwi na machofu huko. Na hiyo ni neema ya daima, wala hawatotoka humo milele.

التفاسير:

external-link copy
49 : 15

۞ نَبِّئۡ عِبَادِيٓ أَنِّيٓ أَنَا ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. info

Ewe Nabii muaminifu! Wape khabari waja wangu wote kwamba Mimi ni Mwingi wa kughufiria na kusamehe kwa mwenye kutubu, akaamini, na akatenda mema. Na kwamba Mimi ni Mwingi wa kuwarehemu.

التفاسير:

external-link copy
50 : 15

وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ ٱلۡعَذَابُ ٱلۡأَلِيمُ

Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu! info

Na wape khabari kwamba adhabu ninayo wateremshia wenye kuasi na kukufuru ni adhabu yenye kutia machungu kweli, na adhabu yoyote nyengineyo haihisabiwi kuwa ina machungu mbele ya hii.

التفاسير:

external-link copy
51 : 15

وَنَبِّئۡهُمۡ عَن ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ

Na uwape khabari za wageni wa Ibrahim. info

Ewe Nabii! Waambie pia, katika kubainisha rehema yangu makhsusi katika dunia na adhabu yangu kwa wenye kuasi humo, khabari ya Malaika walio mfikia Ibrahim kama wageni.

التفاسير: