ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

At-Taghabun

external-link copy
1 : 64

يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Vinamtakasa Mwenyezi Mungu na sifa zisizonasibiana na Yeye vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini. Ni Wake Yeye Mwenyezi Mungu, kutakasika na kila upungufu ni Kwake, uendeshaji mambo usio na kizuizi katika kila kitu. Na Yeye Ndiye Mwenye sifa njema zilizo nzuri. Na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 64

هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ فَمِنكُمۡ كَافِرٞ وَمِنكُم مُّؤۡمِنٞۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewafanya nyinyi mpatikane kutoka kwenye hali ya kutokuwako, kati yenu kuna wenye kuukanusha uungu Wake na baadhi yenu kuna wenye kuuamini na kufuata Sheria Zake kivitendo. Na Yeye, kutakasika na kila sifa za upungufu ni Kwake, ni Mwenye kuviona vitendo vyenu, hakuna chochote chenye kufichamana Kwake, na Atawalipa kwavyo. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 64

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّ وَصَوَّرَكُمۡ فَأَحۡسَنَ صُوَرَكُمۡۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ

Ameumba mbingu na ardhi kwa hekima kubwa, na Akawaumba nyinyi katika sura nzuri, na Kwake Yeye ndio marejeo Siku ya Kiyama, Amlipe kila mtu kwa matendo yake. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 64

يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَيَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Anajua, kutakasika na kutukuka ni Kwake, kila kilichoko mbinguni na ardhini, na Anakijua mnachokificha, enyi watu, na mnachokidhihirisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yale yanayodhamiriawa na vifua na kufichwa na nafsi info
التفاسير:

external-link copy
5 : 64

أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَبَؤُاْ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَبۡلُ فَذَاقُواْ وَبَالَ أَمۡرِهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Je haikuwajia nyinyi, enyi washirikina, habari ya wale waliokufuru miongoni mwa watu waliopita kabla yenu, ulipowafikia wao mwisho mbaya wa ukafiri wao na uovu wa vitendo vyao hapa ulimwenguni na kuwa wao kesho Akhera watakuwa na adhabu kali iumizayo? info
التفاسير:

external-link copy
6 : 64

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُۥ كَانَت تَّأۡتِيهِمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٞ يَهۡدُونَنَا فَكَفَرُواْ وَتَوَلَّواْۖ وَّٱسۡتَغۡنَى ٱللَّهُۚ وَٱللَّهُ غَنِيٌّ حَمِيدٞ

Hayo yaliyowapata duniani na yatakayowapata kesho Akhera ni kwamba wao walikuwa wakijiliwa na Mitume wa Mwenyezi Mungu na alama waziwazi na miujiza iliyofunuka wazi, huwa wakisema, «Je binadamu kama sisi wanatuongoza? Hapo wakamkufuru Mwenyezi Mungu, wakaukanusha ujumbe wa Mitume Wake na wakaipa mgongo haki wasiikubali. Na Mwenyezi Mungu Hana haja na kuamini kwao wala kuabudu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Ana utajiri uliotimia usio na mpaka, ni Mwenye kusifiwa kwa maneno Yake, matendo Yake, na sifa Zake, Hawajali wao wala haumdhuru Yeye upotevu wao chochote. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 64

زَعَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَن لَّن يُبۡعَثُواْۚ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبۡعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلۡتُمۡۚ وَذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ

Walidai wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu kwa ubatilifu kwamba wao hawatatolewa kwenye makaburi yao baada ya kufa. Waambie, ewe Mtume, «Ndio. Naapa kwa Mola wangu! Mtatolewa makaburini mwenu mkiwa hai, kisha mtapewa habari ya yale mliyoyafanya duniani. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni sahali na rahisi. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 64

فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلنُّورِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلۡنَاۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, enyi washirikina, na mjiongoze kwa Qur’ani Aliyomteremshia Mtume Wake. Na Mwenyezi Mungu kwa mnayoyafanya ni Mtambuzi, hakuna kinachofichamana na Yeye cha matendo yenu na maneno yenu, na Yeye ni Mwenye kuwalipa kwa hayo Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 64

يَوۡمَ يَجۡمَعُكُمۡ لِيَوۡمِ ٱلۡجَمۡعِۖ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلتَّغَابُنِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعۡمَلۡ صَٰلِحٗا يُكَفِّرۡ عَنۡهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Ikumbukeni Siku ya Mkusanyo ambayo Mwenyezi Mungu Atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho. Siku hiyo ambayo ina mpunjano na mtengano kati ya viumbe: Waumini wawapunje makafiri na wenye kuasi, na wao hao( hao makafiri na waasi) iwadhihirikie wazi kuwa wao ndio waliopata hasara. Basi wenye Imani wataingia Peponi kwa rehema za Mwenyezi Mungu, na wenye ukafiri wataingia Motoni kwa uadilifu Wake. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na akafanya matendo ya utiifu Kwake, Atamfutia dhambi zake na Amtie kwenye mabustani ya Pepo ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito ya maji, hali ya kukaa milele humo. Kukaa milele huko Peponi ndiko kufaulu kukubwa ambako hakuna kufaulu kushinda huko. info
التفاسير: