ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
10 : 64

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Na wale ambao wanapinga kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki na wakazikanusha dalili za kuwa Yeye Ndiye Mola na hoja za uungu Wake Alizowatuma nazo Mitume Wake, hao ni watu wa Motoni, ni wenye kukaa humo milele. Moto huo wa Jahanamu ni marejeo maovu mno watakayofikia. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 64

مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ يَهۡدِ قَلۡبَهُۥۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Halimpati yoyote jambo lolote la shida isipokuwa kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu na mapitisho Yake na makadirio Yake. Na yoyote anayemuamini Mwenyezi Mungu, Atauongoza moyo Wake ufuate amri Zake na uridhike na mapitisho Yake. Atauongoza kwenye njia nzuri ya maneno, vitendo na hali. Kwani uongofu hasa ni wa moyo, na viungo vinafuata. Na Mwenyezi Mungu kwa kila kitu ni Mjuzi, hakifichamani Kwake chochote miongoni mwa hivyo. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 64

وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ

Na mtiini Mwenyezi Mungu, enyi watu, na muongokee Kwake katika yale Aliyoyaamrisha na Aliyoyakataza, na mfuateni Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, katika yale aliyowafikishia kutoka kwa Mola wake. Na iwapo mtaupa mgongo utiifu wenu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi Mjumbe wetu hana madhara yoyote kutokana na kupa mgongo kwenu. Jukumu lake yeye ni kuwafikishia nyinyi yale Aliyotumilizwa kwayo ufikishaji wenye maelezo ya waziwazi. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 64

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Ambaye hukuna muabudiwa wa kweli isipokiuwa Yeye. Na kwa Mwenyezi Mungu tu na wategemee Waumini, kwa upweke Wake, katika mambo yao yote. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 64

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجِكُمۡ وَأَوۡلَٰدِكُمۡ عَدُوّٗا لَّكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُمۡۚ وَإِن تَعۡفُواْ وَتَصۡفَحُواْ وَتَغۡفِرُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake! Kwa kweli miongoni mwa wake zenu na wana wenu ni maadui wenu, wanawazuia nyinyi na njia ya Mwenyezi Mungu na wanawavunja moyo ya kumtii Mwenyezi Mungu, basi jihadharini nao wala msiwasikilize. Na iwapo mtayasamehe makosa yao, mkayapa mgongo na mkayaficha msiyatangaze, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe ni Mwingi wa rehema, Atawasamehe nyinyi madhambi yenu, kwani Yeye, Aliyetakasika na kila upungufu, ni Mkubwa wa kusamehe ni Mkunjufu wa rehema. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 64

إِنَّمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَأَوۡلَٰدُكُمۡ فِتۡنَةٞۚ وَٱللَّهُ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Hayakuwa mali yenu na watoto wenu isipokuwa ni majaribio na mtihani kwenu. Na Mwenyezi Mungu, Kwake Yeye kuna thawabu kubwa kwa aliyechagua kumtii Yeye kuliko kumtii asiyekuwa Yeye na akatekeleza haki ya Mwenyezi Mungu katika mali yake. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 64

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُمۡ وَٱسۡمَعُواْ وَأَطِيعُواْ وَأَنفِقُواْ خَيۡرٗا لِّأَنفُسِكُمۡۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفۡسِهِۦ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Fanyeni juhudi zenu, enyi Waumini, na tumieni nguvu zenu katika kumcha Mwenyezi Mungu, na msikilizeni Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, usikilizaji wa kuzingatia na kufikiri, zifuateni amri Zake na myaepuke makatazo Yake na mtoe katika kile Alichowaruzuku Mwenyezi Mungu, hilo litakuwa bora kwenu. Na atakayeepukana na uchoyo na kubania kilichozidi katika mali, basi hao ndio watakaozipata kheri zote, watakaofaulu kupata kila wanalolitaka. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 64

إِن تُقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا يُضَٰعِفۡهُ لَكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ

Iwapo mtatoa mali yenu katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Yeye na kwa moyo mzuri, Atawaongezea Mwenyezi Mungu thawabu za ambacho mmekitoa na Atawasamehe madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kurudisha shukrani kwa watoaji kwa kuwapa malipo mema ya kile walichokitoa, ni Mpole kwa kutoharakisha mateso kwa wanaomuasi. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 64

عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Na Yeye, kutakasika na kila upungufu ni Kwake, ni Mjuzi wa kila lililofichika lisionekane na lile lililojitokeza likaonekana, ni Mshindi Asiye na mshindani, ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake. info
التفاسير: