ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
16 : 48

قُل لِّلۡمُخَلَّفِينَ مِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ سَتُدۡعَوۡنَ إِلَىٰ قَوۡمٍ أُوْلِي بَأۡسٖ شَدِيدٖ تُقَٰتِلُونَهُمۡ أَوۡ يُسۡلِمُونَۖ فَإِن تُطِيعُواْ يُؤۡتِكُمُ ٱللَّهُ أَجۡرًا حَسَنٗاۖ وَإِن تَتَوَلَّوۡاْ كَمَا تَوَلَّيۡتُم مِّن قَبۡلُ يُعَذِّبۡكُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا

Waambie wale waliojikalisha nyuma miongoni mwa al-a'rāb (nao ni mabedui) ili kujiepusha na kupigana, «Mtaitwa mwende mpigane na watu wenye nguvu nyingi za kupigana, mpigane nao au wasalimu amri bila ya kupigana. Basi mkimtii Mwenyezi Mungu katika hilo Alilowaitia la kupigana na watu hao Atawapa Pepo, na mkimuasi kama mlivofanya mlipojikalisha nyuma msiende Makkah pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu , rehema ya Mwenyezi Mungu na Amani zimshukie, Atawaadhibu adhabu yenye kuumiza.» info
التفاسير:

external-link copy
17 : 48

لَّيۡسَ عَلَى ٱلۡأَعۡمَىٰ حَرَجٞ وَلَا عَلَى ٱلۡأَعۡرَجِ حَرَجٞ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرِيضِ حَرَجٞۗ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَمَن يَتَوَلَّ يُعَذِّبۡهُ عَذَابًا أَلِيمٗا

Yule aliye kipofu kati yenu, enyi watu, hana dhambi, wala aliye kiguru hana dhambi, wala aliye mgonjwa hana dhambi, wanapojikalisha nyuma wasishiriki katika kupigana jihadi pamoja na Waumini, kwa kuwa wao hawawezi. Na Mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Atamtia kwenye mabustani ya Pepo ambayo chini ya miti yake na majumba yake ya fahari itakuwa ikipita mito. Na Mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake akajikalisha nyuma ili kuhepa kupigana jihadi pamoja na Waumini, Atamuadhibu adhabu yenye uchungu na kuumiza. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 48

۞ لَّقَدۡ رَضِيَ ٱللَّهُ عَنِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذۡ يُبَايِعُونَكَ تَحۡتَ ٱلشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمۡ فَأَنزَلَ ٱلسَّكِينَةَ عَلَيۡهِمۡ وَأَثَٰبَهُمۡ فَتۡحٗا قَرِيبٗا

Mwenyezi Mungu Ameridhika na Waumini pale walipokupa mkono wa ahadi, ewe Mtume, chini ya mti (Hii ndio hiyo Bay 'ah al-Ridwān ya hapo Ḥudaybiyah). Mwenyezi Mungu Alijua yaliyomo ndani ya nyoyo za Waumini hawa ya Imani, ukweli na utekelezaji ahadi, basi Mwenyezi Mungu Akawateremshia utulivu, Akaziimarisha nyoyo zao na Akawapa, badala ya kile kilichowapita katika mapatano ya Ḥudaybiyah, ufunguzi wa karibu, nao ni ufunguzi wa kuiteka Khaybar info
التفاسير:

external-link copy
19 : 48

وَمَغَانِمَ كَثِيرَةٗ يَأۡخُذُونَهَاۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمٗا

na ngawira nyingi za mali za Mayahudi wa Khaybar walizozichukua. Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika kuwatesa maadui Zake, ni Mwingi wa hekimakatika kuendesha mambo ya viumbe Vyake. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 48

وَعَدَكُمُ ٱللَّهُ مَغَانِمَ كَثِيرَةٗ تَأۡخُذُونَهَا فَعَجَّلَ لَكُمۡ هَٰذِهِۦ وَكَفَّ أَيۡدِيَ ٱلنَّاسِ عَنكُمۡ وَلِتَكُونَ ءَايَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ وَيَهۡدِيَكُمۡ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا

Mwenyezi Mungu Amewaahidi nyinyi ngawira nyingi mtakazozichukua katika nyakati zake alizowakadiria, Akawaharakishia ngawira za Khaybar na Akaizuia mikono ya watu isiwafikie nyinyi, lisiwapate ovu lolote kati ya yale maovu ambayo maadui wenu waliwadhamiria ya vita na mapigano, na lisiwapate wale mliowaacha Madina, na ili kule kushindwa kwao, kusalimika kwenu na kughanimu kwenu kuwe ni alama ya nyinyi kuizingatia na kuchukua dalili kwayo kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuwahifadhi nyinyi na kuwanusuru, na yeye Ndiye Anayewaongoza kwenye njia iliyolingana sawa isiyokuwa na mpotoko. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 48

وَأُخۡرَىٰ لَمۡ تَقۡدِرُواْ عَلَيۡهَا قَدۡ أَحَاطَ ٱللَّهُ بِهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٗا

Na hakika Mwenyezi Mungu Amewaahidi nyinyi ngawira nyingine ambayo hamna uwezo nayo, Mwenyezi Mungu, kutakasika na kutukuka ni Kwake, Ndiye Mwenye uweza nayo, nayo iko chini ya mpango Wake na mamlaka Yake, na Ashawaahidi nyinyi kuwapatia, na hapana budi kwamba kile Alichoahidi kitakuwa. Na Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna chochote kinachomshinda. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 48

وَلَوۡ قَٰتَلَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوَلَّوُاْ ٱلۡأَدۡبَٰرَ ثُمَّ لَا يَجِدُونَ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا

Na lau makafiri wa Makkah wangalipigana vita na nyinyi, wangalishindwa na nyinyi na wangaliwapa migongo yao kama vile anavyofanya anayeshindwa vitani, kisha hawatapata, asiyekuwa Mwenyezi Mungu, rafiki wa kushikana na wao kuwapiga vita nyinyi wala msaidizi wa kuwasaidia wao wapigane na nyinyi. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 48

سُنَّةَ ٱللَّهِ ٱلَّتِي قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلُۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ ٱللَّهِ تَبۡدِيلٗا

Huo ndio mpango wa Mwenyezi Mungu Alioupanga kwa viumbe Vyake hapo tangu kuwa Atawanusuru askari Wake na Atawashindisha maadui Wake, na hutapata, ewe Nabii, katika mipango ya Mwenyezi Mungu mabadiliko. info
التفاسير: