ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
47 : 41

۞ إِلَيۡهِ يُرَدُّ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِۚ وَمَا تَخۡرُجُ مِن ثَمَرَٰتٖ مِّنۡ أَكۡمَامِهَا وَمَا تَحۡمِلُ مِنۡ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلۡمِهِۦۚ وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ أَيۡنَ شُرَكَآءِي قَالُوٓاْ ءَاذَنَّٰكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٖ

Kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Peke Yake, Asiye na mshirika, Ndiko kunakorudishwa ujuzi wa kipindi cha kusimama Kiyama, kwani hakuna yoyote anayejua kipindi hiko isipokuwa Yeye. Na hayatoki matunda kwenye vifuko vyake (mitini), na hakuna kiumbe chochote cha kike kinachoshika mimba wala kinachojifungua mimba yake isipokuwa kinajulikana na Mwenyezi Mungu. Hakuna chochote kinachofichamana kwake kuhusu hilo. Na siku ambayo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Atawaita washirikina Siku ya Kiyama kwa kuwakaripia na kuonyesha urongo wao, Awaambie,»Wako wapi washirika wangu ambao mlikuwa mkiwashirikisha katika ibada yangu?» Hapo waseme, «Tunakujulisha sasa kuwa hatuna yoyote atakayeshuhudia Leo kuwa wewe una mshirika.» info
التفاسير:

external-link copy
48 : 41

وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَدۡعُونَ مِن قَبۡلُۖ وَظَنُّواْ مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٖ

Wakawapotea hao washirikina wale washirika wao ambao walikuwa wakiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, wasiwanufaishe na wakajuwa kwa yakini kuwa hakuna makimbilio yoyote ya kuwaepusha wao na adhabu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 41

لَّا يَسۡـَٔمُ ٱلۡإِنسَٰنُ مِن دُعَآءِ ٱلۡخَيۡرِ وَإِن مَّسَّهُ ٱلشَّرُّ فَيَـُٔوسٞ قَنُوطٞ

Binadamu hachoki kumuomba Mola wake Ampatie mema ya duniani, na akipatikana na umasikini na shida, huwa anakata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu na anakufa moyo kwa kuwa na dhana mbaya kwa Mola wake. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 41

وَلَئِنۡ أَذَقۡنَٰهُ رَحۡمَةٗ مِّنَّا مِنۢ بَعۡدِ ضَرَّآءَ مَسَّتۡهُ لَيَقُولَنَّ هَٰذَا لِي وَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآئِمَةٗ وَلَئِن رُّجِعۡتُ إِلَىٰ رَبِّيٓ إِنَّ لِي عِندَهُۥ لَلۡحُسۡنَىٰۚ فَلَنُنَبِّئَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِمَا عَمِلُواْ وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنۡ عَذَابٍ غَلِيظٖ

Na tunapomuonjesha binadamu neema kutoka kwetu baada ya shida na mitihani, hamshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka bali anaruka mpaka na kusema, «Haya niliyoyapata yamenijia kwa kuwa mimi ninastahiki kuyapata, na sidhani kuwa Kiyama ni chenye kuja.» Anasema hayo kwa njia ya kukanusha kufufuliwa «Na kwa kukadiria kuwa Kiyama kitakuja na kuwa mimi nitarudi kwa Mola wangu, basi mimi nitapata Pepo Kwake Yeye.» Basi tutawapasha habari wale walioikanusha Siku ya Kiyama kwa yale maovu waliyoyafanya, na tutawaonjesha adhabu kali. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 41

وَإِذَآ أَنۡعَمۡنَا عَلَى ٱلۡإِنسَٰنِ أَعۡرَضَ وَنَـَٔا بِجَانِبِهِۦ وَإِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ فَذُو دُعَآءٍ عَرِيضٖ

Na tunapomneemesha binadamu kwa afya na riziki au vingineyo, hugeuka na kufanya kiburi kwa kukataa kuifuata haki. Na akipatikana na shida huwa akileta dua ndefu akimuomba Mwenyezi Mungu Amuondolee shida yake; huwa akimjua Mola wake wakati wa shida na hamjui wakati wa neema. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 41

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كَانَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ ثُمَّ كَفَرۡتُم بِهِۦ مَنۡ أَضَلُّ مِمَّنۡ هُوَ فِي شِقَاقِۭ بَعِيدٖ

Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa wakanushaji, «Hebu nipeni habari, iwapo hii Qur’ani inatoka kwa Mwenyezi Mungu kisha nyinyi mkaikataa na mkaikanusha, basi hakuna mpotevu zaidi kuliko nyinyi, kwa kuwa nyinyi mko kinyume kabisa na haki kwa kuikataa kwenu Qur’ani na kuikanusha.» info
التفاسير:

external-link copy
53 : 41

سَنُرِيهِمۡ ءَايَٰتِنَا فِي ٱلۡأٓفَاقِ وَفِيٓ أَنفُسِهِمۡ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمۡ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّۗ أَوَلَمۡ يَكۡفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ

Tutawaonyesha, hawa wakanushaji, aya zetu za kuteka miji na kupata nguvu Uislamu katika majimbo mbalimbali na juu ya dini nyingine na maeneo ya mbingu na ardhi, na katika matukio makubwa Anayoyaleta Mwenyezi Mungu humo na ndani ya nafsi zao, na vile vilivyomo humo miongoni mwa alama za kuvutia za utendakazi wa Mwenyezi Mungu na maajabu ya utengenezaji Wake, (tutawaaonyesha hayo yote) mpaka iwafunukie nyinyi, ufunuzi usiyokubali shaka yoyote, kwamba Qur’ani ndiyo haki iliyoletwa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wa viumbe wote. Je hauwatoshi wao ushahidi wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kuwa ni dalili ya kuwa Qur’ani ni haki na kuwa aliyekuja nayo ni mkweli? Kwani Mwenyezi Mungu Ameishuhudilia kwa kuisadikisha, na Yeye ni shahidi wa kila kitu, na hakuna kitu chochote chenye kutolea ushahidi kuliko ushahidi wa Mwenyezi Mungu, aliyetakasika na kutukuka. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 41

أَلَآ إِنَّهُمۡ فِي مِرۡيَةٖ مِّن لِّقَآءِ رَبِّهِمۡۗ أَلَآ إِنَّهُۥ بِكُلِّ شَيۡءٖ مُّحِيطُۢ

Jueni na mtanabahi kuwa hawa makafiri wako kwenye shaka kubwa kuhusu kufufuliwa baada ya kufa. Jueni na mtanabahi kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Amekizunguka kila kitu kwa ujuzi, uweza na ushindi, hakuna chochote kinachofichamana Kwake ardhini wala mbinguni. info
التفاسير: