ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
39 : 35

هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَٰٓئِفَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ فَمَن كَفَرَ فَعَلَيۡهِ كُفۡرُهُۥۖ وَلَا يَزِيدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ كُفۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ إِلَّا مَقۡتٗاۖ وَلَا يَزِيدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ كُفۡرُهُمۡ إِلَّا خَسَارٗا

Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewafanya nyinyi, enyi watu, baadhi yenu washikilie nafasi ya wengine katika ardhi. Basi Mwenye kukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu miongoni mwenu madhara yake yatamrudia mwenyewe na ule ukafiri wake. Na hauwaongezei wakanushaji ule ukanushaji wao mbele ya Mola wao isipokuwa hasira na ghadhabu, na hakuwaongezei kule kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu isipokuwa upotevu na maangamivu. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 35

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ شُرَكَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُواْ مِنَ ٱلۡأَرۡضِ أَمۡ لَهُمۡ شِرۡكٞ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ أَمۡ ءَاتَيۡنَٰهُمۡ كِتَٰبٗا فَهُمۡ عَلَىٰ بَيِّنَتٖ مِّنۡهُۚ بَلۡ إِن يَعِدُ ٱلظَّٰلِمُونَ بَعۡضُهُم بَعۡضًا إِلَّا غُرُورًا

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Nipasheni habari: Ni kitu gani cha ardhi ambacho washirika wenu wamekiumba? Au hawa washirika wenu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wana ushirika na Mwenyezi Mungu katika uumbaji mbingu? Au tumewapa kitabu, hivyo basi wana ushahidi kutoka humo?» Lakini wakanushaji hawapeani ahadi isipokuwa udanganyifu na uhadazi. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 35

۞ إِنَّ ٱللَّهَ يُمۡسِكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ أَن تَزُولَاۚ وَلَئِن زَالَتَآ إِنۡ أَمۡسَكَهُمَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنۢ بَعۡدِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورٗا

Hakika Mwenyezi Mungu Anazizuia mbingu na ardhi siziondoke pale zilipo. Na lau zitaondoka pale zilipo, hakuna yoyote baada Yake Atakayezizuia. Mwenyezi Mungu ni Mpole katika kuahirisha mateso kwa makafiri na waasi, ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia dhambi zake na akarudi Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 35

وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَئِن جَآءَهُمۡ نَذِيرٞ لَّيَكُونُنَّ أَهۡدَىٰ مِنۡ إِحۡدَى ٱلۡأُمَمِۖ فَلَمَّا جَآءَهُمۡ نَذِيرٞ مَّا زَادَهُمۡ إِلَّا نُفُورًا

Na wakanushaji wa Kikureshi waliapa kwa Mwenyezi Mungu viapo vikali kwamba wakijiwa na mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu wa kuwaonya mateso ya Mwenyezi Mungu, watakuwa ni wenye kusimama wima zaidi na wenye kufuata haki zaidi kuliko Mayahudi, Wanaswara na wengineo. Na alipowajia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, hilo halikuwaongezea wao isipokuwa kuwa mbali na haki na kuikimbia. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 35

ٱسۡتِكۡبَارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَكۡرَ ٱلسَّيِّيِٕۚ وَلَا يَحِيقُ ٱلۡمَكۡرُ ٱلسَّيِّئُ إِلَّا بِأَهۡلِهِۦۚ فَهَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا سُنَّتَ ٱلۡأَوَّلِينَۚ فَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ ٱللَّهِ تَبۡدِيلٗاۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ ٱللَّهِ تَحۡوِيلًا

Kuapa kwao si kwa nia nzuri na kutafuta haki, isipokuwa huko ni kuwafanyia viumbe kiburi katika ardhi, wanakusudia kwa huko kuapa kufanya vitimbi vibaya, udanganyifu na ubatilifu. Na vitimbi vibaya haviwashukii isipokuwa wenyewe. Basi je, wana lolote la kunngojea, hao wenye kiburi na wenye vitimbi, isipokuwa ile adhabu iliyowashukia waliokuwa kama wao ambao waliwatangulia? Hutaupatia mpango wa Mwenyezi Mungu mabadiliko wala mageuko. Hakuna yoyote anayeweza kubadilisha wala kujiepusha na adhabu yeye mwenyewe wala mwingine. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 35

أَوَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ وَكَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعۡجِزَهُۥ مِن شَيۡءٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَلِيمٗا قَدِيرٗا

Je, hawatembei makafiri wa Makkah kwenye ardhi, wakaona ulikuwa vipi mwisho wa wale waliokuwa kabla yao, kama vile 'Ād, Thamūd na mfano wao, na yale yaliyowapata ya maangamivu na yaliyowapata majumba yao ya uharibifu walipowakanusha Mitume, na makafiri hao walikuwa ni wakali zaidi na ni wenye nguvu zaidi kuliko makafiri wa Makkah? Na hakuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kuna kitu chochote mbinguni wala ardhini chenye kumlemea na kumpita. Hakika Yeye ni Mjuzi sana wa matendo yao ni Mwenye uweza wa kuwaangamiza. info
التفاسير: