クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Ali Muhsen Alberwany

Al-A'la

external-link copy
1 : 87

سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى

Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa! info

Litakase jina la Mola wako Mlezi lilio tukufu na kila kitu kisicho kuwa kinaelekeana nalo.

التفاسير:

external-link copy
2 : 87

ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ

Aliye umba, na akaweka sawa! info

Aliye umba kila kitu, na akajaalia uumbaji wote sawa sawa katika hukumu na kupangana.

التفاسير:

external-link copy
3 : 87

وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ

Na ambaye amekadiria na akaongoa,. info

Na akakadiria kwa kila kitu kwa mujibu wa maslaha yake, na akakiongoza.

التفاسير:

external-link copy
4 : 87

وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ

Na aliye otesha malisho! info

Na ambaye akatoa kwenye ardhi mimea namna mbali mbali ya kuwalisha wanyama.

التفاسير:

external-link copy
5 : 87

فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ

Kisha akayafanya makavu, meusi. info

Na akaifanya mimea hiyo baada ya kuwa kijani imestawi, ikakauka na imekuwa myeusi!

التفاسير:

external-link copy
6 : 87

سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ

Tutakusomesha wala hutasahau! info

Ewe Muhammad! Sisi tutakujaalia uwe ni mwenye kuisoma Qur'ani kwa ufunuo kutoka kwetu, na wala hutosahau utacho kihifadhi.

التفاسير:

external-link copy
7 : 87

إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ

Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. info

Isipo kuwa anacho taka Mwenyezi Mungu ukisahau, kwani hakika Yeye Mtukufu anayajua wanayo yadhihirisha waja wake na wanayo yaficha, ikiwa maneno au vitendo.

التفاسير:

external-link copy
8 : 87

وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ

Na tutakusahilishia yawe mepesi. info

Na tutakuwezesha kupita njia ya kufikilia kwa wepesi mambo yako yote.

التفاسير:

external-link copy
9 : 87

فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ

Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. info

Basi wakumbushe watu ikiwa kukumbusha kutaleta manufaa, kwani inavyo faa ndio kuwanafiisha.

التفاسير:

external-link copy
10 : 87

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ

Atakumbuka mwenye kuogopa. info

Watanafiika kwa ukumbusho wako wanao mwogopa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
11 : 87

وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى

Na atajitenga mbali nayo mpotovu, info

Na atajitenga na ukumbusho mpotovu anaye shikilia kufanya inda na ukafiri.

التفاسير:

external-link copy
12 : 87

ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ

Ambaye atauingia Moto mkubwa. info

Ambaye ataingia kwenye Moto mkubwa ulio andaliwa kuwa ndio malipo yake.

التفاسير:

external-link copy
13 : 87

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ

Tena humo hatakufa wala hawi hai. info

Tena hatokufa huko Motoni akapumzika kwa kifo, wala hawi hai kwa uhai wa kustarehe nao.

التفاسير:

external-link copy
14 : 87

قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ

Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. info

Hakika amefuzu mwenye kujisafisha na ukafiri na maasi.

التفاسير:

external-link copy
15 : 87

وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ

Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali. info

Na akalikumbuka jina la Muumba wake kwa moyo wake na ulimi wake, na akaswali kwa unyenyekevu kama itakikanavyo.

التفاسير:

external-link copy
16 : 87

بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا

Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! info

Bali nyinyi hamfanyi hayo yanayo pelekea kufanikiwa, lakini katika hima zenu mnatanguliza maisha ya duniani kuliko ya Akhera.

التفاسير:

external-link copy
17 : 87

وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ

Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. info

Na Akhera ni bora kuliko dunia, kwa usafi wa neema zake, na ni yenye kubaki na kudumu zaidi.

التفاسير:

external-link copy
18 : 87

إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ

Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, info

Hakika haya yote yaliyo tajwa katika Sura hii bila ya shaka yamethibitishwa katika Vitabu vya zamani,

التفاسير:

external-link copy
19 : 87

صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ

Vitabu vya Ibrahimu na Musa. info

Vitabu vya Ibrahimu na Musa; kwani haya yamewafikiana na mafunzo ya dini zote na yamesajiliwa katika Vitabu vya mbinguni.

التفاسير: