クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Ali Muhsen Alberwany

external-link copy
44 : 4

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ نَصِيبٗا مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ يَشۡتَرُونَ ٱلضَّلَٰلَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّواْ ٱلسَّبِيلَ

Huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wananunua upotovu na wanakutakeni nanyi mupotee Njia? info

Hebu huyastaajabii mambo ya hawa walio pewa sehemu ya Vitabu vilivyo tangulia wanavyo acha uwongofu na wakatafuta upotovu katika mambo yaliyo wakhusu nafsi zao! Na wao tena wanakutakeni nyinyi mjitenge na Haki ambayo ndiyo Njia ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka!

التفاسير: