クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis

ページ番号:close

external-link copy
17 : 79

ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ

«Enda kwa Firauni. Hakika yeye amekiuka mno katika kuasi. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 79

فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ

Ukamwambie, ‘Je, unapendelea kuitakasa nafsi yako na upungufu na kuipamba na imani? info
التفاسير:

external-link copy
19 : 79

وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ

Na nikuelekeze njia ya kumtii Mola wako, upate kumcha na kumuogopa?’» info
التفاسير:

external-link copy
20 : 79

فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ

Mūsā alimuonyesha Firauni alama kubwa: fimbo na mkono. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 79

فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ

Hapo Firauni alimkanusha Nabii wa Mwenyezi Mungu , naye ni Mtume Mūsā, amani imshukie, na alimuasi Mola wake Aliyetukuka. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 79

ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ

Kisha alikengeuka hali ya kuipa mgongo Imani na kufanya bidii katika kumpinga Mūsā. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 79

فَحَشَرَ فَنَادَىٰ

Hapo aliwakusanya raia wa utawala wake na akawaita kwa info
التفاسير:

external-link copy
24 : 79

فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ

kuwaambia,»Mimi ndiye mola wenu ambaye hakuna mola mwengine aliye juu yake.» info
التفاسير:

external-link copy
25 : 79

فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ

Hapo Mwenyezi Mungu Alimtesa kwa adhabu ya duniani na ya Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 79

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ

Na Akaifanya adhabu hiyo iwe ni mazingatio na ni onyo kwa watu mfano wake kati ya wale waasi. Hakika Firauni na kile kilichompata cha adhabu ni mawaidha kwa mwenye kuwaidhika na kutishika. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 79

ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا

Je, kufufuliwa kwenu, enyi watu, baada ya kufa ni kugumu zaidi, katika vipimo vyenu, au ni kuumbwa kwa mbingu? info
التفاسير:

external-link copy
28 : 79

رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا

Amezipanga juu yenu kama jengo. Na Ameinua sakafu yake angani, haina tofauti wala nyufa. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 79

وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا

Na Ameutia giza usiku wake kwa kutwa kwa jua lake. Na Ameweka wazi mchana wake kwa kuchomoza kwake. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 79

وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ

Na ardhi baada ya kuumba mbingu Ameitandaza. Na Ameweka humo manufaa yake. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 79

أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا

Na Ametumbua humo chemchemu za maji. Na Ameotesha humo mimea inayolishwa. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 79

وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا

Na Ameyakita humo majabali yakiwa ni vigingi vyake. Ameumba, Aliyetakasika na kila upungufu, info
التفاسير:

external-link copy
33 : 79

مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ

neema zote hizi zikiwa ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu. (Hakika kurudisha kuumbwa kwenu, Siku ya Kiyama, ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kushinda kuumba viumbe hivyo vyingine. Na vyote hivyo, kwa Mwenyezi Mungu, ni rahisi na ni vipesi). info
التفاسير:

external-link copy
34 : 79

فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ

Pindi kitakapokuja Kiyama Kikubwa na balaa nzito, nao ni Mvuvio wa pili. Kipindi hicho zitaoneshwa kwa binadamu vitendo vyake vyote, za kheri na za shari. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 79

يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ

Hapo atazikumbuka na kuzitambua. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 79

وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ

Na utaoneshwa Moto wa Jahanamu kwa kila aonaye, uwe waonekana waziwazi. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 79

فَأَمَّا مَن طَغَىٰ

Ama yule atakayekiuka amri ya Mwenyezi Mungu info
التفاسير:

external-link copy
38 : 79

وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا

na akapendelea maisha ya ulimwenguni kuliko ya Akhera, info
التفاسير:

external-link copy
39 : 79

فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ

basi kwa kweli marejeo yake ni Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 79

وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ

Na ama yule atakayeogopa kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu kuhesabiwa na akaikanya nafsi yake na matamanio mapotofu, info
التفاسير:

external-link copy
41 : 79

فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ

basi Peponi ndiko makazi yake. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 79

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا

Wanakuuliza washirikina, ewe Mtume, kwa madharau, kuhusu wakati wa kuanzia Kiyama unachowaonya. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 79

فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ

Wewe huna kamwe ujuzi nacho. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 79

إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ

Bali mambo ya ujuzi huo yarejeshwe kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Sifa Tukufu. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 79

إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا

Wewe linalokuhusu katika habari zake ni kumuonya nacho yule anayekiogopa. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 79

كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا

Kama kwamba wao siku watakapouona Kiyama kimesimama, watakuwa hawakukaa katika maisha yao ya duniani, kwa vituko vya hiko Kiyama, isipokuwa ni kama kwamba wamkaa kati ya adhuhuri mpaka kutwa juwa, au ni kama kati ya kuchomoza jua mpaka nusu ya mchana. info
التفاسير: