クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis

Al-Haqqah

external-link copy
1 : 69

ٱلۡحَآقَّةُ

Kiyama chenye kutukia kikweli ambacho ndani yake inahakikika ahadi ya Mwenyezi Mungu na onyo Lake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 69

مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Kiyama chenye kutukia kikweli ni zipi sifa zake na hali zake? info
التفاسير:

external-link copy
3 : 69

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Na kitu gani kilichokujulisha wewe, ewe Mtume, na kukueleza uhakika wa Kiyama na kikakupa wewe picha ya janga lake na shida zake? info
التفاسير:

external-link copy
4 : 69

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ

Thamūd, nao ni watu wa Ṣāliḥ, na ‘Ād, nao ni watu wa Hūd, walikikanusha Kiyama ambacho kinagonga nyoyo kwa vituko janga lake. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 69

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ

Ama hao Thamūd waliangamizwa kwa ukelele mkubwa uliopita kiasi ukali wake, info
التفاسير:

external-link copy
6 : 69

وَأَمَّا عَادٞ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٖ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٖ

na ama‘Ād waliangamizwa kwa upepo baridi unaovuma kwa nguvu. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 69

سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٖ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومٗاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٖ

Mwenyezi Mungu Aliwasaliti nao masiku saba na michana minane yenye kufuatana, isiyokatika wala kusimama. Utawaona watu katika masiku hayo na michana wamekufa, kama kwamba wao ni vigogo mitende iliyo mibovu iliyolika ndani. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 69

فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٖ

Basi je utamuona mtu yoyote miongoni mwao mwenye kusalia bila kuangamia? info
التفاسير:

external-link copy
9 : 69

وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ

Na akaja mpita kiasi katika uasi Fir’awn na ummah waliomtangulia waliokanusha Mitume wao, na watu wakazi wa vijiji vya watu wa Lūṭ ambao majumba yao yaliwapindukia kwa sababu ya kitendo kibaya walichokifanya, cha ukafiri, ushirikina na mambo machafu. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 69

فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةٗ رَّابِيَةً

Kila ummah kati yao walimuasi mjumbe wa Mola wao ambaye alitumwa kwao, basi Mwenyezi Mungu Akawashika mshiko mkali mno. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 69

إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ

Sisi, maji yalipopita kipimo chake, mpaka yakawa juu na kuangatika juu ya kila kitu, tuliwabeba watu wa asili zenu pamoja na Nūḥ ndani ya jahazi ambayo ilikuwa ndio sababu ya kuokoka Waumini na kuzamishwa makafiri, info
التفاسير:

external-link copy
12 : 69

لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةٗ وَتَعِيَهَآ أُذُنٞ وَٰعِيَةٞ

hili likiwa ni mazingatio na mawaidha, na lipate kulihifadhi tukio hilo kila shikio ambalo kazi yake ni kuhifadhi, na lielewe kile ambacho limekisikia. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 69

فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٞ وَٰحِدَةٞ

Pindi Malaika atakapopuliza kwenye barugumu mpulizo mmoja, nao ni mpulizo wa kwanza ambao hapo patapatikana maangamivu ya ulimwengu,. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 69

وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةٗ وَٰحِدَةٗ

Na pindi ardhi na milima itakapoinuliwa kutoka mahali ilipo ikavunjwavunjwa na kugongwagongwa mara moja, info
التفاسير:

external-link copy
15 : 69

فَيَوۡمَئِذٖ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ

Wakati huo Kiyama kitasimama. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 69

وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٖ وَاهِيَةٞ

Na mbingu zitafanya ufa na ziwe dhaifu na kulegea Siku hiyo, hazitakuwa na mshikamano wala ugumu. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 69

وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ ثَمَٰنِيَةٞ

Na Malaika watakuwa kwenye pambizo na pande zake, na wataibeba «Arshi ya Mola wako juu yao Siku ya Kiyama Malaika wanane miongoni mwa Malaika wakubwa. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 69

يَوۡمَئِذٖ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٞ

Katika Siku hiyo, mtaorodheshwa kwa Mwenyezi Mungu, enyi wat, ili mhesabiwe na mlipwe, hakuna chochote kitakachofichamana kwa Mwenyewzi Mungu miongoni mwa siri zenu. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 69

فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ

Ama yule Atakayepewa kitabu cha matendo yake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwa katika hali ya ubashasha na furaha, ‘Chukueni kitabu changu mkisome! info
التفاسير:

external-link copy
20 : 69

إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ

Mimi nilikuwa na yakini duniani kuwa nitapata malipo yangu Siku ya Kiyama, nikajiandalia nayo kwa matayarisho ya Imani na matendo mema.» info
التفاسير:

external-link copy
21 : 69

فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ

Basi yeye atakuwa kwenye maisha ya furaha ya kumridhisha; info
التفاسير:

external-link copy
22 : 69

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ

kwenye Pepo ya juu kimahali na daraja; info
التفاسير:

external-link copy
23 : 69

قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ

matunda yake yako karibu, anayachuma anayesimama, anayeketi na anayelala. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 69

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ

Wataambiwa, «Kuleni na mnyweni kila aina ya vyakula na vinywaji, mkiwa mbali na kila kero, mkiwa mmesalimika na kila mnalolichukia, kwa sababu ya matendo mema mliyoyatanguliza siku za ulimwenguni.» info
التفاسير:

external-link copy
25 : 69

وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ

Na ama yule atakayepewa kitabu cha matendo yake kwa mkono wake wa kushoto, info
التفاسير:

external-link copy
26 : 69

وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ

atasema akiwa katika hali ya kujuta na kupata hasara, info
التفاسير:

external-link copy
27 : 69

يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ

«Natamani lau mimi sikupewa kitabu changu na sikujua malipo yangu! Natamani lau kile kifo nilichokufa duniani kilikuwa ndicho chenye kukata kabisa mambo yangu na nisifufuliwe baada yake! info
التفاسير:

external-link copy
28 : 69

مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ

Mali yangu niliyoyakusanya hayakuninufaisha duniani! info
التفاسير:

external-link copy
29 : 69

هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ

Hoja zangu zote zimenionokea, na sina hoja tena ya kuitumia kama hoja.» info
التفاسير:

external-link copy
30 : 69

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ

Hapo waambiwe walinzi wa Moto wa Jahanamu, «Mchukueni mhalifu huyu mfanya dhambi, ikusanyeni mikono yake shingoni mwake muitie pingu, info
التفاسير:

external-link copy
31 : 69

ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ

kisha mtieni kwenye Moto unaowaka sana, apate kulihisi joto lake. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 69

ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ

Kisha mfungeni mnyororo wa chuma ambao urefu wake ni dhiraa sabini mumkokote nao na mumtie humo. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 69

إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ

Kwani yeye hakuwa akiamini kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa Haki, Peke Yake, Asiye na mshirika. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 69

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Wala hakuwa akitenda matendo yanayoambatana na uongofu Wake, wala hakuwa akiwahimiza watu duniani kuwalisha wenye uhitaji miongoni mwa masikini na wengineo. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 69

فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ

basi kafiri huyu Siku ya Kiyama hatakuwa na jamaa wa karibu wa kumuepushia adhabu, info
التفاسير:

external-link copy
36 : 69

وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ

wala hatakuwa na chakula isipokuwa kile kinachotokana na usaa wa watu wa motoni, info
التفاسير:

external-link copy
37 : 69

لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ

hakuna mwenye kukila isipokuwa wale wenye dhambi, wanaoshikilia kumkanusha Mwenyezi mungu. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 69

فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ

Naapa kwa mnavyoviona miongoni mwa vitu vinavyooonekana, info
التفاسير:

external-link copy
39 : 69

وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ

na vile msivyoviona miongoni mwa vile vilivyoghibu kwenu., hakika Qur’ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 69

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ

Inasomwa na mjumbe mkubwa wa cheo na utukufu. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 69

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ

Na si maneno ya mshairi kama mnavyodai, ni uchache mno mnavyoamini. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 69

وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Wala si tungo kama zile tungo za makuhani, ni kuchache mno kule kukumbuka kwenu na kutia akilini kuwa kuna tafauti baina ya mawili hayo. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 69

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Lakini hiyo Qur’ani ni maneno ya Mola wa viumbe wote Aliyoyateremshia Mtume Wake Muhaammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 69

وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ

Na lau Muhammad angalitusingizia maneno tusiyoyanena info
التفاسير:

external-link copy
45 : 69

لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ

tungalimtesa na tungalimkamata kwa nguvu na uweza, kwani nguvu ya kila kitu iko kwenye upande wake wa kulia, info
التفاسير:

external-link copy
46 : 69

ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ

kisha tungalimkata mshipa wa moyo wake., info
التفاسير:

external-link copy
47 : 69

فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ

hataweza yoyote kuyazuia mateso yetu yasimpate. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 69

وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ

Na hii Qur’ani ni mawaidha kwa wachamungu wanaofuata amri za Mwenyezi Mungu na kuyaepuka makatazo yake. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 69

وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ

Na sisi kwa hakika tunajua kwamba miongoni mwenu kuna wanaoikanusha hii Qur’ani pamoja na kuwa dalili zake ziko wazi. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 69

وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na kwa hakika kuikanusha Qur’ani ni majuto makubwa kwa wenye kuikanusha pindi watakapoiona adhabu yao na kuona starehe za wenye kuiamini. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 69

وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Na kwa hakika hii Qur’ani ni haki iliyothibiti na yakini isiyo na shaka. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 69

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi Mwepushie Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kila sifa isiyonasibiana na haiba Yake, na umtaje kwa jina Lake tukufu. info
التفاسير: