クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis

ページ番号:close

external-link copy
34 : 4

ٱلرِّجَالُ قَوَّٰمُونَ عَلَى ٱلنِّسَآءِ بِمَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ وَبِمَآ أَنفَقُواْ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡۚ فَٱلصَّٰلِحَٰتُ قَٰنِتَٰتٌ حَٰفِظَٰتٞ لِّلۡغَيۡبِ بِمَا حَفِظَ ٱللَّهُۚ وَٱلَّٰتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَٱهۡجُرُوهُنَّ فِي ٱلۡمَضَاجِعِ وَٱضۡرِبُوهُنَّۖ فَإِنۡ أَطَعۡنَكُمۡ فَلَا تَبۡغُواْ عَلَيۡهِنَّ سَبِيلًاۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيّٗا كَبِيرٗا

Wanaume ni wasimamizi wa kuwaelekeza wanawake na kuwatunza, kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu Amewatunuku nacho cha sifa za usimamizi na kutukuzwa, na mahari na matumizi waliyowapa hao wanawake. Basi wale walio wema katika wao, hao wanawake, kwa kuhifadhiwa na Mwenyezi Mungu na kuafikiwa, wanasimama imara kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu, wanamtii Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na wanatunza kila lisilojulikana na waume zao katika mambo waliyoaminiwa nayo. Na wale katika wao mnaochelea kuwafanyia nyinyi ujeuri kwa kuacha kuwatii, wapeni nasaha kwa maneno mazuri; iwapo maneno mazuri hayakuzaa matunda kwao, wahameni vitandani wala msiwakaribie. Iwapo kuwahama hakukuwafanya waathirike na kubadili mwenendo wao, basi wapigeni kipigo kisicho na madhara. Na wakiwa watawatii, jihadharini kuwafanyia maonevu. Kwani Mwenye zi Mungu Aliye juu, Aliye Mkubwa Ndiye Msaidizi wao, na Yeye ni Mwenye kuwalipiza wale waliowadhulumu na kuwaonea. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 4

وَإِنۡ خِفۡتُمۡ شِقَاقَ بَيۡنِهِمَا فَٱبۡعَثُواْ حَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهِۦ وَحَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصۡلَٰحٗا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيۡنَهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرٗا

Na mkijua, enyi wasimamizi wa mume na mke, kuwa kuna ugomvi baina yao unaopelekea kutengana, wapelekeeni mwamuzi muadilifu wa upande wa mume na mwamuzi muadilifu wa upande wa mke, ili watazame na kutoa uamuzi wenye maslahi ya wao wawili. Na kwa kuwa wale waamuzi wawili wana hamu ya kupatanisha na wanatumia njia nzuri, Mwenyezi Mungu Atawatilia taufiki baina ya mume na mke. Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, hakuna chochote kinachofichamana Kwake kuhusu mambo ya waja Wake, ni Mtambuzi wa yaliyomo ndani ya nafsi zao. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 4

۞ وَٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗا وَبِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱلۡجَارِ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡجَارِ ٱلۡجُنُبِ وَٱلصَّاحِبِ بِٱلۡجَنۢبِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخۡتَالٗا فَخُورًا

Na muabuduni Mwenyezi Mungu na mtiini Yeye Peke Yake, wala msimfanyie mshirika katika ustahiki wa kuwa Ndiye Mola na Ndiye Mwenye kuabudiwa, na wafanyieni wema wazazi wawili na mtekeleze haki zao na haki za jamaa wa karibu, na mayatima na wahitaji, na jirani wa karibu na wa mbali, na rafiki wa safari na wa mjini, na msafiri mwenye uhitaji, na waliomilikiwa na nyinyi, wanaume na wanawake. Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi, katika waja Wake, wenye kiburi na kujigamba kwa watu. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 4

ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ وَيَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبُخۡلِ وَيَكۡتُمُونَ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۗ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا

Nao ni wale wanaojizuia kutumia na kutoa kile Alichowaruzuku Mwenyezi Mungu, wakawaamuru wengineo kufanya ubahili, wakazikanusha neema za Mwenyezi Mungu juu yao na wakazificha fadhila Zake na vipewa Vyake. Na tumewaandalia wenye kukanusha adhabu yenye kudhalilisha. info
التفاسير: