クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis

Saba

external-link copy
1 : 34

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُ فِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Shukrani ni za Mwenyezi Mungu kwa sifa Zake ambazo zote ni sifa za ukamilifu, na kwa neema Zake za nje na za ndani za kidini na za kidunia, Ambaye Ana ufalme wa vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, na ni Zake Yeye sifa njema zilizotimia huko Akhera, na Yeye Ndiye Mwenye hekima katika matendo Yake, Aliye Mtambuzi wa mambo ya viumbe Vyake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 34

يَعۡلَمُ مَا يَلِجُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا يَخۡرُجُ مِنۡهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا يَعۡرُجُ فِيهَاۚ وَهُوَ ٱلرَّحِيمُ ٱلۡغَفُورُ

Anakijua kila kinachoingia ardhini miongoni mwa matone ya maji na kinachotoka humo miongoni mwa mimea, madini na maji, na kinachoshuka kutoka juu miongoni mwa mvua, Malaika na Vitabu, na vinavyopanda huko miongoni mwa Malaika na matendo ya waja. Na Yeye Ndiye Mwenye kuwarehemu waja Wake, Hawaharakishii mateso wale wenye kuasi kati yao, ni Mwingi wa msamaha wa dhambi za wenye kutubia Kwake, wenye kujitegemeza Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 34

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَأۡتِينَا ٱلسَّاعَةُۖ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأۡتِيَنَّكُمۡ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِۖ لَا يَعۡزُبُ عَنۡهُ مِثۡقَالُ ذَرَّةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَآ أَصۡغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرُ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ

Na makafiri wenye kukanusha kufufuliwa walisema. «Kiyama hakitatujia.» Sema, ewe Mtume, uwaambie, «Kwani! Ninaapa kwa Mola wangu, kitawajia! Lakini hakuna yoyote anayejua wakati wa kuja kwake isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa visivyoonekana, Ambaye haufichamani Kwake uzito wa kadiri ya chungu mdogo uliyo mbinguni au ardhini, hata mdogo zaidi kuliko huo na hata mkubwa, isipokuwa uko kwenye Kitabu kilichotunzwa, nacho ni Ubao Uliohifadhiwa. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 34

لِّيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ

Ili Awalipe mema wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakamfuata Mtume Wake na wakafanya matendo mema, hao watakuwa na msamaha wa dhambi zao na riziki njema, nayo ni Pepo.» info
التفاسير:

external-link copy
5 : 34

وَٱلَّذِينَ سَعَوۡ فِيٓ ءَايَٰتِنَا مُعَٰجِزِينَ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٞ مِّن رِّجۡزٍ أَلِيمٞ

Na wale wanaotembea katika kuizuia njia ya Mwenyezi Mungu, kuwakanusha Mitume Wake na kuzitangua aya zetu huku wakiteta na Mwenyezi Mungu wakipinga amri Zake, hao watakuwa na adhabu mbaya zaidi na yenye ukali mwingi zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 34

وَيَرَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ هُوَ ٱلۡحَقَّ وَيَهۡدِيٓ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ

Na wale waliopatiwa elimu wanajua kwamba Qur’ani uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako ndiyo haki na kwamba inaongoza kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, Aliye Mshindi Asiyeshindwa wala kuzuiliwa, bali Amekitendesha nguvu kila kitu na Amekishinda, Ndiye Mwenye kusifiwa katika maneno Yake, matendo Yake na Sheria Zake. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 34

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ هَلۡ نَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ يُنَبِّئُكُمۡ إِذَا مُزِّقۡتُمۡ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّكُمۡ لَفِي خَلۡقٖ جَدِيدٍ

Na makafiri wanasema, wakiambiana wao kwa wao kwa njia ya shere, «Je, tuwaoneshe mtu ( wakimkusudia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie) atakayewaambia kwamba nyinyi mkifa na miili yenu ikawa mbalimbali kabisa kuwa nyinyi mtahuishwa na mtafufuliwa kutoka makaburini mwenu» wanasema hayo kwa kupita kiasi katika kukanusha kwao. info
التفاسير: