クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis

ページ番号:close

external-link copy
55 : 33

لَّا جُنَاحَ عَلَيۡهِنَّ فِيٓ ءَابَآئِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآئِهِنَّ وَلَآ إِخۡوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآءِ إِخۡوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآءِ أَخَوَٰتِهِنَّ وَلَا نِسَآئِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُنَّۗ وَٱتَّقِينَ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدًا

Hakuna dhambi kwa wanawake kutojifinika mbele ya baba zao, wana wao wa kiume,ndugu zao wa kiume, wana wa kiume wa ndugu zao wa kiume, wana wa kiume wa ndugu zao wa kike, wanawake waumini na watumwa waliomilikiwa na wao kwa kuwa wanahitaji utumishi wao sana. Na muogopeni Mwenyezi Mungu , enyi wanawake, msipite mpaka mliowekewa mkaonyesha pambo lenu msiofaa kulionyesha, au mkaacha kujifinika mbele ya yule ambaye ni lazima mjifinike mbele yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu, Anashuhudia matendo ya waja , ya nje na ya ndani, na Atawalipa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 33

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِيِّۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ صَلُّواْ عَلَيۡهِ وَسَلِّمُواْ تَسۡلِيمًا

Hakika Mwenyezi Mungu Anamsifu Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, mbele ya Malaika waliokurubishwa. Na Malaika Wake wanamsifu Nabii na wanamuombea Mwenyezi Mungu, basi enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, mswalieni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mtakieni amani, kwa kumwamkia na kumtukuza. Na namna ya kumswalia Nabii, rehema na amani zimshukie, imethibiti kwenye Sunnah kwa aina mabalimbali, miongoni mwazo ni: «Ewe Mola! Mrehemu Muhammad na watu wa Muhammad, kama ulivyowarehemu watu wa Ibrāhīm, hakika wewe ni Mwingi wa kushukuriwa ni Mwingi wa kutukuzwa. Ewe Mola! Mbariki Muhammad na watu wa Muhammad kama ulivyowabariki watu wa Ibrāhīm, hakika wewe ni Mwingi wa kushukuriwa, ni Mwingi wa kutukuzwa.» info
التفاسير:

external-link copy
57 : 33

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمۡ عَذَابٗا مُّهِينٗا

Hakika ya wale wanaomuudhi Mwenyezi Mungu kwa kumshirikisha na kufanya maasia mengine, na wakamuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa maneno na vitendo, Mwenyezi Mungu atawafukuza na Atawaweka mbali na kheri duniani na Akhera, na Amewaandalia, huko Akhera, adhabu kali yenye kuwadhalilisha na kuwafanya wanyonge. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 33

وَٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ بِغَيۡرِ مَا ٱكۡتَسَبُواْ فَقَدِ ٱحۡتَمَلُواْ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا

Na wale wenye kuwaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike kwa maneno au vitendo bila ya kosa walilolifanya, basi watakuwa wametenda tendo la urongo na uzushi mbaya kabisa, na wamefanya kosa chafu waziwazi, ambalo kwalo watastahili kupewa adhabu huko Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 33

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ قُل لِّأَزۡوَٰجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَآءِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ يُدۡنِينَ عَلَيۡهِنَّ مِن جَلَٰبِيبِهِنَّۚ ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن يُعۡرَفۡنَ فَلَا يُؤۡذَيۡنَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Ewe Nabii! Waambie wake zako, watoto wako wa kike na wanawake Waumini wateremshe juu ya vichwa vyao na nyuso zao mashuka yao na mitandio yao, ili kufinika nyuso zao, vifua vyao na vichwa vyao. Kufanya hivyo kuko karibu zaidi kuwafanya wao watenganishwe kwa kusitirika na kuhifadhika, wasiwe ni wenye kusumbuliwa kwa kukerwa wala kuudhiwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na kurehemu kwa kuwa Amewasamehe yaliyopita na Akawarehemu kwa kuwabainishia halali na haramu. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 33

۞ لَّئِن لَّمۡ يَنتَهِ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡمُرۡجِفُونَ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لَنُغۡرِيَنَّكَ بِهِمۡ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَآ إِلَّا قَلِيلٗا

Wasipokomeka, wale wanaoficha ukafiri na kudhihirisha Imani, wale ambao ndani ya nyoyo zao muna shaka na wasiwasi na wale wanaoeneza habari za urongo katika mji wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na mabaya yao na shari zao, tutakupa uwezo juu yao, kisha hawatakaa pamoja na wewe humo isipokuwa muda mchache. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 33

مَّلۡعُونِينَۖ أَيۡنَمَا ثُقِفُوٓاْ أُخِذُواْ وَقُتِّلُواْ تَقۡتِيلٗا

Hali ya kuwa wamefukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu; mahali popote watakapopatikana watekwe na wawe ni wenye kuuawa muda wa kuendelea kwao katika unafiki na kueneza habari za urongo baina ya Waislamu kwa lengo la kuleta fitina na uharibifu. info
التفاسير:

external-link copy
62 : 33

سُنَّةَ ٱللَّهِ فِي ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلُۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ ٱللَّهِ تَبۡدِيلٗا

Huu ndio mpango wa Mwenyezi Mungu na njia Yake kuhusu ummah waliopita, ni kuwa watekwe na wawe ni wenye kuuawa popote waliopo. Na hutapata , ewe Nabii, mageuzi wala mabadiliko katika njia ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير: