[86] Wala msikae katika kupinga kila njia za Haki na uwongofu na a'mali njema, mkiwatishia wapitao, na kwa hivyo mkawazuia watafutao kheri wasiifikie. Nao hao ndio watu wa Imani wanao muamini Mwenyezi Mungu, nanyi mnaitaka njia iliyo potoka! Na kumbukeni mlivyo kuwa ni watu wachache, Mwenyezi Mungu akakufanyeni mkawa wengi kwa kwenda sawa kutaka uzazi na mali. Na zingatieni nini ulikuwa mwisho wa waharibifu walio kuwa kabla yenu.