Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

external-link copy
186 : 7

مَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَا هَادِيَ لَهُۥۚ وَيَذَرُهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Aliye mwacha Mwenyezi Mungu kupotea hana wa kumwongoa. Atawaacha hao wakitangatanga katika upotofu wao. info

Aliye andikiwa na Mwenyezi Mungu kupotea kwa uwovu wa uchaguzi wake mwenyewe, basi hapana mtu wa kumhidi. Na Yeye Subhana, Aliye takasika, anawaacha watu kama hao wakihangaika wala hawaitambui njia.

التفاسير: