Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

external-link copy
180 : 7

وَلِلَّهِ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ فَٱدۡعُوهُ بِهَاۖ وَذَرُواْ ٱلَّذِينَ يُلۡحِدُونَ فِيٓ أَسۡمَٰٓئِهِۦۚ سَيُجۡزَوۡنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda. info

Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye Majina yenye kuonyesha sifa za ukamilifu. Basi mtumilieni hayo mnapo muomba, au mnapo mwita au kumtaja. Na waepukeni hao wanao mili katika hayo yasiyo elekeana na dhati ya utukufu wake. Hao watakuja lipwa malipo ya vitendo vyao.

التفاسير: