Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

external-link copy
168 : 7

وَقَطَّعۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ أُمَمٗاۖ مِّنۡهُمُ ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنۡهُمۡ دُونَ ذَٰلِكَۖ وَبَلَوۡنَٰهُم بِٱلۡحَسَنَٰتِ وَٱلسَّيِّـَٔاتِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ

Na tuliwafarikisha katika ardhi makundi makundi. Wako kati yao walio wema, na wengine kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mema na mabaya ili wapate kurejea. info

Na Sisi tumewagawa makundi makundi duniani. Wamo kati yao walio wema. Na hao ndio walio amini wakenda mwendo ulio sawa. Na wapo miongoni mwao watu wasio sifika kwa wema. Na wote tumewafanyia mitihani kwa kuwapa neema na kuwapa nakama, ili watubu, waache waliyo katazwa.

التفاسير: