Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

external-link copy
167 : 7

وَإِذۡ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبۡعَثَنَّ عَلَيۡهِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَن يَسُومُهُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِۗ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na pale alipo tangaza Mola wako Mlezi kwamba hapana shaka atawaletea watu ambao watawaadhibu kwa adhabu mbaya mpaka Siku ya Kiyama. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na Mwenye kurehemu. info

Na wakumbushe pia hao Mayahudi pale alipo wajuvya Mola Mlezi wako wenzao walio watangulia kwa ndimi za Manabii wao: Mwenyezi Mungu atawasalitisha Mayahudi mpaka Siku ya Kiyama adhabu mbaya kabisa kwa sababu ya dhulma yao na upotovu wao. Kwani Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuwaadhibu watu makafiri, kwani adhabu yake itakuja tu bila ya shaka yoyote. Na kila kijacho kipo karibu, (chambilecho Waarabu). Na Yeye Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu kwa anaye rejea kwake akatubu.

التفاسير: