[37] Na Musa alisema kumjibu Firauni na kaumu yake: Mola wangu Mlezi anajua kwa hakika kuwa mimi nimeleta Ishara hizi zenye kuonyesha Haki na Uwongofu kutokana naye Yeye. Basi Yeye ndiye shahidi wangu kwa haya, ikiwa nyinyi mnanikadhibisha. Na Yeye anajua kuwa mwisho mwema ni wetu sisi watu wa Haki. Hakika makafiri hawapati kheri.