Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

An-Nahl

external-link copy
1 : 16

أَتَىٰٓ أَمۡرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسۡتَعۡجِلُوهُۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiihimize. Ametakasika na Ametukuka na wanayo mshirikisha nayo. info

Enyi washirikina! Kuweni na yakini kwamba aliyo kuahidini Mwenyezi Mungu kuwa yatakuwa Siku ya Kiyama yapo karibu kutokea bila ya shaka. Basi msifanye maskhara kwa kuyahimiza yatokee. Mwenyezi Mungu ametakasika na kuwa na mshirika wa kuabudiwa badala yake. Na hiyo miungu mnayo mshirikisha naye haiwezi jambo lolote.

التفاسير:

external-link copy
2 : 16

يُنَزِّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرُوٓاْ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ

Huwateremsha Malaika na Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake ili nyinyi muonye kwamba hapana mungu ila Mimi, basi nicheni Mimi. info

Mwenyezi Mungu huteremsha Malaika kwa yanayo huisha nyoyo katika Wahyi wake (ndio hiyo Roho) juu ya anaye mkhiari kumpa Utume katika waja wake, ili watu wajue kwamba hapana mungu wa kuabudiwa kwa Haki ila Mimi. Basi jitengeni na yanayo nikasirisha na yatayo kuleteeni adhabu. Na shikamaneni na ut'iifu ili ukukingeni na adhabu.

التفاسير:

external-link copy
3 : 16

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ تَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Ametukuka na wanayo shirikisha. info

Yeye ameumba mbingu na ardhi kwa mujibu wa hikima. Ametakasika kuwa na mshirika wa kufanya lolote katika utawala wake, au wa kuabudiwa kama Yeye.

التفاسير:

external-link copy
4 : 16

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٖ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٞ مُّبِينٞ

Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri. info

Amemuumba kila mmoja katika wanaadamu kutokana na maji maji yasiyo shikamana, nayo ni manii. Kutokana na hayo ndio anakuwa mtu mwenye nguvu za kujitetea nafsi yake, mshindani na makhasimu zake, mwenye kuweka wazi hoja zake.

التفاسير:

external-link copy
5 : 16

وَٱلۡأَنۡعَٰمَ خَلَقَهَاۖ لَكُمۡ فِيهَا دِفۡءٞ وَمَنَٰفِعُ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ

Na nyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa vya kutia joto,na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala. info

Enyi waja! Mwenyezi Mungu amekufadhilini - amekuumbieni nyama hoa, wanyama wa kufuga, kama ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, ili mpate kutokana na sufi zao na manyoa yao vifaa vya kukupatieni joto kujihifadhi na baridi, na mle nyama yao mhifadhi uhai wenu.

التفاسير:

external-link copy
6 : 16

وَلَكُمۡ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسۡرَحُونَ

Na wanakupeni furaha pale mnapo warudisha jioni na mnapo wapeleka malishoni asubuhi. info

Na mnapata kwao raha na furaha mnapo waona wanarejea kutoka machungani na matumbo yao na viwele vimejaa, na mnapo toka nao kwenda makondeni na machungani wakikimbilia malisha yao.

التفاسير: