Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

Al-Humazah

external-link copy
1 : 104

وَيۡلٞ لِّكُلِّ هُمَزَةٖ لُّمَزَةٍ

Ole wake kila safihi, msengenyaji! info

Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.

التفاسير:

external-link copy
2 : 104

ٱلَّذِي جَمَعَ مَالٗا وَعَدَّدَهُۥ

Aliye kusanya mali na kuyahisabu. info

Ambaye amekusanya chungu ya mali na akawa kazi yake kuyahisabu tu, kwa kuona ladha huko kuhisabu.

التفاسير:

external-link copy
3 : 104

يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ

Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! info

Anadhani huyo kuwa mali yake yatamweka milele duniani, na yatamkinga na hayo anayo yachukia?

التفاسير:

external-link copy
4 : 104

كَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ

Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama. info

Na aache dhana hiyo! Wallahi! Hapana shaka yoyote kwa vitendo vyake viovu hivyo atakuja tumbukizwa katika Moto unao vuruga kila kinacho tupwa humo!

التفاسير:

external-link copy
5 : 104

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ

Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? info

Na kitu gani kitacho kujuvya nini ukweli wa Moto huu wa H'ut'ama?

التفاسير:

external-link copy
6 : 104

نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ

Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. info

Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa kwa amri yake, na daima unawaka!

التفاسير:

external-link copy
7 : 104

ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ

Ambao unapanda nyoyoni. info

Ambao unafikilia nyoyoni na kuzizunguka nyoyo.

التفاسير:

external-link copy
8 : 104

إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةٞ

Hakika huo utafungiwa nao info

Huo utakuwa umefungwa milango yake, na wao watakuwa wamefungwa humo ndani

التفاسير:

external-link copy
9 : 104

فِي عَمَدٖ مُّمَدَّدَةِۭ

Kwenye nguzo zilio nyooshwa. info

Kwenye maguzo yaliyo nyooka. Hawawezi kutaharaki, wala kutoka.

التفاسير: