Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Numero di pagina: 170:151 close

external-link copy
160 : 7

وَقَطَّعۡنَٰهُمُ ٱثۡنَتَيۡ عَشۡرَةَ أَسۡبَاطًا أُمَمٗاۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ إِذِ ٱسۡتَسۡقَىٰهُ قَوۡمُهُۥٓ أَنِ ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡحَجَرَۖ فَٱنۢبَجَسَتۡ مِنۡهُ ٱثۡنَتَا عَشۡرَةَ عَيۡنٗاۖ قَدۡ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٖ مَّشۡرَبَهُمۡۚ وَظَلَّلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلۡغَمَٰمَ وَأَنزَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰۖ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Na tuliwagawa watu wa Mūsā miongoni mwa Wana wa Isrāīl makabila kumi na mbili, kwa idadi ya Asbāṭ- wana wa Ya’qūb-, kila kabila ikajulikana kupitia kiongozi wake. Na tulimpelekea wahyi Mūsā, walipotaka watu wake kwake maji ya kunywa waliposhikwa na kiu katika kuzunguka kwao, tukamwambia, «Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako.» Akalipiga na pakabubujika chemchemi za maji sehemu kumi na mbili, na watu wa kila kabila, miongoni mwa yale makabila kumi na mbili, walijua mahali pao pa kunywa, hakuna kabila litakaloingia sehemu ya kunywa ya kabila lingine. Na tukawafinika kiwingu juu yenu, na tukawateremshia mann- kitu kinachofanana na gundi chenye ladha kama ya asali- na salwā- ndege wanaofanana na wale wanaoitwa sumānā (tomboro), na tukawaambia, «Kuleni vitu vizuri tulivyowaruzuku.» Walivichukia na kuvichoka hivyo kwa muda mrefu wa kuvitumia na wakasema, «Hatutavumilia juu ya chakula kimoja.» Na wakataka kubadilishiwa kizuri walichonacho kwa ambacho ni kiovu. Na wao hawakutudhulumu sisi walipoacha kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuacha kusimama na yale Aliyoyalazimisha Mwenyezi Mungu juu yao, lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao, kwa kuwa walizikosesha kila jema na kuzipeleka kwenye shari na mateso. info
التفاسير:

external-link copy
161 : 7

وَإِذۡ قِيلَ لَهُمُ ٱسۡكُنُواْ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةَ وَكُلُواْ مِنۡهَا حَيۡثُ شِئۡتُمۡ وَقُولُواْ حِطَّةٞ وَٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا نَّغۡفِرۡ لَكُمۡ خَطِيٓـَٰٔتِكُمۡۚ سَنَزِيدُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na kumbuka, ewe Mtume, uasi kwa Wana wa Isrāīl Mola wao, kutakata na sifa pungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, na Nabii wao Mūsā, amani imshukiye, na kugeuza kwao maneno waliyoamrishwa wayaseme pindi Alipowaambia Mwenyezi Mungu, «kaeni mji wa Baitul Maqdis na kuleni matunda yake, nafaka zake na mimea yake popote mtakapo na wakati wowote mtakao na semeni, ‘tuondoshee dhambi zetu,’ na ingieni mlangoni mkimnyenyekea Mwenyezi Mungu, tutawasamehe makosa yenu na hatutawaadhibu kwayo, na tutawaongezea walio wema kheri mbili: za ulimwengu na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
162 : 7

فَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ قَوۡلًا غَيۡرَ ٱلَّذِي قِيلَ لَهُمۡ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَظۡلِمُونَ

Waliomkanusha Mwenyezi Mungu kati yao waliligeuza neno ambalo Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha waliseme, wakaingia mlangoni wakijikokota kwa matako yao na wakasema, «habbah fī sha'rah» (mbegu kwenye unywele), hapo tukawateremshia adhabu kutoka mbinguni, tukawaangamiza kwayo, kwa sababu ya udhalimu wao na uasi wao. info
التفاسير:

external-link copy
163 : 7

وَسۡـَٔلۡهُمۡ عَنِ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِي كَانَتۡ حَاضِرَةَ ٱلۡبَحۡرِ إِذۡ يَعۡدُونَ فِي ٱلسَّبۡتِ إِذۡ تَأۡتِيهِمۡ حِيتَانُهُمۡ يَوۡمَ سَبۡتِهِمۡ شُرَّعٗا وَيَوۡمَ لَا يَسۡبِتُونَ لَا تَأۡتِيهِمۡۚ كَذَٰلِكَ نَبۡلُوهُم بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ

Na waulize, ewe Mtume, hawa Mayahudi kuhusu habari ya watu wa kijiji kilichokuwa karibu ya bahari, ambacho watu wake walikuwa wakipita mipaka siku ya Jumamosi kwa kufanya mambo yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, kwani Alikuwa Amewaamrisha waitukuze siku ya Jumamosi na wasivue samaki siku hiyo. Mwanyezi Mungu Akawajaribu na kuwapa mtihani, wakawa samaki wao wawajia siku ya Jumamosi kwa wingi wakiwa juu ya uso wa bahari, na Jumamosi ikipita wakawa samaki wanapotea na hawawaoni kabisa. Basi wakawa wafanya hila ya kuwatega siku ya Jumamosi kwenye mashimo na kuwavua baada yake. Na kama tulivyowaelezea vile Mwenyezi Mungu Alivyowajaribu na kuwapa mtihani kwa kuwatoa samake juu ya bahari katika siku ambayo waliharamishiwa kuwavua na kuwaficha wasiwaone katika siku ambazo ni halali kwao kuwavua, ndivyo tunavyowafanyia mtihani wao kwa sababu ya uasi wao na kutoka kwao kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير: