Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Al-Hashr

external-link copy
1 : 59

سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Vimemtakasa Mwenyezi Mungu na kumuepusha na kila kisichonasibiana na Yeye, vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, na Yeye Ndiye Mshindi Asiyekuwa na mwenye kushindana na Yeye, Mwingi wa hekima katika makadirio Yake, uendeshaji Wake na utengezaji Wake na Sheria Zake, Anaweka kila jambo mahali pake panapostahiki. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 59

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ مِن دِيَٰرِهِمۡ لِأَوَّلِ ٱلۡحَشۡرِۚ مَا ظَنَنتُمۡ أَن يَخۡرُجُواْۖ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمۡ حُصُونُهُم مِّنَ ٱللَّهِ فَأَتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِنۡ حَيۡثُ لَمۡ يَحۡتَسِبُواْۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلرُّعۡبَۚ يُخۡرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيۡدِيهِمۡ وَأَيۡدِي ٱلۡمُؤۡمِنِينَ فَٱعۡتَبِرُواْ يَٰٓأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ

Yeye, kutakasika ni Kwake, Ndiye Aliyewatoa wale walioukanusha unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, miongoni mwa watu waliopewa Kitabu, nao ni Mayahudi wa ukoo wa Banū al Nadīr, kutoka majumbani mwao ambayo wakiwa humo walikuwa ni majirani na Waislamu pambizoni mwa Madina. Huko kulikuwa ndio mwanzo wa kutolewa nje ya Bara Arabu hadi Shām. Hamkudhani, enyi Waislamu, kuwa watatoka majumbani mwao kwa unyonge huu na utwevu, kwa silaha kali waliokuwa nazo na hifadhi ya nguvu waliokuwa nayo. Na walidhani Mayahudi kuwa ngome zao zitawakinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwa hakuna anayeziweza. Basi amri ya Mwenyezi Mungu ilizijilia kwa namna ambayo haikupita kwenye akili zao, na Mwenyezi Mungu Akawatia hofu na kicho kikubwa, wakawa wanazivunja nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini, basi zingatieni, enyi wenye busara timamu na akili nyingi kwa hayo yaliyowafika wao. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 59

وَلَوۡلَآ أَن كَتَبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡجَلَآءَ لَعَذَّبَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابُ ٱلنَّارِ

Na lau si Mwenyezi Mungu kupitisha na kuamua kuwa wao watoke majumbani mwao, Angaliwaadhibu duniani kwa kuuawa na kutekwa, na huko Akhera watakuwa na adhabu ya Motoni. info
التفاسير: