Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Adh-Dhariyat

external-link copy
1 : 51

وَٱلذَّٰرِيَٰتِ ذَرۡوٗا

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anaapa kwa upepo wenye kurusha mchanga, info
التفاسير:

external-link copy
2 : 51

فَٱلۡحَٰمِلَٰتِ وِقۡرٗا

na mawingu yenye kubeba uzito mkubwa wa maji, info
التفاسير:

external-link copy
3 : 51

فَٱلۡجَٰرِيَٰتِ يُسۡرٗا

na jahazi zinazopita baharini na kutembea kwa upesi na usahali, info
التفاسير:

external-link copy
4 : 51

فَٱلۡمُقَسِّمَٰتِ أَمۡرًا

na Malaika wenye kugawanya amri za Mwenyezi Mungu kwa viumbe Vyake, info
التفاسير:

external-link copy
5 : 51

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٞ

kwamba mnayoahidiwa, enyi watu, ya kufufuliwa na kuhesabiwa ni tukio lenye kuwa kwa kweli na yakini, info
التفاسير:

external-link copy
6 : 51

وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٞ

na kwamba kuhesabiwa na kulipwa mema kwa amali njema ni jambo lisilo na budi. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 51

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡحُبُكِ

Na Anaapa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa mbingu zenye umbo zuri, kwamba nyinyi, enyi wakanushaji, info
التفاسير:

external-link copy
8 : 51

إِنَّكُمۡ لَفِي قَوۡلٖ مُّخۡتَلِفٖ

mko kwenye neno linalogongana kuhusu Qur’ani na kuhusu Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 51

يُؤۡفَكُ عَنۡهُ مَنۡ أُفِكَ

Anaepushwa na Qur’ani na Mtume yule aliyeepushwa na lile la kuviamini hivyo viwili kwa kuzipa mgongo dalili za Mwenyezi Mungu na hoja Zake za yakini, na kwa hivyo haafikiwi kwenye kheri. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 51

قُتِلَ ٱلۡخَرَّٰصُونَ

Wamelaaniwa warongo wenye dhana zisizo za kweli, info
التفاسير:

external-link copy
11 : 51

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي غَمۡرَةٖ سَاهُونَ

waliomo ndani ya dimbwi la ukafiri na upotevu hali ya kuwa wameghafilika na kujikita kwenye ubatilifu wao. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 51

يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Wanauliza hawa wenye kukanusha suali la kuonyesha kuwa ni jambo lisilowezekana na la kuonyesha ukanushaji, «Ni lini Siku ya kuhesabiwa na kulipwa?» info
التفاسير:

external-link copy
13 : 51

يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ

Siku ya Malipo ni Siku ya wao kuadhibiwa kwa kuchomwa kwa Moto na waambiwe, info
التفاسير:

external-link copy
14 : 51

ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ

«Onjeni adhabu yenu ambayo mlikuwa mkiifanyia haraka duniani.» info
التفاسير:

external-link copy
15 : 51

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ

Hakika ya wale wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo makubwa na chemchemi za maji yenye kutembea. Mwenyezi Mungu Atawapa yote wanayoyatamani ya aina mbalimbali za starehe. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 51

ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ

Watazipokea neema hizo wakiwa wameridhika nazo na nafsi zao zina furaha. Hakika wao, kabla ya kupata sterehe hizo, walikuwa wema duniani kwa matendo yao mema. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 51

كَانُواْ قَلِيلٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ

Wema hawa walikuwa wakilala kipindi kichache usiku, wakiswali kwa Mola wao wakimnyenyekea, info
التفاسير:

external-link copy
18 : 51

وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ

na katika nyakati za mwisho wa usiku, kabla ya alfajiri kwa muda mchache, walikuwa wakimuomba Mwenyezi Mungu msamaha wa dhambi zao. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 51

وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ

Na katika mali yao kulikuwa na haki ya lazima na ya kupendekezwa kupewa wahitaji wanaowaomba watu na wasiowaomba kwa kuona haya. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 51

وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتٞ لِّلۡمُوقِنِينَ

Na katika ardhi kuna mazingatio na dalili waziwazi za uweza wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, Aliye Peke Yake na asiye na mshirika, na wenye kumuamini Mtume Wake. rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 51

وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ

Na katika kuwaumba nyinyi kuna dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na kuna mazingatio ya kuwaonyesha nyinyi upweke wa Muumba wenu na kwamba Yeye hakuna Mola Anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Je, mumeghafilika na hilo mkawa hamlioni mkazingatia kwalo? info
التفاسير:

external-link copy
22 : 51

وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ

Na mbinguni kuna riziki yenu na yale mnayoahidiwa ya kheri na shari, na thawabu na mateso na yasiyokuwa hayo. Yote yameandikwa na kukadiriwa. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 51

فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقّٞ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa dhati Yake tukufu kwamba kile Alichowaahidi ni kweli, msikifanyie shaka kama ambavyo hamshuku kuwa nyinyi mnasema. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 51

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ

Je imekujia wewe, ewe Mtume, habari ya wageni wa Ibrāhīm aliyewakirimu info
التفاسير:

external-link copy
25 : 51

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ

na walikuwa ni miongoni mwa Malaika watukufu- wakati walipomjia nyumbani kwake, wakamwamkia kwa kumwambia, «Salama!»Akawarudishia maamkizi kwa kusema, «Salama ni kwenu! Nyinyi ni watu wageni hatuwajui.» info
التفاسير:

external-link copy
26 : 51

فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٖ سَمِينٖ

Akaondoka kwa siri na akaelekea kwa watu wa nyumbani kwake akamlenga ndama mnono akamchinja, akamchoma info
التفاسير:

external-link copy
27 : 51

فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ

kisha akamuweka mbele yao na akawakaribisha kwa upole kwa kusema, «Si mle». info
التفاسير:

external-link copy
28 : 51

فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ

Alipowaona hawali aliingiwa na kicho cha kuwaogopa, na hapo wakamwambia, «Usiogope! Sisi ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu. Na wakampa bishara kwamba mkewe Sarah atamzalia mtoto atakayekuwa ni miongoni mwa watu wanaomjua Mwenyezi Mungu na kuijua Dini Yake, naye ni Isḥāq, amani imshukie. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 51

فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةٖ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٞ

Aliposikia mke wa Ibrāhīm maneno ya bishara ya hao Malaika, alielekea upande wao na ukelele, akajipiga uso wake kwa kulionea ajabu jambo hili na akasema, «Vipi nitazaa na mimi ni tasa sizai?» info
التفاسير:

external-link copy
30 : 51

قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ

Malaika wa Mwenyezi Mungu wakamwambia, «Hivyo ndivyo Alivyosema Mola wako kama tulivyokwambia. Na Yeye Muweza wa hilo, hapana la ajabu kutokana na uweza Wake. Hakika Yeye, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Mwenyew hekima Anayeviweka vitu mahali pake, Ndiye Mwenye kuyajua maslahi ya waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 51

۞ قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ

Akasema Ibrāhīm, amani imshukie, kuwaambia Malaika wa Mwenyezi Mungu «Mna jambo gani na mmetumwa na ujumbe gani? info
التفاسير:

external-link copy
32 : 51

قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ

Wakasema, «Mwenyezi Mungu Ametutuma tuende kwa watu waliofanya uhalifu kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu, info
التفاسير:

external-link copy
33 : 51

لِنُرۡسِلَ عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن طِينٖ

ili tuwaangamize kwa mawe ya udongo uliokuwa mkavu kama mawe, info
التفاسير:

external-link copy
34 : 51

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُسۡرِفِينَ

uliotiwa alama kutoka kwa Mola wako ya hawa waliokiuka mpaka katika uchafu na uasi. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 51

فَأَخۡرَجۡنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Tukamtoa kila aliyekuwa kwenye mji wa watu wa Lūṭ katika watu walioamini. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 51

فَمَا وَجَدۡنَا فِيهَا غَيۡرَ بَيۡتٖ مِّنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

Hatukupata kwenye mji huo isipokuwa nyumba moja ya Waislamu, nayo ni nyumba ya Lūṭ, amani imshukie. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 51

وَتَرَكۡنَا فِيهَآ ءَايَةٗ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ

Na tukaacha kwenye mji huo uiliotajwa athari iliyosalia ya adhabu iwe ni alama ya uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na vile alivyowatesa makafiri. Ili hilo liwe ni zingatio kwa wale wanaoiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyo kali na yenye kuumiza. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 51

وَفِي مُوسَىٰٓ إِذۡ أَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ

Na katika kumtumiliza kwetu Mūsā, aende kwa Fir'awn na wakuu wa utawala wake, kwa aya na miujiza yenye kushinda, kuna alama kwa wanaoogopa adhabu kali. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 51

فَتَوَلَّىٰ بِرُكۡنِهِۦ وَقَالَ سَٰحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٞ

Fir'awn akayapa mgongo akighurika nguvu zake na wasaidizi wake na akasema kuhusu Mūsā, «Yeye ni mchawi au ni mwendawazimu,» info
التفاسير:

external-link copy
40 : 51

فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٞ

Tukamchukua Fir'awn na askari wake tukawatupa baharini, na hali ameleta jambo la kulaumiwa kwa sababu ya ukafiri wake, kukanusha kwake na ubaya wake. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 51

وَفِي عَادٍ إِذۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلۡعَقِيمَ

Na kuhusu mambo ya watu wa kabila la 'Ād na kuwaangamiza wao kuna dalili na mazingatio kwa mwenye kutia mambo akilini, tulipowapelekea wao upepo usiokuwa na baraka na usioleta kheri yoyote, info
التفاسير:

external-link copy
42 : 51

مَا تَذَرُ مِن شَيۡءٍ أَتَتۡ عَلَيۡهِ إِلَّا جَعَلَتۡهُ كَٱلرَّمِيمِ

hauachi kitu chochote unachokipitia isipokuwa hukifanya ni kama kitu kilichochakaa. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 51

وَفِي ثَمُودَ إِذۡ قِيلَ لَهُمۡ تَمَتَّعُواْ حَتَّىٰ حِينٖ

Na kuhusu watu wa kabila la Thamūd na kuangamizwa kwao kuna dalili na mazingatio, walipoambiwa-na msemaji hapa ni Nabii wao Ṣāliḥ, amani imshukie-, «Jistarehesheni mjini kwenu siku tatu mpaka muda wenu wa kuishi ukome. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 51

فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ

Wakaasi amri ya Mola wao, wakapatikana na ukelele wa adhabu, na huku wanayaangalia mateso yao kwa macho yao. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 51

فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مِن قِيَامٖ وَمَا كَانُواْ مُنتَصِرِينَ

Haikumkinika wao kukimbia wala kusimama kwa adhabu waliokuwa nayo, na hawakuwa ni wenye kujitetea nafsi zao. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 51

وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ

Na tuliwaangamiza watu wa Nūḥ kabla ya hawa, hakika wao walikuwa ni watu wenye kuenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kutoka nje ya utiifu Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 51

وَٱلسَّمَآءَ بَنَيۡنَٰهَا بِأَيۡيْدٖ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ

Na mbingu tuliziumba na tukazitengeneza vizuri, na tukazifanya ni sakafu ya ardhi kwa nguvu na uweza mkubwa, na sisi tutayapanua maeneo yake na pande zake. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 51

وَٱلۡأَرۡضَ فَرَشۡنَٰهَا فَنِعۡمَ ٱلۡمَٰهِدُونَ

Na ardhi tuliifanya ni tandiko la viumbe wapate kutulia juu yake, Basi bora wa wenye kutandika ni sisi. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 51

وَمِن كُلِّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

Na kutokana na kila kitu katika jinsi ya vitu vilivyoko tumeumba aina mbili tafauti, ili mjikumbushe uweza wa Mwenyezi Mungu na mzingatie. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 51

فَفِرُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Basi kimbieni, enyi watu , kutoka kwenye mateso ya Mwenyezi Mungu na muelekee kwenye rehema Yake kwa kumuamini Yeye na Mtume Wake, kufuata amri Yake na kufanya mambo ya utiifu Kwake. Hakika mimi, kwenu nyinyi, ni muonyaji ambaye maonyo yake yako waziwazi. Na Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alikuwa akizungukwa na mambo hukimbilia Swala, na huku ndiko kumkimbilia Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 51

وَلَا تَجۡعَلُواْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Na msimfanye pamoja na Mwenyezi Mungu muabudiwa mwingine, Hakika mimi kwenu nyinyi ni muonyaji amabaye uonyaji wake uko waziwazi. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 51

كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُواْ سَاحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٌ

Kama walivyomkanusha Makureshi Mtume wao Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakasema, «Yeye ni mshairi, au mchawi, au mwendawazimu.», ndivyo walivyofanya ummah waliowakanusha Mitume wao kabla ya Makureshi, na Mwenyezi Mungu Akawashushia mateso Yake. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 51

أَتَوَاصَوۡاْ بِهِۦۚ بَلۡ هُمۡ قَوۡمٞ طَاغُونَ

Je, waliusiana wa mwanzo na wa mwisho kumkanusha Mtume waliposema hivyo kwa umoja wao? Bali wao ni watu wenye kukiuka mipaka kwa uhalifu, nyoyo zao zimefanana na vitendo vyao kwa ukafiri na ukiukaji mipaka, ndipo waliokuja nyuma wakasema hayo kama walivyosema waliotangulia. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 51

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٖ

Wapuuze hao washirikina, ewe Mtume, mpaka itakapokujia wewe amri ya Mwenyezi Mungu kuhusu wao, hapatakuwa na yoyote mwenye kukulaumu, kwani ushafikisha yale uliyotumilizwa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 51

وَذَكِّرۡ فَإِنَّ ٱلذِّكۡرَىٰ تَنفَعُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Pamoja na kuwapuuza wao, ewe Mtume, na kutoshughulika na ufidhuli wao, endelea kuwaidhia wale uliotumilizwa kwao, kwani kukumbusha na kuwaidhia watanufaika nako wale wenye nyoyo zenye kuamini, na katika kufanya mawili hayo kuna kusimamisha hoja kwa wenye kupa mgongo. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 51

وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ

Na sikuumba majini na binadamu na kutumiliza Mitume wote isipokuwa kwa lengo tukufu, nalo niabudiwe mimi Peke Yangu, na sio asiyekuwa mimi. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 51

مَآ أُرِيدُ مِنۡهُم مِّن رِّزۡقٖ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطۡعِمُونِ

Sitaki kutoka kwao riziki wala sitaki wanilishe, kwani mimi Ndiye Mpaji Mwenye kuruzuku. Kwani Yeye, Aliyetakasika na kila sifa za upungufu, hawahitaji viumbe Vyake, bali wao ndio wahitaji Kwake katika hali zao zote, Yeye Ndiye Mwenye kuwaumba na kuwaruzuku na Aliyejikwasisha nao kwa kutowahitajia. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 51

إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلۡقُوَّةِ ٱلۡمَتِينُ

Hakika Mwenyezi Mungu , Peke Yake, Ndiye Mwenye kuviruzuku viumbe Vyake, Ndiye Anayedhamini chakula chao, Mwenye nguvu Aliye Thabiti, Hatendeshwi nguvu wala hakuna Mwenye kushindana Naye. Ni Wake Yeye uweza wote na nguvu. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 51

فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذَنُوبٗا مِّثۡلَ ذَنُوبِ أَصۡحَٰبِهِمۡ فَلَا يَسۡتَعۡجِلُونِ

Hakika wale waliodhulumu kwa kumkanusha kwao Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wana fungu la adhabu ya Mwenyezi Mungu mfano wa fungu la wenzi wao waliopita kabla yao. Basi wasiifanyie haraka adhabu , kwani hapana budi ni yenye kuwajia. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 51

فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن يَوۡمِهِمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ

maangamivu na usumbufu ni wa wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kutokana na Siku yao wanayoahidiwa kuteremkiwa na adhabu, nayo ni Siku ya Kiyama. info
التفاسير: