Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Numero di pagina:close

external-link copy
8 : 40

رَبَّنَا وَأَدۡخِلۡهُمۡ جَنَّٰتِ عَدۡنٍ ٱلَّتِي وَعَدتَّهُمۡ وَمَن صَلَحَ مِنۡ ءَابَآئِهِمۡ وَأَزۡوَٰجِهِمۡ وَذُرِّيَّٰتِهِمۡۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

«Mola wetu! Na uwatie Waumini kwenye mabustani ya Pepo ya 'Adn uliyowaahidi wao na baba zao, wake zao na watoto wao waliokuwa wema kwa Imani na matendo mazuri. Hakika wewe Ndiye Mshindi Mwenye kukilazimisha kila kitu, Ndiye Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake na utengenezaji Wake. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 40

وَقِهِمُ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ وَمَن تَقِ ٱلسَّيِّـَٔاتِ يَوۡمَئِذٖ فَقَدۡ رَحِمۡتَهُۥۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

«Na uwaepushie mwisho mbaya wa dhambi zao, usiwaadhibu kwa dhambi hizo. Na yoyote yule utakayemuepushia maovu Siku ya kuhesabiwa, huyo umeshamrehemu na umempa neema ya kuokolewa na adhabu yako. Na huko ndiko kufaulu kukubwa ambako hakuna kufaulu kupita huko.» info
التفاسير:

external-link copy
10 : 40

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُنَادَوۡنَ لَمَقۡتُ ٱللَّهِ أَكۡبَرُ مِن مَّقۡتِكُمۡ أَنفُسَكُمۡ إِذۡ تُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلۡإِيمَٰنِ فَتَكۡفُرُونَ

Hakika ya wale waliokanusha kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki na wakaielekeza ibada kwa asiyekuwa Yeye, watakapovishuhudia wenyewe vituko vya Moto watajichukia machukivu makubwa, na hapo walinzi wa Moto wa Jahanamu watawaita na kuwaambia, «Machukivu ya Mwenyezi Mungu kwenu huko ulimwenguni, Alipowataka nyinyi mumuamini Yeye na muwafuate Mitume Wake na mkakataa, yalikuwa makubwa zaidi kuliko vile mnavyojichukia nyinyi wenyewe hivi sasa, baada ya kujua kwenu kuwa mnastahili hasira za mwenyezi Mungu na adhabu Yake.» info
التفاسير:

external-link copy
11 : 40

قَالُواْ رَبَّنَآ أَمَتَّنَا ٱثۡنَتَيۡنِ وَأَحۡيَيۡتَنَا ٱثۡنَتَيۡنِ فَٱعۡتَرَفۡنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلۡ إِلَىٰ خُرُوجٖ مِّن سَبِيلٖ

Makafiri watasema, «Mola wetu! Umetufisha mara mbili: tulipokuwa matone ya manii ndani ya matumbo ya mama zetu kabla ya kupulizwa roho na ulipokoma muda wetu wa kuishi katika uhai wa duniani, na umetuhuisha mara mbili:katika nyumba ya duniani siku tuliyozaliwa na siku tuliyofufuliwa kutoka makaburini mwetu. Kwa hivyo sisi sasa tunakubali makosa yetu yaliyotangulia, basi je kuna njia yoyote ya sisi kutoka Motoni na uturudishe kupitia njia hiyo duniani tukapate kufanya matendo ya utiifu kwako?» Lakini haliwi hilo kabisa la wao kunufaika kwa kukubali kwao huku. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 40

ذَٰلِكُم بِأَنَّهُۥٓ إِذَا دُعِيَ ٱللَّهُ وَحۡدَهُۥ كَفَرۡتُمۡ وَإِن يُشۡرَكۡ بِهِۦ تُؤۡمِنُواْۚ فَٱلۡحُكۡمُ لِلَّهِ ٱلۡعَلِيِّ ٱلۡكَبِيرِ

Adhabu hiyo ambayo itakayowapata, enyi makafiri, ni kwa sababu ya kuwa nyinyi mlikuwa mkiitwa kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia matendo mema Kwake mnalikanusha hilo, na ashirikishwapo Mwenyezi Mungu mnaliamini hilo na mnalifuata. Basi Mwenyezi Mungu Ndiye Muamuzi kwa viumbe wake, Ndiye Muadilifu Asiyedhulumu, Anamuongoza Ananayemtaka na Anampoteza Anayemtaka, Anamrehemu Anayemtaka na Anamuadhibu Anayemtaka. Hapana Mola isipokuwa Yeye, Aliye juu kidhati, kicheo na kinguvu (kupitisha Analolitaka). info
التفاسير:

external-link copy
13 : 40

هُوَ ٱلَّذِي يُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ رِزۡقٗاۚ وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ

Yeye Ndiye Anayewaonyesha, enyi watu, uweza Wake kwa zile alama kubwa zenye kutolea ushahidi ukamilifu wa Mwenye kuziumba na kuzianzisha, na Anawateremshia mvua kutoka mawinguni ambayo kwayo mnaruzukiwa. Na hajikumbushi kwa alama hizi isipokuwa yule anayerudi kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 40

فَٱدۡعُواْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Basi, enyi waumini, mtakasieni Mwenyezi Mungu Peke Yake ibada na dua, na endeni kinyume na washirikina katika nyendo zao, na hata kama hilo litawakasirisha wao msiwajali. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 40

رَفِيعُ ٱلدَّرَجَٰتِ ذُو ٱلۡعَرۡشِ يُلۡقِي ٱلرُّوحَ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ لِيُنذِرَ يَوۡمَ ٱلتَّلَاقِ

Mwenyezi Mungu Ndiye Mtukufu Aliye juu kabisa Ambaye daraja Zake zimepaa juu sana kwa namna ya kuwa Yeye, kwa daraja hizo, Ameepukana na viumbe Vyake na kimekuwa juu cheo Chake. Yeye Ndiye Mwenye 'Arsh iliyo kubwa. Na miongoni mwa rehema Zake kwa waja Wake ni kuwatumia Wajumbe kuwapelekea wahyi ambao kwa wahyi huo wanapata uhai na kuwa kwenye mwangaza wa kuwapa muelekeo katika mambo yao, ili hao Mitume (walioletewa wahyi) wawaogopeshe waja wa Mwenyezi Mungu na wawaonye Siku ya Kiyama ambayo watakutana Siku hiyo wa mwanzo na wa mwisho. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 40

يَوۡمَ هُم بَٰرِزُونَۖ لَا يَخۡفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِنۡهُمۡ شَيۡءٞۚ لِّمَنِ ٱلۡمُلۡكُ ٱلۡيَوۡمَۖ لِلَّهِ ٱلۡوَٰحِدِ ٱلۡقَهَّارِ

Siku ya Kiyama watajitokeza viumbe mbele ya Mola wao, hakuna chochote kuhusu wao au kuhusu matendo yao waliyoyafanya ulimwenguni kitakachofichamana kwa Mwenyezi Mungu. Hapo Atasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, «Ni wa nani ufalme na mamlaka Siku ya Leo?» Na Ajijibu Mwenyewe, «Ni vya Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake, Mwenye kutendesha nguvu Aliyevilazimisha viumbe vyote kwa uweza Wake na enzi Yake.» info
التفاسير: