Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Numero di pagina:close

external-link copy
44 : 28

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلۡغَرۡبِيِّ إِذۡ قَضَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَى ٱلۡأَمۡرَ وَمَا كُنتَ مِنَ ٱلشَّٰهِدِينَ

Na hukuwako, ewe Mtume, upande wa jabali la jua la kuchwa wa Mūsā, tulipombebesha maamrisho yetu na makatazo yetu, na hukuwa ni kati ya wale waliolishuhudia hilo mpaka kusemwe kwamba habari hii imekufikia kwa njia hii. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 28

وَلَٰكِنَّآ أَنشَأۡنَا قُرُونٗا فَتَطَاوَلَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡعُمُرُۚ وَمَا كُنتَ ثَاوِيٗا فِيٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ تَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِنَا وَلَٰكِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ

Lakini sisi tuliwaumba watu baada ya Mūsā, wakakaa kwa muda mrefu, wakasahau ahadi ya Mwenyezi Mungu, wakaacha amri yake. Wala hukuwa ni miongoni mwa wakazi wa mji wa Madyan ukiwasomea kwao Kitabu chetu, na kwa hivyo ikakujia habari yao na ukaisimulia. Lakini habari uliokuja nayo kuhusu Mūsā ni wahyi na ni ushahidi wa utume wako. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 28

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلطُّورِ إِذۡ نَادَيۡنَا وَلَٰكِن رَّحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوۡمٗا مَّآ أَتَىٰهُم مِّن نَّذِيرٖ مِّن قَبۡلِكَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ

Na hukuwako, ewe Mtume, upande wa jabali la Tūr tulipomuita Mūsā, na hukushuhudia lolote katika hayo. Lakini sisi tulikutumiliza ukiwa ni rehema kutoka kwa Mola wako, ili uwaonye watu ambao hawakujiwa na muonyaji kabla yako, huenda wao wakakumbuka wema uliokuja nao wakaufuata na uovu ulioukataza wakajiepusha nao. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 28

وَلَوۡلَآ أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ فَيَقُولُواْ رَبَّنَا لَوۡلَآ أَرۡسَلۡتَ إِلَيۡنَا رَسُولٗا فَنَتَّبِعَ ءَايَٰتِكَ وَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na lau si adhabu iteremke kwa hawa makafiri kwa sababu ya ukafiri wao, kisha waseme, «Si mwanzo utuletee Mtume kwetu, tupate kuzifuata aya zako zilizoteremshwa kwenye Kitabu chao na tuwe ni miongoni mwa wenye kukuamini» info
التفاسير:

external-link copy
48 : 28

فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ مِنۡ عِندِنَا قَالُواْ لَوۡلَآ أُوتِيَ مِثۡلَ مَآ أُوتِيَ مُوسَىٰٓۚ أَوَلَمۡ يَكۡفُرُواْ بِمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبۡلُۖ قَالُواْ سِحۡرَانِ تَظَٰهَرَا وَقَالُوٓاْ إِنَّا بِكُلّٖ كَٰفِرُونَ

Na alipowajia Muhammad watu hawa akiwa ni muonyaji kwao walisema, «Si apewe, huyu aliyetumilizwa kwetu, mfano wa kile alichopewa Mūsā, cha miujiza inayoonekana na Kitabu kilichoteremshwa mara moja.» Waambie, ewe Mtume, «Je, si Mayahudi walikikanusha kile alicholetewa Mūsā hapo kabla? Walisema kwamba ndani ya Taurati na Qur’ani kuna aina mbili za uchawi zilizosaidiana katika uchawi utokanao na hivyo viwili, na wakasema, «Sisi ni wenye kuvikanusha vyote viwili.» info
التفاسير:

external-link copy
49 : 28

قُلۡ فَأۡتُواْ بِكِتَٰبٖ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ هُوَ أَهۡدَىٰ مِنۡهُمَآ أَتَّبِعۡهُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Waambie hawa, ewe Mtume, «Basi Leteni kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu ambacho ni cha sawa zaidi kuliko Taurati na Qur’ani, nipate kukifuata mkiwa nyinyi ni wakweli katika madai yenu.» info
التفاسير:

external-link copy
50 : 28

فَإِن لَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكَ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَمَنۡ أَضَلُّ مِمَّنِ ٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ بِغَيۡرِ هُدٗى مِّنَ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Wasipokuitikia kwa kuleta Kitabu, na hawakusaliwa na hoja yoyote, basi ujue kwamba wao wanafuata matamanio yao. Na hakuna yoyote aliye mpotevu zaidi kuliko yule aliyefuata matamanio yake bila ya kuwa na uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Hawaafikii kuifikilia haki watu madhalimu walioenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na wakakiuka mipaka Yake. info
التفاسير: