Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Numero di pagina:close

external-link copy
84 : 18

إِنَّا مَكَّنَّا لَهُۥ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَءَاتَيۡنَٰهُ مِن كُلِّ شَيۡءٖ سَبَبٗا

Sisi tulimpa udhibiti katika ardhi na tukampa sababu na njia za kila kitu za kufikia ayatakayo ya kukomboa miji nakuwashinda maadui na yasiyokuwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
85 : 18

فَأَتۡبَعَ سَبَبًا

Akazifuata hizo sababu na njia kwa bidii na juhudi. info
التفاسير:

external-link copy
86 : 18

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَغۡرِبَ ٱلشَّمۡسِ وَجَدَهَا تَغۡرُبُ فِي عَيۡنٍ حَمِئَةٖ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوۡمٗاۖ قُلۡنَا يَٰذَا ٱلۡقَرۡنَيۡنِ إِمَّآ أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّآ أَن تَتَّخِذَ فِيهِمۡ حُسۡنٗا

Mpaka alipofika Dhulqarnain upande wa jua la kuchwa, alilikuta jua kwa vile alivyoliona kama kwamba linakuchwa ndani ya chemchemu ya maji moto yenye udongo mweusi, na akawakuta watu upande huo wa jua la kuchwa. Tulisema, «Ewe Dhulqarnain! Ima uwaadhibu kwa kuwaua au kwa linginelo, iwapo hawatakubali upweke wa Mwenyezi Mungu au uwatendee wema uwafundishe uongofu na uwaonyeshe usawa.» info
التفاسير:

external-link copy
87 : 18

قَالَ أَمَّا مَن ظَلَمَ فَسَوۡفَ نُعَذِّبُهُۥ ثُمَّ يُرَدُّ إِلَىٰ رَبِّهِۦ فَيُعَذِّبُهُۥ عَذَابٗا نُّكۡرٗا

Dhulqarnain akasema, «Ama yule aliyeidhulumu nafsi yake miongoni mwao na akamkanusha Mola wake, basi tutamuadhibu ulimwenguni kisha atarudi kwa Mola wake Amuadhibu adhabu kubwa katika moto wa Jahanamu. info
التفاسير:

external-link copy
88 : 18

وَأَمَّا مَنۡ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَلَهُۥ جَزَآءً ٱلۡحُسۡنَىٰۖ وَسَنَقُولُ لَهُۥ مِنۡ أَمۡرِنَا يُسۡرٗا

«Na ama aliyemuamini Mola wake miongoni mwao, akamkubali, akampwekesha na akafanya matendo ya utiifu Kwake, basi atapata Pepo ikiwa ni malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na tutamfanyia wema na tutasema naye kwa upole na tutaamiliana naye kwa usahali.» info
التفاسير:

external-link copy
89 : 18

ثُمَّ أَتۡبَعَ سَبَبًا

Kisha Dhulqarnain akarudi akaelekea upande wa Mashriki akifuata njia na sababu alizompa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 18

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَطۡلِعَ ٱلشَّمۡسِ وَجَدَهَا تَطۡلُعُ عَلَىٰ قَوۡمٖ لَّمۡ نَجۡعَل لَّهُم مِّن دُونِهَا سِتۡرٗا

Mpaka alipofika upande wa kutoka jua alilikuta hilo jua linawatokea watu wasiokuwa na mjengo ya kuwasitiri wala miti ya kuwapatia kivuli cha kuwakinga na jua. info
التفاسير:

external-link copy
91 : 18

كَذَٰلِكَۖ وَقَدۡ أَحَطۡنَا بِمَا لَدَيۡهِ خُبۡرٗا

Hivyo basi ujuzi wetu umeyazunguka mema aliyokuwa nayo na sababu kubwa alizokuwa nazo popote alipoelekea na kuenda. info
التفاسير:

external-link copy
92 : 18

ثُمَّ أَتۡبَعَ سَبَبًا

Kisha akaenda Dhulqarnain akifuata njia na sababu tulizomtunukia. info
التفاسير:

external-link copy
93 : 18

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ بَيۡنَ ٱلسَّدَّيۡنِ وَجَدَ مِن دُونِهِمَا قَوۡمٗا لَّا يَكَادُونَ يَفۡقَهُونَ قَوۡلٗا

Mpaka alipofika baina ya majabali mawili yaliyozuia vilivyo nyuma yake, aliwakuta hapo watu wasiokaribia kuelewa maneno ya wasiokuwa wao. info
التفاسير:

external-link copy
94 : 18

قَالُواْ يَٰذَا ٱلۡقَرۡنَيۡنِ إِنَّ يَأۡجُوجَ وَمَأۡجُوجَ مُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَهَلۡ نَجۡعَلُ لَكَ خَرۡجًا عَلَىٰٓ أَن تَجۡعَلَ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَهُمۡ سَدّٗا

Wakasema, «Ewe Dhulqarnain, kwa hakika, Ya’jūj na Ma’jūj - nao ni binadamu wa mataifa mawili makubwa- wanafanya uharibifu katika ardhi kwa kuangamiza mazao ya ukulima na vizazi, basi je, tukupatie ujira na tukukusanyie mali ili utuwekee kizuizi baina yetu na wao chenye kupambanua baina yetu na wao?» info
التفاسير:

external-link copy
95 : 18

قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيۡرٞ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجۡعَلۡ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُمۡ رَدۡمًا

Dhulqarnain akasema, «Haya Aliyonipa Mwenyezi Mungu ya ufalme na udhibiti wa mambo, ni bora kwangu mimi kuliko mali yenu, basi nisaidieni kwa nguvu zenu niwafanyie kizuizi baina yenu na wao.» info
التفاسير:

external-link copy
96 : 18

ءَاتُونِي زُبَرَ ٱلۡحَدِيدِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا سَاوَىٰ بَيۡنَ ٱلصَّدَفَيۡنِ قَالَ ٱنفُخُواْۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَعَلَهُۥ نَارٗا قَالَ ءَاتُونِيٓ أُفۡرِغۡ عَلَيۡهِ قِطۡرٗا

«Nipeni vipande vya chuma» Walipkuja navyo, wakaviweka na wakavipanga karibu baina ya yale majabali mawili, aliwaambia wanaofanya kazi, «Washeni moto.» Na kilpogeuka chuma kuwa moto alisema, «Nipatieni shaba iliyodeuka niimimine juu yake.» info
التفاسير:

external-link copy
97 : 18

فَمَا ٱسۡطَٰعُوٓاْ أَن يَظۡهَرُوهُ وَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ لَهُۥ نَقۡبٗا

Hawakuweza Ya’jūj na Ma’jūj kupanda juu ya kile kizuizi kwa kuwa kilikuwa kirefu na kinateleza, na hawakuweza kukitoboa kwa chini yake kwa umbali wa upana wake na ugumu wake. info
التفاسير: