Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Numero di pagina:close

external-link copy
62 : 10

أَلَآ إِنَّ أَوۡلِيَآءَ ٱللَّهِ لَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Jueni mtanabahi kwamba mawalii wa Mwenyezi Mungu hawatakuwa na kicho cha mateso ya Mwenyezi Mungu Akhera, wala wao hawatasikitika juu ya hadhi za kilimwengu walizozikosa. info
التفاسير:

external-link copy
63 : 10

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ

Sifa za Mawalii hawa ni kwamba wao wamemuamini Mwenyezi Mungu na wamemfuata Mtume Wake na yale ambayo alikuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwamba wao wanamcha Mwenyezi Mungu kwa kuzifuata amri Zake na kuyaepuka matendo ya kumuasi. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 10

لَهُمُ ٱلۡبُشۡرَىٰ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ لَا تَبۡدِيلَ لِكَلِمَٰتِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Mawalii hawa wana bishara njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa watapata ya kuwafurahisha katika maisha ya kilimwengu, na miongoni mwayo ni ndoto njema anayoiona mwenyewe au akaonewa na duguye, na watapata Pepo kesho Akhera. Mwenyezi Mungu Haendi kinyume na ahadi Yake wala Haigeuzi. Huko ndiko kufaulu kukubwa, kwa kuwa bishara hiyo imekusanya kuokoka na kila lifanyiwalo hadhari na kufaulu kupata kila litakwalo na kupendwa. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 10

وَلَا يَحۡزُنكَ قَوۡلُهُمۡۘ إِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًاۚ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na yasikusikitishe, ewe Mtume, maneno ya washirikina juu ya Mola wao na kumzulia kwao Yeye urongo na kuishirikisha kwao mizimu ya masanamu pamoja na Yeye. Kwani Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyepwekeka kwa nguvu zilizokamilika na uwezo uliotimia, ulimwenguni na Akhera; na Yeye Ndiye Msikizi wa maneno yao Ndiye Mjuzi wa nia zao na matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 10

أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَمَا يَتَّبِعُ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُرَكَآءَۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنۡ هُمۡ إِلَّا يَخۡرُصُونَ

Jueni mtanabahi kwamba ni wa Mwenyezi Mungu kila aliye mbinguni au ardhini miongoni mwa Malaika, binadamu, majini na wengineo. Na ni nini wanachofuata wale wanaowaomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika hao washirika? Hawana wanachokifuata isipokuwa shaka, na wao hawana lolote isipokuwa wanasema urongo katika yale ambayo wanamnasibisha nayo Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 10

هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ لِتَسۡكُنُواْ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبۡصِرًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ

Yeye Ndiye Ambaye Amewaekea nyinyi, enyi wtu, usiku ili mtuliye ndani yake na mpumzike na usumbufu wa harakati za kutafuta maisha , na Amewaekea mchana ili muone ndani yake na muende mbio kutafuta riziki yenu. Hakika katika kupishana usiku na mchana na hali ya watu katiaka vipindi viwili hivyo pana dalili na hoja, kwa watu wanaozisikia hoja hizi na kuzitafakari, kwamba Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa. info
التفاسير:

external-link copy
68 : 10

قَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدٗاۗ سُبۡحَٰنَهُۥۖ هُوَ ٱلۡغَنِيُّۖ لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ إِنۡ عِندَكُم مِّن سُلۡطَٰنِۭ بِهَٰذَآۚ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Washirikina walisema, «Mwenyezi Mungu amejifanyia mwana» kama vile wanavyosema: ‘Malaika ni watoto wa kike wa Mwenyezi Mungu’, au ‘Al-Masīh( ni mwana wa Mwenyezi Mungu’. Mwenyezi Mungu Ametakasika na hayo yote na Ameepukana nayo! Yeye Ndiye Mkwasi Asiyemuhitajia kila asiyekuwa Yeye. Ni Vyake Yeye vyote vilivyoko kwenye mbingu na ardhi. Vipi basi Atakuwa na mwana miongoni mwa Aliyewaumba na hali ni kwamba kila kitu kinamilikiwa na Yeye? Na nyinyi hamuna dalili yoyote juu ya urongo mnaouzua. Je, mnasema kuhusu Mwenyezi Mungu maneno msiyoyajua ukweli wake na usawa wake? info
التفاسير:

external-link copy
69 : 10

قُلۡ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ

Sema, «Hakika wale ambao wanamzulia Mwenyezi Mungu urongo, kuwa Amejifanyia mwana na kumuengezea mshirika, hawatapata matakwa yao ulimenguni wala Akhera.» info
التفاسير:

external-link copy
70 : 10

مَتَٰعٞ فِي ٱلدُّنۡيَا ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ ٱلۡعَذَابَ ٱلشَّدِيدَ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ

Hakika wao wanastarehe ulimwenguni, kwa ukafiri wao na urongo wao, starehe fupi. Kisha ukomapo muda wao wa kuishi, kuja kwetu ndio mwisho wao. Kisha tutawaonjesha adhabu ya Jahanamu kwa kumkufuru kwao Mwenyezi Mungu, kumkanusha kwao Mitume wa Mwenyezi Mungu na kupinga kwao aya Zake. info
التفاسير: