Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Nomor Halaman:close

external-link copy
24 : 5

قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّا لَن نَّدۡخُلَهَآ أَبَدٗا مَّا دَامُواْ فِيهَا فَٱذۡهَبۡ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَٰتِلَآ إِنَّا هَٰهُنَا قَٰعِدُونَ

Watu wa Mūsā walisema kumwambia, «Hatutaungia mji huo kabisa, iwapo hao majabari wamo humo. Hivyo basi, nenda wewe na Mola wako mkapigane. Ama sisi, tunakaa hapa- hapa na hatutapigana na wao.» Hii inaonesha kushikilia kwao kuenda kinyume na Mūsā, amani imshukie. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 5

قَالَ رَبِّ إِنِّي لَآ أَمۡلِكُ إِلَّا نَفۡسِي وَأَخِيۖ فَٱفۡرُقۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Mūsā alielekea kwa Mola wake akiomba, «Mimi sina uwezo isipokuwa wa nafsi yangu na ndugu yangu, basi hukumu kati yetu na watu wenye kuasi.» info
التفاسير:

external-link copy
26 : 5

قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيۡهِمۡۛ أَرۡبَعِينَ سَنَةٗۛ يَتِيهُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ فَلَا تَأۡسَ عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Mwenyezi Mungu Alisema kumwambia Nabii Wake Mūsā, amani imshukie, «Hakika hiyo ardhi takatifu ni haramu kwa hawa Mayahudi kuiingia kwa muda wa miaka arubaini, watakuwa wakitanga katika ardhi wakiwa kwenye hali ya mshangao. Basi usiwasikitikie, ewe Mūsā, watu waliotoka kwenye utiifu wangu.» info
التفاسير:

external-link copy
27 : 5

۞ وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱبۡنَيۡ ءَادَمَ بِٱلۡحَقِّ إِذۡ قَرَّبَا قُرۡبَانٗا فَتُقُبِّلَ مِنۡ أَحَدِهِمَا وَلَمۡ يُتَقَبَّلۡ مِنَ ٱلۡأٓخَرِ قَالَ لَأَقۡتُلَنَّكَۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Wasimulie, ewe Mtume, Wana wa Isrāīl habari ya wana wawili wa Ādam, Qābīl na Hābīl, nayo ni habari ya kweli, alipotoa kila mmoja wao sadaka, nayo ni ile inayotolewa ili kujisogeza karibu kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Hapo Mwenyezi Mungu Aliikubali sadaka ya Hābīl kwa kuwa alikuwa mcha-Mungu, na Hakuikubali sadaka ya Qābīl, kwa kuwa hakuwa mcha-Mungu. Qābīl alimhusudu ndugu yake na akasema, «Nitakuua.» Hābīl akajibu, «Kwa hakika Mwenyezi Mungu Huikubali sadaka itokayo kwa wale wenye kumuogopa.» info
التفاسير:

external-link copy
28 : 5

لَئِنۢ بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقۡتُلَنِي مَآ أَنَا۠ بِبَاسِطٖ يَدِيَ إِلَيۡكَ لِأَقۡتُلَكَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Hābīl akasema, akimpa mawaidha ndugu yake, «Iwapo utaunyosha mkono wako kwangu ili uniue, hutapata kutoka kwangu mfano wa kitendo chako. Mimi namuogopa Mwenyezi Mungu mola wa viumbe wote. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 5

إِنِّيٓ أُرِيدُ أَن تَبُوٓأَ بِإِثۡمِي وَإِثۡمِكَ فَتَكُونَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلنَّارِۚ وَذَٰلِكَ جَزَٰٓؤُاْ ٱلظَّٰلِمِينَ

«Mimi nataka urudi ukiwa umebeba dhambi la kuniua mimi na dhambi lililokuwa juu yako kabala ya hilo, upate kuwa ni miongoni mwa watu wa Motoni na watakaosalia humo. Na hayo ndiyo malipo ya wanaofanya uadui.» info
التفاسير:

external-link copy
30 : 5

فَطَوَّعَتۡ لَهُۥ نَفۡسُهُۥ قَتۡلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُۥ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Basi ilimpambia Qābīl nafsi yake amuue ndugu yake, akamuua na akawa ni kati ya waliopata hasara, ambao waliuza Akhera yao kwa dunia yao. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 5

فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابٗا يَبۡحَثُ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُۥ كَيۡفَ يُوَٰرِي سَوۡءَةَ أَخِيهِۚ قَالَ يَٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٰرِيَ سَوۡءَةَ أَخِيۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّٰدِمِينَ

Qābīl alipomuua ndugu yake, hakujua aufanye nini mwili wake. Hapo Mwenyezi Mungu Alimtuma kunguru, akawa anafukuwa shimo katika ardhi ili amzike humo kunguru aliyekufa, ili amjulishe Qābīl namna ya kuuzika mwili wa ndugu yake. Qābīl alistaajabu na akasema, «Kwani nimeshindwa kufanya vile kunguru huyu alivyofanya nikapata kuificha aibu ya ndugu yangu?» Hapo Qābīl alimzika ndugu yake. Na baada ya hasara aliyorudi nayo, Mwenyezi Mungu alimpa mateso ya majuto. info
التفاسير: