Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Nomor Halaman:close

external-link copy
203 : 2

۞ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ فِيٓ أَيَّامٖ مَّعۡدُودَٰتٖۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوۡمَيۡنِ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۖ لِمَنِ ٱتَّقَىٰۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Na mtajeni Mwenyezi Mungu kwa kuleta Tasbihi na Takbiri, katika siku chache, nazo ni siku za tshrīq: siku ya kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu za mwezi wa Mfungotatu.Atakaye kufanya haraka kuondoka Mina kabla ya kutwa jua la siku ya kumi na mbili, baada ya kurusha vjiwe, hana makosa. Na yule atakaye kuchelewa kwa kulala Mina kungojea mpaka arushe vijiwe siku ya kumi na tatu, pia hana makosa, kwa aliyemcha Mwenyezi Mungu katika Hija yake. Na kuchelewa ni bora zaidi, maana huko ni kujiongezea mapato katika ibada na kufuata kitendo cha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Na muogopeni Mwenyezi Mungu, enyi Waislamu, na mumweke mbele katika amali zenu zote; na mjue kwamba nyinyi kwake Yeye Peke Yake mtakusanywa baada ya kufa kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa. info
التفاسير:

external-link copy
204 : 2

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعۡجِبُكَ قَوۡلُهُۥ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيُشۡهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلۡبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلۡخِصَامِ

Na baadhi ya watu miongoni mwa wanafiki yanakuvutia, ewe Mtume, maneno yake yaliyo fasaha ambayo kwayo anataka fungu la hadhi za duniani, si za Akhera, na anaapa huku akimshuhudisha Mwenyezi Mungu yaliyo moyoni mwake ya kuupenda Uislamu, hali ya kuwa yeye ana uadui na utesi mkubwa juu ya Uislamu na Waislamu. Huo ni upeo wa ujasiri juu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
205 : 2

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُفۡسِدَ فِيهَا وَيُهۡلِكَ ٱلۡحَرۡثَ وَٱلنَّسۡلَۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَسَادَ

Na anapoondoka kutoka kwako, ewe Mtume, hufanya bidii na akachangamka katika ardhi ili alete uharibifu humo na kutilifisha mazao ya watu na kuua wanyama wao. Na Mwenyezi Mungu Hapendi uharibifu. info
التفاسير:

external-link copy
206 : 2

وَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتۡهُ ٱلۡعِزَّةُ بِٱلۡإِثۡمِۚ فَحَسۡبُهُۥ جَهَنَّمُۖ وَلَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Na anaponasihiwa mnafiki huyo mharibifu na akaambiwa, «Mche Mwenyezi Mungu,ujihadhari na adhabu Yake na ukomeke na kuleta uharibifu katika ardhi,» huwa hakubali nasaha. Bali kile kiburi chake na mori wa kijinga humfanya kutenda maovu zaidi. Basi adhabu yenye kumtosheleza yeye na kumkifu ni Jahanamu. Na hakika uovu wa tandiko ndilo hilo. info
التفاسير:

external-link copy
207 : 2

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشۡرِي نَفۡسَهُ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Na baadhi ya watu huziuza nafsi zao kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, kwa kupigana jihadi katika njia Yake na kujilazimisha kumtii. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja, Anawarehemu waja wake Waumini rehema kunjufu, katika ulimwengu wao na Akhera yao, na kuwalipa malipo mazuri zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
208 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِي ٱلسِّلۡمِ كَآفَّةٗ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola na Muhammad kuwa ndiye Mtume na Uislamu kuwa ndiyo Dini, ingieni katika sheria zote za Uislamu, hali ya kutekeleza hukumu zake zote, wala msiache chochote kati yazo, wala msiandame njia za Shetani katika yale anayowaitia ya maasia.Hakika Shetani kwenu ni adui mwenye uadui uliyo wazi. Basi jihadharini naye. info
التفاسير:

external-link copy
209 : 2

فَإِن زَلَلۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡكُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Na iwapo mtapondoka kwenye njia ya haki, baada ya kujiliwa na hoja wazi-wazi za Qur’ani na Suna, basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika ufalme Wake, hakuna chochote kilicho nje ya mamlaka Yake, ni Mwingi wa hekima kwenye amri Zake na Makatazo yake, Anaweka kila kitu pahali pake palinganapo nacho. info
التفاسير:

external-link copy
210 : 2

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن يَأۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ فِي ظُلَلٖ مِّنَ ٱلۡغَمَامِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ

Hawangojei hawa wakaidi wenye kukanusha, baada ya kusimama dalili wazi, isipokuwa Awajie Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, kwa namna inayolingana na Yeye, Aliyetakasika na kila sifa mbaya, katika vivuli vya Mawingu Siku ya Kiyama ili Aamue baina yao kwa hukumu adilifu, na waje Malaika. Wakati huo, Atahukumu Mwenyezi Mungu, kati yao, hukumu Yake. Na kwake Yeye Peke Yake hurudishwa mambo yote ya viumbe. info
التفاسير: