Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Nomor Halaman:close

external-link copy
197 : 2

ٱلۡحَجُّ أَشۡهُرٞ مَّعۡلُومَٰتٞۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ ٱلۡحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي ٱلۡحَجِّۗ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ يَعۡلَمۡهُ ٱللَّهُۗ وَتَزَوَّدُواْ فَإِنَّ خَيۡرَ ٱلزَّادِ ٱلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُونِ يَٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Wakati wa Hija ni miezi ijulikanayo, nayo ni Mfungomosi, Mfungopili na siku kumi za Mfungotatu.Basi mwenye kujilazimisha nafsi yake kuhiji ndani ya miezi hiyo, kwa kutia nia ya kuhirimia Hija, ni haramu kwake kuundama na vitangulizi vyake vya kimaneno na kivitendo. Pia ni haramu kwake kutoka kwenye twaa ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa kutenda maasia, kubishana, katika Hija, kuletako hasira na chuki. Na wema wowote mnaoufanya, Mwenyezi Mungu Anaujua, na Atamlipa kila mtu kwa amali yake. Na jichukulieni akiba ya chakula na kinwaji kwa safari ya Hija, na akiba ya amali njema kwa nyumba ya Akhera. Hakika akiba iliyo bora zaidi ni kumuogopa Mwenyezi Mungu. Basi niogopeni, enyi wenye akili timamu. info
التفاسير:

external-link copy
198 : 2

لَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَبۡتَغُواْ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكُمۡۚ فَإِذَآ أَفَضۡتُم مِّنۡ عَرَفَٰتٖ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ عِندَ ٱلۡمَشۡعَرِ ٱلۡحَرَامِۖ وَٱذۡكُرُوهُ كَمَا هَدَىٰكُمۡ وَإِن كُنتُم مِّن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلضَّآلِّينَ

Hapana ubaya wowote kwenu kutafuta riziki itokayo kwa Mola wenu, kwa kupata faida ya biashara, ndani ya siku za Hija.Basi mtakapo kuondoka, baada ya kutwa jua, mkirejea kutoka Arafa- napo ni pahali ambapo Mahujaji husimama siku ya tisa ya Mfungotatu-, mtajeni Mwenyezi Mungu kwa kuleta Tasbihi, Talbiyah(Labbaika Allahumma labbaika..) na dua katika sehemu tukufu ya Al- Mashcar al-Harām: Muzdalifa. Na mumtaje Mwenyezi Mungu kwa njia ya kisawa Aliyowaongoza nayo. Na mlikuwa kabla yauongofu huo mko katika upotevu, hamuijui haki. info
التفاسير:

external-link copy
199 : 2

ثُمَّ أَفِيضُواْ مِنۡ حَيۡثُ أَفَاضَ ٱلنَّاسُ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na iwe kuondoka kwenu kutoka kisimamo cha Arafa, ambapo ndipo alipoondoka Ibrahim, amani imshukie, ni katika hali ya kumkhalifu, kwa hilo, yule asiyesimama hapo miongoni mwa watu wa zama za ujinga. Na muombeni Mwenyezi Mungu Awasamehe madhambi yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaghufiria waja wake waombao maghufira, wanaotubia, ni mwenye huruma kwao. info
التفاسير:

external-link copy
200 : 2

فَإِذَا قَضَيۡتُم مَّنَٰسِكَكُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَذِكۡرِكُمۡ ءَابَآءَكُمۡ أَوۡ أَشَدَّ ذِكۡرٗاۗ فَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا وَمَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنۡ خَلَٰقٖ

Basi mtakapokamilisha ibada yenu na mkamaliza amali zenu za Hija, mtajeni Mwenyezi Mungu na mumsifu kwa wingi kama vile mnavyotaja fahari za wazee wenu na zaidi ya hivyo. Kwani wamo miongoni mwa watu kikundi ambacho hima yao yote ni dunia. Hapo, wao huomba wakisema, «Ewe Mola wetu, tupe duniani afya, mali na wana.» Hao hawana Akhera hisa wala fungu lolote, kwa kuipuza Akhera na kujishughulisha na dunia tu. info
التفاسير:

external-link copy
201 : 2

وَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ حَسَنَةٗ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Na miongoni mwa watu kuna kikundi chenye Imani kinachosema katika dua yake, «Mola wetu, tupe duniani afya, mali, elimu inufaishayo, vitendo vyema na mengineyo katika mambo ya dini na dunia. Na katika Akhera, tupe Pepo na utuepushie adhabu ya Moto.» Dua hii ni miongoni mwa dua zilizokusanya. Kwa hivyo, ilikuwa ni dua ambayo Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alikuwa akiiyomba mara nyingi zaidi, kama ilivyothibiti kwenye Sahihi Mbili: ya Bukhari na ya Muslim. info
التفاسير:

external-link copy
202 : 2

أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ نَصِيبٞ مِّمَّا كَسَبُواْۚ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Wale wenye kuomba dua hii wana thawabu kubwa kwa sababu ya amali njema walizozichuma. Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuvihesabu vitendo vya waja wake na Mwenye kuwalipa navyo. info
التفاسير: