क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अली मुहसिन बरवानी

At-Tur

external-link copy
1 : 52

وَٱلطُّورِ

Naapa kwa mlima wa T'ur! [1] info

[1] Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s. alisemezwa.

التفاسير:

external-link copy
2 : 52

وَكِتَٰبٖ مَّسۡطُورٖ

Na Kitabu kilicho andikwa . [2] info

[2] Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s.

التفاسير:

external-link copy
3 : 52

فِي رَقّٖ مَّنشُورٖ

Katika ngozi iliyo kunjuliwa! [3] info

[3] Kilicho andikwa katika kurasa zilio nyepesi kuzisoma,

التفاسير:

external-link copy
4 : 52

وَٱلۡبَيۡتِ ٱلۡمَعۡمُورِ

Na kwa Nyumba iliyo jengwa! [4] info

[4] Na kwa Nyumba iliyo jengwa kwa sababu ya wenye kuizunguka kwa ibada na wenye kusimama na kurukuu na kusujudu kwa Swala,

التفاسير:

external-link copy
5 : 52

وَٱلسَّقۡفِ ٱلۡمَرۡفُوعِ

Na kwa dari iliyo nyanyuliwa! [5] info

[5] Na naapa kwa mbingu iliyo nyanyuliwa bila ya nguzo, na bahari iliyo jaa.

التفاسير:

external-link copy
6 : 52

وَٱلۡبَحۡرِ ٱلۡمَسۡجُورِ

Na kwa bahari iliyo jazwa! [6] info

[6] Na bahari iliyo jaa.

التفاسير:

external-link copy
7 : 52

إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعٞ

Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea. [7] info

[7] Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi waliyo ahidiwa makafiri bila ya shaka itawateremkia hapana hivi wala hivi.

التفاسير:

external-link copy
8 : 52

مَّا لَهُۥ مِن دَافِعٖ

Hapana wa kuizuia. [8] info

[8] Hapana wa kuizuia isiwafikilie.

التفاسير:

external-link copy
9 : 52

يَوۡمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوۡرٗا

Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso! [9] info

[9] Siku mbingu itapo tikisika kwa mtikiso mkubwa.

التفاسير:

external-link copy
10 : 52

وَتَسِيرُ ٱلۡجِبَالُ سَيۡرٗا

Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa. [10] info

[10] Na milima itapo ng'oka kutoka hapo ilipo kwa kuonekana khasa.

التفاسير:

external-link copy
11 : 52

فَوَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Basi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha, [11] info

[11] Maangamio makubwa yatawapata siku hiyo hao wanao kadhibisha Haki.

التفاسير:

external-link copy
12 : 52

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي خَوۡضٖ يَلۡعَبُونَ

Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi. [12] info

[12] Ambao katika upotovu ndio mchezo wao wanapo chezea.

التفاسير:

external-link copy
13 : 52

يَوۡمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا

Siku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu, [13] info

[13] Siku watakapo sukumwa kuingizwa Motoni kwa nguvu.

التفاسير:

external-link copy
14 : 52

هَٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ

(Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha! [14] info

[14] Wataambiwa: Huu ndio Moto mlio kuwa mkiukanusha duniani.

التفاسير: