કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની

Al-Mu'minun

external-link copy
1 : 23

قَدۡ أَفۡلَحَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

HAKIKA wamefanikiwa Waumini! info

Kumethibiti kufanikiwa kwa Waumini wanao muamini Mwenyezi Mungu na waliyo kuja nayo Mitume; na wamefuzu kwa wayatakayo.

التفاسير:

external-link copy
2 : 23

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي صَلَاتِهِمۡ خَٰشِعُونَ

Ambao ni wanyenyekevu katika Swala zao! info

Hao ambao wameambatisha juu ya Imani yao vitendo vyema. Basi hao katika Swala zao humuelekea Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zenye kumkhofu na kumnyenyekea, wanahisi unyenyekevu wa mwisho kwake Yeye .

التفاسير:

external-link copy
3 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنِ ٱللَّغۡوِ مُعۡرِضُونَ

Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi! info

Hao wanashughulikia mambo ya maana, wanapuuza vitendo na maneno yasiyo na kheri ndani yake.

التفاسير:

external-link copy
4 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِلزَّكَوٰةِ فَٰعِلُونَ

Na ambao wanatoa Zaka! info

Nao wanashikilia kutoa Zaka kuwapa wanao stahiki. Kwa hivyo wanakusanya ibada ya mwili na ibada ya mali, na baina ya kujisafisha nafsi na kuyasafisha mali. "Na ambao wanatoa Zaka,": Huu waajibu wa kutoa Zaka unapelekea kujenga mashikamano ya umoja baina ya Waislamu, na kutia katika moyo wa kila mtu kuwa ana jukumu kwa nduguye, anahisi kama anavyo hisi yeye, na anaungulika kama anavyo ungulika yeye. Kwa hivyo ni waajibu wake kufanya awezavyo kumkinga na balaa za kilimwengu, na machungu ya ukosefu. Kwa hivyo fakiri au masikini hatomchukia tajiri, bali wote watahisi kama ni ukoo mmoja unao saidiana na wenye kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu. Wala mwenye deni hakati tamaa kuweza kulipa deni lake lilio bakia ikiwa hana cha kumalizia hilo deni. Wala haianguki chini azma ya mujaahidi anaye pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuinusuru Dini yake na kukomboa nchi yake kwa sababu ya kukosa mali ya kutimizia makusudio yake. Wala msafiri au mgeni mhitaji aliye mbali na mali yake hakosi wa kumkidhia haja zake kwa kumsaidia mpaka afike kwake. Na juu ya haya Zaka ilikuwa ni njia moja katika njia kubwa ulio chukua Uislamu kukombolea mateka na wafungwa na kuondoa utumwa. Na Uislamu umeongeza kutimiza malengo yake ya kijamii kwa ulimwengu mzima ikatupilia mbali chuki zinazo chusha za kidini, na ikatoa ruhusa Zaka wapewe makafiri ikihitajia haja kuwakopesha. Hali kadhaalika hupewa wale wanao itumikia Zaka, kama kuikusanya na kuigawa. Pia waandishi, na wasafiri, na wanao khasiri kwa ajili ya kupatanisha wenye kugombana, na wanao wasaidia Waislamu katika vita. Ama makusudio ya kiuchumi ya Zaka ni kuondoa ufakiri popote ulipo, na kumsaidia kila mwenye haja kama ilivyo kwisha tangulia.

التفاسير:

external-link copy
5 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ

Na ambao wanazilinda tupu zao! info

Nao wanajihifadhi nafsi zao wasiingiane na wanawake. "Na ambao wanazilinda tupu zao, isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka." Aya hizi zinaambatana na Aya nyengine ziliomo katika Suratun Nur zilio anzia: "Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mpigeni kila mmoja wao bakora mia." Hakika Aya hizi tukufu zilizo tajwa zinaashiria maovu ya katika umma yanayo tokea kwa uzinzi. Ama katika umma ni kuvurugika nasaba ya watoto isijuulikane, ama katika siha ni sehemu mbili. KWANZA ni katika mwili, mfano wa kisonono, tego, AIDS n.k. Kisonono huweza kuzalisha maradhi ya urithi kwa watoto hata huweza kuleta upofu. Ama tego (Syphilis) huenea katika mishipa ya damu na ya hisiya na huweza kuishia wazimu, na pia huenea mpaka kwa vizazi, na huenda mtoto akafa tumboni au akatoka na kilema. Ama maradhi ya AIDS (Ukimwi) hayo ni maafa yasiyo semeka, Mwenyezi Mungu atulinde nayo. PILI ni kuathirika mishipa ya hisiya na akili, kwani uzinzi huweza kuathiri dhamiri ya mtu, na kuadhibika nayo, na hata mwishoe huweza kuingia wazimu.

التفاسير:

external-link copy
6 : 23

إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ

Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. info

Isipo kuwa kwa njia ya ndoa ya kisharia, au wenye kumiliki masuria. Hao hawalaumiwi. Zamani utumwa ulikuwa ni jambo la kawaida, na ilikuwa mtu akiweza kuchukua katika wajakazi wake akawafanya kuwa ni wakeze. Na Uislamu ulihalalisha utumwa wa mateka katika vita vilivyo fuata sharia ikiwa maadui nao wanakamata watumwa, basi ilikuwa ni halali kuwatendea wao hali kadhaalika. Ikiwa maadui hawawafanyi mateka kuwa ni watumwa basi ilikuwa haiwafalii Waislamu kuwafanya mateka kuwa ni watumwa.

التفاسير:

external-link copy
7 : 23

فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ

Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. info

Mwenye kutaka kuingiliana na mwanamke bila ya kupitia njia hizi mbili, basi huyo amevuka mipaka ya sharia hadi ya kuvuka. Na (hao Waumini) wawe ni wenye kuhifadhi kila walicho pewa kuwa ni amana, ikiwa mali au neno au kitendo au chenginecho, na watimize kila ahadi iliyo baina yao na Mwenyezi Mungu au na watu. Wasikhuni amana, wala wasivunje ahadi.

التفاسير:

external-link copy
8 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ

Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao! info

Na (hao Waumini) wawe ni wenye kuhifadhi kila walicho pewa kuwa ni amana, ikiwa mali au neno au kitendo au chenginecho, na watimize kila ahadi iliyo baina yao na Mwenyezi Mungu au na watu. Wasikhuni amana, wala wasivunje ahadi.

التفاسير:

external-link copy
9 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَوَٰتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na ambao Swala zao wanazihifadhi . info

Na wawe wenye kudumisha kutimiza Swala kwa nyakati zake, na kuzitekeleza kwa nguzo zake na unyenyekevu wake, mpaka yapatikane makusudio yake. Nayo ni kuachisha uchafu na maovu.

التفاسير:

external-link copy
10 : 23

أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡوَٰرِثُونَ

Hao ndio warithi, info

Hawa wenye kusifiwa hivi ndio watakao rithi kheri yote na wataipata Siku ya Kiyama. Hawa ndio Mwenyezi Mungu atawafadhili kwa kuwapa Firdausi, ndio pahala pa juu kabisa huko Peponi, wastarehe humo peke yao.

التفاسير:

external-link copy
11 : 23

ٱلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡفِرۡدَوۡسَ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo. info

Hawa ndio Mwenyezi Mungu atawafadhili kwa kuwapa Firdausi, ndio pahala pa juu kabisa huko Peponi, wastarehe humo peke yao.

التفاسير:

external-link copy
12 : 23

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن سُلَٰلَةٖ مِّن طِينٖ

Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo. info

Yawapasa watu waangalie asli ya kuumbwa kwao; kwani hiyo ni dalili za kuonyesha uwezo wetu zenye kupelekea kumuamini Mwenyezi Mungu, na kuamini kufufuliwa. Kwani Sisi tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo.

التفاسير:

external-link copy
13 : 23

ثُمَّ جَعَلۡنَٰهُ نُطۡفَةٗ فِي قَرَارٖ مَّكِينٖ

Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. info

Kisha tukaumba vizazi vyake, navyo ni kuwa tulimfanya mtu kwanza tone ya mbegu ya uzazi - yaani maji yenye kila sifa ya uhai wa mwanzo. Tukaiweka kwenye tumbo la uzazi, napo ni pahala pa utulivu palipo lindwa.

التفاسير:

external-link copy
14 : 23

ثُمَّ خَلَقۡنَا ٱلنُّطۡفَةَ عَلَقَةٗ فَخَلَقۡنَا ٱلۡعَلَقَةَ مُضۡغَةٗ فَخَلَقۡنَا ٱلۡمُضۡغَةَ عِظَٰمٗا فَكَسَوۡنَا ٱلۡعِظَٰمَ لَحۡمٗا ثُمَّ أَنشَأۡنَٰهُ خَلۡقًا ءَاخَرَۚ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ أَحۡسَنُ ٱلۡخَٰلِقِينَ

Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji. info

Kisha tukaifanya hii mbegu ya manii baada ya kuipandisha na yai la mwanamke kuwa damu. Kisha damu tukaigeuza kuwa kipande cha nyama, kisha tukafanya mafupa, na mafupa tukayavika nyama. Kisha tukatimiza uumbaji wake mwishoe baada ya kuipulizia roho kuwa kiumbe kingine mbali ili kuanza kumjenga. Shani ya Mwenyezi Mungu imetukuka kwa utukufu wake na uwezo wake. Yeye hana mshabaha wake na yeyote katika kuumba kwake na kutengeza kwake na kuanzisha kwake. Kisha hakika nyinyi wanaadamu baada ya haya mambo yenu tuliyo yataja ni wenye kuyaendea mauti bila ya shaka yoyote.

التفاسير:

external-link copy
15 : 23

ثُمَّ إِنَّكُم بَعۡدَ ذَٰلِكَ لَمَيِّتُونَ

Kisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa. info

Kisha hakika nyinyi wanaadamu baada ya haya mambo yenu tuliyo yataja ni wenye kuyaendea mauti bila ya shaka yoyote.

التفاسير:

external-link copy
16 : 23

ثُمَّ إِنَّكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ تُبۡعَثُونَ

Kisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa. info

Na kisha nyinyi mtafufuliwa Siku ya Kiyama kwa ajili ya kuhisabiwa na kulipwa jaza yenu.

التفاسير:

external-link copy
17 : 23

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعَ طَرَآئِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ ٱلۡخَلۡقِ غَٰفِلِينَ

Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe. info

Na hakika Sisi tumeziumba mbingu saba zilizo nyanyuka juu yenu. Ndani yake vipo viumbe ambavyo hatukughafilika navyo. Tunavihifadhi na tunaviendesha. Na Sisi kabisa hatughafiliki na viumbe vyetu vyote. Bali tunavilinda visipotee na kuharibika, na tunavipangia mambo yao yote kwa hikima. "Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe." Hizo njia saba zilizo tajwa katika hiyo Aya maana yake ni mbingu saba, na kwamba hizo si mbingu moja, na Mwenyezi Mungu haghafiliki na mbingu hizo na viumbe viliomo ndani yake.

التفاسير: