Na ukiwaona miili yao inakupendeza kwa uzuri wao, na wakizungumza unavutika kuwasikiliza kwa utamu wa maneno yao. Kumbe wao juu ya yote hayo nyoyo zao zitupu, hazina Imani ndani yake. Kama magogo yaliyo egemezwa, hayana uhai wowote. Wao hudhania kila linalo zuka basi linawalenga wao, kwa sababu wanaitambua hali yao ya unaafiki. Hao ndio maadui, basi tahadhari nao. Mwenyezi Mungu kesha wafukuza kwenye rehema yake. Vipi wanavyo iacha Haki wakauendea unaafiki wanao ushikilia?