Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - 'Alî Muhsin Al Barwânî

external-link copy
24 : 35

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗاۚ وَإِن مِّنۡ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٞ

Hakika Sisi tumekutuma wewe kwa Haki, kuwa ni mbashiri na mwonyaji. Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao. info

Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma wewe uwafikishie watu wote hii Dini ya Haki, ukiwabashiria Pepo wenye kuamini, na ukiwaonya kwa adhabu ya Moto wanao ikataa hii Dini. Na hapana kaumu yoyote katika kaumu zilizo pita ila walijiwa na mtu kutokana na Mwenyezi Mungu wa kuwahadharisha na adhabu yake.

التفاسير: