Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - 'Alî Muhsin Al Barwânî

An-Nas

external-link copy
1 : 114

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ

Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, info

Sema: Najikinga na Mola Mlezi wa wanaadamu, Mwenye kuendesha mambo yao.

التفاسير:

external-link copy
2 : 114

مَلِكِ ٱلنَّاسِ

Mfalme wa wanaadamu, info

Mfalme wa wanaadamu, kwa ufalme ulio timia, kuwamiliki wote wafalme wao na maraia.

التفاسير:

external-link copy
3 : 114

إِلَٰهِ ٱلنَّاسِ

Mungu wa wanaadamu, info

Mungu wa wanaadamu, Mwenye uweza kwa kuwasarifu kwa ukamilifu atakavyo.

التفاسير:

external-link copy
4 : 114

مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ

Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, info

Na shari ya mwenye kutia wasiwasi watu, ambaye hurudi nyuma ukiomba msaada kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake.

التفاسير:

external-link copy
5 : 114

ٱلَّذِي يُوَسۡوِسُ فِي صُدُورِ ٱلنَّاسِ

Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, info

Ambaye hutia kwa kificho katika vifua vya watu ya kuwaachisha wasende kwenye njia ya uwongofu.

التفاسير:

external-link copy
6 : 114

مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ

Kutokana na majini na wanaadamu. info

Kutokana na majini na wanaadamu.

التفاسير: