Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

An-Naba

external-link copy
1 : 78

عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ

Kuhusu kitu gani baadhi ya makafiri wa Kikureshi wanaulizana? info
التفاسير:

external-link copy
2 : 78

عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ

Wanaulizana kuhusu habari iliyo na uzito mkubwa kabisa, info
التفاسير:

external-link copy
3 : 78

ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ

nayo ni Qur’ani tukufu inayotoa habari za kufufuliwa ambako makafiri wa Kikureshi wana shaka nako na wanakukanusha. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 78

كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ

Mambo sivyo kama wanavyodhania hawa washirikina. Hapo watajua hawa washirikina upeo wa kukanusha kwao na kitawadhihirikia waziwazi kile Atakachowatenda Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 78

ثُمَّ كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ

Kisha litahakikishika kwao jambo hilo na utahakikishika kwao ukweli wa yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuhusu Qur’ani na kufufuliwa. Huu ni utisho na makemeo kwao. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 78

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدٗا

Kwani hatukuwatandazia ardhi kama tandiko? info
التفاسير:

external-link copy
7 : 78

وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادٗا

Na Tukawafanyia majabali kuwa ni vigingi, ili isitisike nanyi? info
التفاسير:

external-link copy
8 : 78

وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجٗا

Na Tukawaumba aina mbali-mbali, mume na mke. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 78

وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتٗا

Na Tukafanya usingizi wenu ni mapumziko kwa viwiliwili vyenu: ndani yake mnatulia na kupumzika? info
التفاسير:

external-link copy
10 : 78

وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا

Na Tukaufanya usiku kuwa ni vazi, unawavisha giza lake na kuwafinika, kama nguo inavyomsitiri mwenye kuivaa. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 78

وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشٗا

Na Tukaufanya mchana ni kipindi cha kutafuta maisha, mnaenea humo kwa ajili ya maisha yenu na mnatembea humo kwa ajili ya maslahi yenu? info
التفاسير:

external-link copy
12 : 78

وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعٗا شِدَادٗا

Na Tukajenga juu yenu mbingu saba, madhubuti jengo lake, lilioumbwa kwa uzuri, halina mapasuko wala nyufa? info
التفاسير:

external-link copy
13 : 78

وَجَعَلۡنَا سِرَاجٗا وَهَّاجٗا

Na Tukalifanya jua kuwa ni taa iwakayo na kung’ara? info
التفاسير:

external-link copy
14 : 78

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءٗ ثَجَّاجٗا

Na Tukateremsha kutoka kwenye mawingu yanyeshayo maji yamiminikayo kwa wingi, info
التفاسير:

external-link copy
15 : 78

لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبّٗا وَنَبَاتٗا

ili Tutoe kwa maji hayo nafaka inayoliwa na watu, info
التفاسير:

external-link copy
16 : 78

وَجَنَّٰتٍ أَلۡفَافًا

nyasi zinazoliwa na wanyama na miti iliyosongamana kwa kutawanyika tagaa zake? info
التفاسير:

external-link copy
17 : 78

إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتٗا

Hakika Siku ya Uamuzi kati ya viumbe, info
التفاسير:

external-link copy
18 : 78

يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجٗا

nayo ni Siku ya Kiyama, imekuwa ni wakati na ahadi iliyowekewa muda maalimu kwa watu wa mwanzo na wa mwisho. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 78

وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبٗا

Na zikafunguliwa mbingu zikawa ni zenye milango mingi kwa ajili ya kuteremka Malaika. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 78

وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا

Na yakalipuliwa majabali baada ya kuwa yamekita, yakawa ni kama mangati. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 78

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادٗا

Hakika Jahanamu, Siku Hiyo, itawalindiza wenye ukafiri ambao Moto huo umeandaliwa wao. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 78

لِّلطَّٰغِينَ مَـَٔابٗا

Kwa makafiri ndio marejeo. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 78

لَّٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابٗا

Watabakia humo muda mrefu ufuatanao, usiokoma. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 78

لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدٗا وَلَا شَرَابًا

Hawatakula humo chochote kitakachozizimisha joto la moto kwao. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 78

إِلَّا حَمِيمٗا وَغَسَّاقٗا

Wala kinywaji kitakachowaondolea kiu yao. Isipokuwa maji moto na usaha wa watu wa motoni. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 78

جَزَآءٗ وِفَاقًا

Watakuwa wanalipwa kwa hilo malipo ya sawa yanayolingana na vitendo vyao walivyovitenda duniani info
التفاسير:

external-link copy
27 : 78

إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابٗا

Hakika wao walikuwa hawaiyogopi Siku ya Hesabu, na kwa hivyo hawakujitayarisha nayo kwa kufanya matendo ya kuwafaa. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 78

وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابٗا

Na waliyakanusha waziwazi yaliyoletwa na Mitume. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 78

وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبٗا

Na kila kitu Tulikijua na Tukakiandika katika Ubao uliohifadhiwa (Al-Lawḥ Al-Maḥfūd). info
التفاسير:

external-link copy
30 : 78

فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا

Basi Onjeni, enyi makafiri, hayo yakiwa ni malipo ya vitendo vyenu, Hatutawazidishia isipokuwa adhabu juu ya adhabu yenu. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 78

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا

Hakika kwa wale ambao wanamuogopa Mola wao na huku wanatenda mema kuna kufaulu kwa kuingia Peponi. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 78

حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبٗا

Hakika watapata Mabustani makubwa na zabibu. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 78

وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابٗا

Na watapata wanawake wenye umri mdogo, wenye vifua vilivyojaza, marika na waume zao. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 78

وَكَأۡسٗا دِهَاقٗا

Na watapata glasi zlizojaa pombe. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 78

لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا كِذَّٰبٗا

Hawatasikia katika Pepo hiyo maneno ya upotofu wala kudanganyana. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 78

جَزَآءٗ مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابٗا

Watayapata yote hayo yakiwa ni malipo na zawadi na kipewa kingi cha kuwatosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, info
التفاسير:

external-link copy
37 : 78

رَّبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلرَّحۡمَٰنِۖ لَا يَمۡلِكُونَ مِنۡهُ خِطَابٗا

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati ya hizo, Mwenye kuwarehemu duniani na Akhera. Hawataweza kumuomba isipokuwa kile walichopewa ruhusa kumuomba. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 78

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ صَفّٗاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابٗا

Siku atakaposimama Jibrili na Malaika wengine hali ya kujipanga mlolongo. Hawatamuombea isipokuwa yule aliyetolewa ruhusa na Mwingi wa Rehema ya kuombewa na akasema maneno ya haki na ya sawa. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 78

ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا

Hiyo ndiyo siku ya haki isiyokuwa na shaka kuja kwake. Kwa hivyo, yule atakaye kuokoka na vituko vya Siku hiyo, na ajifanyie njia ya marejeo kwa Mola wake kutenda vitendo vyema. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 78

إِنَّآ أَنذَرۡنَٰكُمۡ عَذَابٗا قَرِيبٗا يَوۡمَ يَنظُرُ ٱلۡمَرۡءُ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلۡكَافِرُ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ تُرَٰبَۢا

Sisi Tunawaonya nyinyi adhabu ya Siku ya mwisho iliyo karibu. Siku ambayo atayaona kila mtu aliyoyatenda katika kheri au aliyoyachuma miongoni mwa madhambi. Na kafiri atasema, kwa kitisho cha Hesabu, «Laiti mimi nilikuwa mchanga na sikufufuliwa.» info
التفاسير: