Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
9 : 6

وَلَوۡ جَعَلۡنَٰهُ مَلَكٗا لَّجَعَلۡنَٰهُ رَجُلٗا وَلَلَبَسۡنَا عَلَيۡهِم مَّا يَلۡبِسُونَ

Na lau kama tulimfanya mtume aliyeteremshwa kwao ni Malaika, kwani hawakukinai na Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, tungalimfanya Malaika huyo kwenye sura za mwanadamu, ili waweze kumsikia na kusema naye. Kwani haimkiniki kwao kumuona Malaika katika sura zake za kimalaika. Na lau Malaika aliwajia kwa sura za mtu, jambo hilo lingaliwafanya wachanganyikiwe kama lilivyowafanya wachanganyikiwe jambo la Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 6

وَلَقَدِ ٱسۡتُهۡزِئَ بِرُسُلٖ مِّن قَبۡلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُواْ مِنۡهُم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Na kwa kuwa kutaka kwao kuteremshwa Malaika kulikuwa ni kwa njia ya kumfanyia shere Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, Mwenyeyezi Mungu, Aliyetukuka, Aliwaelezea kwamba kuwafanyia shere Mitume, amani iwashukie, si jambo jipya; kwani jambo hilo lilitukia kwa makafiri waliopita kuwafanyia Mitume wao, wakazungukwa na adhabu ambayo walikuwa wakiifanyia shere na wakipinga kuja kwake. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 6

قُلۡ سِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ ثُمَّ ٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Sema kuwaambia, ewe Mtume, «Endeni katika ardhi kisha muangalie: namna gani Mwenyezi Mungu aliwaletea maangamivu na hizaya mwishoni? Basi tahadharini yasiwafikie mfano wa maanguko yao, na ogopeni yasije yakawashukia nyinyi kama yale yaliyowashukia wao.» info
التفاسير:

external-link copy
12 : 6

قُل لِّمَن مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قُل لِّلَّهِۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفۡسِهِ ٱلرَّحۡمَةَۚ لَيَجۡمَعَنَّكُمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا رَيۡبَ فِيهِۚ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Ni ya nani mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake?» Sema, «Ni ya Mwenyezi Mungu. Na kama mnavyolikubali hilo na kulijua, basi muabuduni Yeye Peke Yake. Mwenyezi Mungu Amechukua ahadi juu ya nafsi Yake kurehemu, Hatawaangusiliza waja Wake kwa kuwatesa. Kwa hakika Atawakusanya nyinyi kwenye Siku ya Kiyama ambayo haina shaka ili mhesabiwe na mlipwe. Wale waliomshirikisha Mwenyezi Mungu wamejiangamiza nafsi zao; wao hawampwekeshi Mwenyezi Mungu wala hawaiamini ahadi Yake ya Pepo na Moto na hawaukubali unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 6

۞ وَلَهُۥ مَا سَكَنَ فِي ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Ni wa Mwenyezi Mungu umiliki wa kila kitu, kilicho mbinguni na ardhini, kilichotulia na kinachotembea, kilichofichika na kilicho wazi. Vyote ni watumwa Wake na viumbe Vyake na viko chini ya utendeshaji nguvu Wake, uendeshaji Wake na upangaji Wake. Yeye Ndiye Msikizi wa maneno ya waja Wake, Ndiye Mjuzi wa siri zao na matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 6

قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيّٗا فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَهُوَ يُطۡعِمُ وَلَا يُطۡعَمُۗ قُلۡ إِنِّيٓ أُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَسۡلَمَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na asiyekuwa Yeye, «Je, nimchukue asiyekuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni msaidizi na ni mwokozi, na hali Yeye ni Muumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Yeye Ndiye Mwenye kuwaruzuku viumbe Wake na hakuna mwenye kumruzuku Yeye?» Sema,ewe Mtume, «Mimi nimeamrishwa niwe ni wa mwanzo aliyemnyenyekea Yeye na kumwandama katiika umma huu. Na nimekatazwa kuwa ni miongoni mwa wanaomshirikisha Yeye na asiyekuwa Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 6

قُلۡ إِنِّيٓ أَخَافُ إِنۡ عَصَيۡتُ رَبِّي عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asiyekuwa Yeye, «Mimi naogopa nikimuasi Mola wangu, nikaenda kinyume na maamrisho Yake, na nikamshirikisha Yeye na asiyekuwa Yeye, kuteremkiwa na adhabu kubwa Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 6

مَّن يُصۡرَفۡ عَنۡهُ يَوۡمَئِذٖ فَقَدۡ رَحِمَهُۥۚ وَذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡمُبِينُ

Yule ambaye Mwenyezi Mungu Amemuepushia adhabu kali hiyo, basi Amemrehemu. Kuepushwa huko ndiko kufaulu kuliko wazi kwa kuokolewa na adhabu kubwa. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 6

وَإِن يَمۡسَسۡكَ ٱللَّهُ بِضُرّٖ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَۖ وَإِن يَمۡسَسۡكَ بِخَيۡرٖ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na Akikupatia Mwenyezi Mungu jambo la kukudhuru, kama ufukara na ugonjwa, hakuna mwenye kuliondoa hilo isipokuwa Yeye; na Akikupatia zuri, kama utajiri na afya, hakuna mwenye kuondoa wema wake na hakuna mwenye kuzuia mapitisho Yake, kwani Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, ni muweza wa kila kitu. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 6

وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Ndiye Mwenye kutendesha nguvu, Aliye juu ya waja Wake. Shingo zimemdhalilikia na majabari wamenyongeka Kwake. Yeye Ndiye Mwenye hekima Anayeweka vitu mahali pake kulingana na hekima Yake. Ndiye Mtambuzi Ambaye hakuna kitu chenye kufichika Kwake. Na mwenye kusifika na sifa hizi inapasa asishirikishwe. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya ujuu kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kuwa Yuko juu ya ya viumbe vyake vyote; ujuu wa aina zote unaonasibiana na utukufu Wake, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake. info
التفاسير: