Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
18 : 5

وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ وَٱلنَّصَٰرَىٰ نَحۡنُ أَبۡنَٰٓؤُاْ ٱللَّهِ وَأَحِبَّٰٓؤُهُۥۚ قُلۡ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُمۖ بَلۡ أَنتُم بَشَرٞ مِّمَّنۡ خَلَقَۚ يَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۚ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ

Mayahudi na Wanaswara walidai kuwa wao ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake. Sema kuwaambia, ewe Mtume, «Basi ni kwa nini Atawaadhibu kwa madhambi yenu.» Lau mlikuwa ni vipenzi Vyake hangaliwaadhibu. Kwani Mwenyezi Mungu Hampendi isipokuwa Anayemtii. Na waambie wao, «Bali nyinyi ni viumbe kama walivyo binadamu wengine, mkifanya wema mtalipwa mema kwa wema wenu, na mkifanya ubaya mtalipwa shari kwa ubaya wenu.» Mwenyezi Mungu Atamsamehe Anayemtaka, na Atamuadhibu Anayemtaka. Yeye Ndiye Anayeumiliki ufalme, Anaupeleka Anavyotaka na Kwake ndio marudio. Na hapo Atatoa uamuzi kwa waja Wake na Atamlipa kila mmoja anachostahiki. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 5

يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ عَلَىٰ فَتۡرَةٖ مِّنَ ٱلرُّسُلِ أَن تَقُولُواْ مَا جَآءَنَا مِنۢ بَشِيرٖ وَلَا نَذِيرٖۖ فَقَدۡ جَآءَكُم بَشِيرٞ وَنَذِيرٞۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Enyi Mayahudi na Wanaswara, amewajia mjumbe wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,, ili kuwafunulia haki na uongofu baada ya kipindi kirefu cha wakati baina ya kumtuma yeye na kumtuma ‘Īsā mwana wa Maryam, ili msije mkasema, «Hakutujia mjumbe, mwenye kutoa bishara wala mwenye kuonya.» Hakika ashawajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu mjumbe anayempa bishara njema mwenye kumuamini na anayemuonya mwenye kumuasi. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, wa kumtesa mwenye kuasi na kumpa thawabu mwenye kutii. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 5

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ جَعَلَ فِيكُمۡ أَنۢبِيَآءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكٗا وَءَاتَىٰكُم مَّا لَمۡ يُؤۡتِ أَحَدٗا مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na kumbuka, ewe Mtume, pindi aliposema Mūsā, amani imshukie, kuwaambia watu wake, «Enyi Wana wa Isrāīl, Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu, pindi Alipochagua Manabii kati yenu, Akawafanya wafalme, mnayatawala mambo yenu baada ya kuwa mumetawaliwa na Fir‘aun na watu wake. Na hakika Aliwatunuku nyinyi aina mbalimbali za neema ambazo Hakumtunuku nazo yoyote miongoni mwa walimwengu wa zama zenu. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 5

يَٰقَوۡمِ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡأَرۡضَ ٱلۡمُقَدَّسَةَ ٱلَّتِي كَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمۡ وَلَا تَرۡتَدُّواْ عَلَىٰٓ أَدۡبَارِكُمۡ فَتَنقَلِبُواْ خَٰسِرِينَ

«Enyi watu wangu, Ingieni kwenye ardhi takatifu, yaani iliyotakaswa, nayo ni Bait al-Maqdis na sehemu zilizo kando-kando yake, ambayo Mwenyezi Mungu Ametoa ahadi muingie na mkapigane na makafiri waliyo humo wala msirudi nyuma mkaacha kupigana na hao majabari, kwani mkifanya hivyo mtaikosa heri ya duniani na heri ya Akhera.» info
التفاسير:

external-link copy
22 : 5

قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّ فِيهَا قَوۡمٗا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدۡخُلَهَا حَتَّىٰ يَخۡرُجُواْ مِنۡهَا فَإِن يَخۡرُجُواْ مِنۡهَا فَإِنَّا دَٰخِلُونَ

Walisema, «Ewe Mūsā, hakika huko kuna watu wakali wenye nguvu ambao hatuna uwezo wa kupigana nao. Na sisi hatutaweza kuingia huko na wao wako. Watakapotoka huko, sisi tutaingia.» info
التفاسير:

external-link copy
23 : 5

قَالَ رَجُلَانِ مِنَ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمَا ٱدۡخُلُواْ عَلَيۡهِمُ ٱلۡبَابَ فَإِذَا دَخَلۡتُمُوهُ فَإِنَّكُمۡ غَٰلِبُونَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَتَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Walisema watu wawili kati ya wale wanaomuogopa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ambao Mwenyezi Mungu Aliwapa neema kwa kumtii kwao Yeye na kumtii Mtume Wake, kuwaambia Wana wa Isrāīl, «Ingieni kwa majabari hao kupitia lango la mji wao, ikiwa ni mojawapo ya njia za kutafuta sababu za ushindi. Mtakapoingia langoni, mtawashinda. Na kwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, jitegemezeni, iwapo nyinyi mnamuamini Mtume Wake katika yale Aliyowaletea, mnaiandama sheria Yake kivitendo.» info
التفاسير: