Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
39 : 41

وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦٓ أَنَّكَ تَرَى ٱلۡأَرۡضَ خَٰشِعَةٗ فَإِذَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡهَا ٱلۡمَآءَ ٱهۡتَزَّتۡ وَرَبَتۡۚ إِنَّ ٱلَّذِيٓ أَحۡيَاهَا لَمُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰٓۚ إِنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Na miongoni mwa alama za upweke wa Mwenyezi Mungu na uweza Wake ni kuwa wewe unaiona ardhi ikiwa kavu haina mimea, na tunapoiteremshia mvua, uhai unatambaa ndani yake na inasukikasukika kwa mimea, na ikafura na kunyanyuka. Hakika Yule Anayeihuisha ardhi hii baada ya ukavu wake ni Muweza wa kuwahuisha viumbe baada ya kufa kwao. Hakika Yeye juu ya kila jambo ni Muweza. Na kama usivyoelemewa uweza Wake kuhuisha ardhi baada ya kufa kwake, hivyo hivyo uweza Wake hauelemewi kuwahuisha waliokufa. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 41

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُلۡحِدُونَ فِيٓ ءَايَٰتِنَا لَا يَخۡفَوۡنَ عَلَيۡنَآۗ أَفَمَن يُلۡقَىٰ فِي ٱلنَّارِ خَيۡرٌ أَم مَّن يَأۡتِيٓ ءَامِنٗا يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ ٱعۡمَلُواْ مَا شِئۡتُمۡ إِنَّهُۥ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Hakika ya wale wanaopotoka na haki wakaikanusha Qur’ani na wakaipotoa, hawafichamani kwetu sisi, bali sisi tunawaona wao. Je, huyu mwenye kuzipotosha aya za Mwenyezi Mungu atakayetiwa Motoni ni bora au ni yule atakayekuja Siku ya Kiyama hali ya kuwa amesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kustahiki malipo mema Yake kwa kumuamini na kuzisadiki aya Zake? Fanyeni, enyi wapotofu, mnalolitaka, kwani Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anayaona matendo yenu, hakuna kinachofichika Kwake, na Atawalipa kwa hayo. Hapa pana onyo na hadharisho kwao. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 41

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِٱلذِّكۡرِ لَمَّا جَآءَهُمۡۖ وَإِنَّهُۥ لَكِتَٰبٌ عَزِيزٞ

Hakika ya wale walioikataa hii Qur’ani na wakaikanusha ilipowajia ni wenye kuangamia na kuadhibiwa. Na hii Qur’ani ni Kitabu kitukufu kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amekitukuza na kukitunza na kila ugeuzaji au ubadilishaji. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 41

لَّا يَأۡتِيهِ ٱلۡبَٰطِلُ مِنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَلَا مِنۡ خَلۡفِهِۦۖ تَنزِيلٞ مِّنۡ حَكِيمٍ حَمِيدٖ

Ubatilifu haukifikii kutoka upande wowote katika pande Zake, na hakuna kitu chenye kukibatilisha, kwani hiko kimetunzwa kisipunguzwe wala kisizidishwe. Ni teremsho kutoka kwa Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo ya waja Wake, Mwenye kushukuriwa kwa sifa za ukamilifu Alizonazo. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 41

مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدۡ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبۡلِكَۚ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغۡفِرَةٖ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٖ

Hawakwambii hao washirikina, ewe Mtume, isipokuwa kile ambacho washakisema kabla yao ummah waliopita kuwaambia Mitume wao. Basi vumilia juu ya kinachokupata katika njia ya ulinganizi kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako ni Mwenye msamaha mwingi wa dhambi za wenye kutubia, ni mwenye mateso kwa mwenye kuendelea kumkufuru na kumkanusha. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 41

وَلَوۡ جَعَلۡنَٰهُ قُرۡءَانًا أَعۡجَمِيّٗا لَّقَالُواْ لَوۡلَا فُصِّلَتۡ ءَايَٰتُهُۥٓۖ ءَا۬عۡجَمِيّٞ وَعَرَبِيّٞۗ قُلۡ هُوَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ هُدٗى وَشِفَآءٞۚ وَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ فِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَقۡرٞ وَهُوَ عَلَيۡهِمۡ عَمًىۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُنَادَوۡنَ مِن مَّكَانِۭ بَعِيدٖ

Na lau tungaliifanya hii Qur’ani tuliyokuteremshia, ewe Mtume, ni kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu, washirikina wangalisema, «Je, si zifafanuliwe aya zake tupate kuzifahamu na kuzijua? Ni vipi hii Qur’ani ni kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu na hali lugha ya huyu aliyeteremshiwa ni ya Kiarabu? Hili haliwi!» Waambie, ewe Mtume, «Hii Qur’ani, kwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, ni uongofu kutoka kwenye upotevu na ni ponyesho la yaliyomo vifuani ya shaka na magonjwa. Na wale wasioiamini Qur’ani kuna uziwi ndani ya mashikio yao unaowafanya wasiisikie na wasiizingatie; nayo (hiyo Qur’ani) ni upofu kwao wa nyoyo zao, hawaongoki kwayo.» Basi washirikina hao ni kama yule anayeitwa naye yuko mahali mbali, hamsikii mwenye kulingania wala hamuitiki mwenye kuita. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 41

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ فَٱخۡتُلِفَ فِيهِۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُ مُرِيبٖ

Hakika tulimpelekea Mūsā Taurati kama tulivyokuletea wewe, ewe Mtume, Qur’ani, wakatafautiana watu wake kuhusu hiyo: katika wao kuna aliyeamini na katika wao kuna aliyekanusha. Na lau si neno (la ahadi) lililotangulia kutoka kwa Mola wako la kuwacheleweshea watu wako adhabu, uamuzi baina yao ungalitolewa wa kuwaangamiza makafiri papo hapo. Na kwa hakika washirikina wana shaka nayo sana Qur’ani. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 41

مَّنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا فَلِنَفۡسِهِۦۖ وَمَنۡ أَسَآءَ فَعَلَيۡهَاۗ وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّٰمٖ لِّلۡعَبِيدِ

Mwenye kufanya mema, akamtii mwenyezi Mungu na Mtume Wake, atajipatia mwenyewe thawabu za matendo yake. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, atajionea mwenyewe dhambi za matendo yake. Na Mola wako si Mwenye kuwadhulumu waja kwa kuwapunguzia japo thawabu ya jema moja au kuwaongezea japo dhambi la ovu moja. info
التفاسير: