Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
25 : 30

وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦٓ أَن تَقُومَ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ بِأَمۡرِهِۦۚ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمۡ دَعۡوَةٗ مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ إِذَآ أَنتُمۡ تَخۡرُجُونَ

Na miongoni mwa alama Zake zenye kuonyesha uweza Wake ni kuwa mbingu na ardhi zinasimama, zinatulia na zinajikita kwa Amri Yake, zisitikisike na mbingu isianguke juu ya ya ardhi, kisha Mwenyezi Mungu Atakapowaita nyinyi kwenye kufufuliwa Siku ya Kiyama, muda si muda mtajikuta mnatoka makaburini kwa haraka. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 30

وَلَهُۥ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ كُلّٞ لَّهُۥ قَٰنِتُونَ

Ni wa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, wote waliyoko mbinguni na ardhini, miongoni mwa Malaika, binadamu, majini, wanyama, mimea na visivyo na uhai, wote hao wanafuata amri Yake wanaunyenyekea ukamilifu Wake. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 30

وَهُوَ ٱلَّذِي يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَهُوَ أَهۡوَنُ عَلَيۡهِۚ وَلَهُ ٱلۡمَثَلُ ٱلۡأَعۡلَىٰ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Na ni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anayeanzisha uumbaji viumbe kutoka kwenye hali ya kutokuwako, kisha Atawarudisha wakiwa hai baada ya kufa. Na kuwarudishia viumbe uhai baada ya kufa ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kuanzisha kuwaumba, na yote mawili ni rahisi Kwake. Na ni ya Mwenyezi Mungu sifa ya hali ya juu katika kila anachosifiwa, Hakuna chochote mfano Wake, na Yeye Ndiye Mwenye kusikia, Ndiye Mwenye kuona, Na Yeye Ndiye Mshindi Asiyeshindwa, Ndiye Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake na uendeshaji mambo ya viumbe Vyake. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 30

ضَرَبَ لَكُم مَّثَلٗا مِّنۡ أَنفُسِكُمۡۖ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُم مِّن شُرَكَآءَ فِي مَا رَزَقۡنَٰكُمۡ فَأَنتُمۡ فِيهِ سَوَآءٞ تَخَافُونَهُمۡ كَخِيفَتِكُمۡ أَنفُسَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Mwenyezi Mungu Amewapigia mfano, enyi washirikina, utokao na nafsi zenu: Je kuna yoyote, kati ya watumwa wenu na wajakazi wenu, anayeshirikiana na nyinyi katika riziki yenu na mkaona kuwa nyinyi na wao muko sawa katika hiyo, ikawa mnawaogopa wao kama mnavyowaogopa waungwana washirika katika ugawaji wa mali zenu? Nyinyi hamtaridhika na hilo, basi vipi mtaridhika na hilo upande wa Mwenyezi Mungu kwa kumfanya kuwa Ana mshirika miongoni mwa viumbe Vyake? Kwa mfano wa ufafanuzi huu, tunawafafanulia ushahidi na hoja watu wenye akili timamu ambao watanufaika nao. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 30

بَلِ ٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ أَهۡوَآءَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٖۖ فَمَن يَهۡدِي مَنۡ أَضَلَّ ٱللَّهُۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Bali washirikina walifuata matamanio yao kwa kuwaiga wazazi wao bila ujuzi wowote, wakashirikiana nao katika ujinga na upotevu. Na hakuna yoyote anayeweza kumuongoza yule ambaye Mwenyezi Mungu Amempoteza kwa sababu ya kuendelea kwake kwenye ukafiri na ukaidi. Na hawa hawana wasaidizi wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 30

فَأَقِمۡ وَجۡهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفٗاۚ فِطۡرَتَ ٱللَّهِ ٱلَّتِي فَطَرَ ٱلنَّاسَ عَلَيۡهَاۚ لَا تَبۡدِيلَ لِخَلۡقِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Basi simamisha uso wako, ewe Mtume, wewe na waliokufuata na uendelee kwenye msimamo wa dini ambayo Mwenyezi Mungu Amekuwekea, nayo ni Uislamu ambao Mwenyezi Mungu Ameifanya ilingane na maumbile ya watu. Basi kuendelea kwenu kubaki kwenye Uislamu, na kushikamana kwenu nao ni kushikamana na umbile la Mwenyezi Mungu la kumuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake. Hapana ugeuzaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu na Dini Yake, kwani hiyo ndiyo njia iliyonyoka yenye kupelekea kwenye radhi za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote, na Pepo Yake. Lakini wengi wa watu hawajui kuwa yale niliyokumrisha nayo, ewe Mtume, ndiyo Dini ya haki na si nyigine. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 30

۞ مُنِيبِينَ إِلَيۡهِ وَٱتَّقُوهُ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَلَا تَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na muwe ni wenye kurejea kwa Mwenyezi mungu kwa kutubia na kumtakasia matendo mema. Na muogopeni Yeye kwa kufanya maamrisho na kujiepusha na makatazo, na msimamishe Swala kikamilifu kwa nguzo zake na mambo yake yanayopasa na sharti zake, na msiwe ni miongoni mwa wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu katika ibada. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 30

مِنَ ٱلَّذِينَ فَرَّقُواْ دِينَهُمۡ وَكَانُواْ شِيَعٗاۖ كُلُّ حِزۡبِۭ بِمَا لَدَيۡهِمۡ فَرِحُونَ

Na msiwe ni miongoni mwa washirikina na watu wa (kufuata) matamanio na mambo ya uzushi, walioibadilisha dini yao na wakaigeuza kwa kuchukuwa baadhi yake na kuacha baadhi yake kwa kufuata matamanio yao, wakawa ni makundi na mapote, wanafuata mikao ya viongozi wao na vyama vyao na maoni yao, wanasaidiana wao kwa wao katika batili, kila watu wa kundi wanashangilia na kufurahia mkao wao, wanajihukumia wenyewe kuwa wao wako kwenye haki na wasiokuwa wao wako kwenye ubatilifu. info
التفاسير: