Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Al-Aadiyat

external-link copy
1 : 100

وَٱلۡعَٰدِيَٰتِ ضَبۡحٗا

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda shoti katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 100

فَٱلۡمُورِيَٰتِ قَدۡحٗا

Na wenye kutoa cheche za moto kwa kwato zao ngumu wanapokimbia kwa kasi. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 100

فَٱلۡمُغِيرَٰتِ صُبۡحٗا

Wenye kushambulia maadui kipindi cha asubuhi. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 100

فَأَثَرۡنَ بِهِۦ نَقۡعٗا

Wakarusha vumbi kwa mbio zao. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 100

فَوَسَطۡنَ بِهِۦ جَمۡعًا

Wakautia kati, kwa kuuzunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui. info
التفاسير: