Na mjaalie baba yangu astahili msamaha kwa kumwezesha kuwa Muislamu. Na yeye alikuwa kamuahidi kusilimu siku alio achana naye, kwani yeye huyo baba alikuwa ameitupa kando njia ya uwongofu na uwongozi.
Badala ya Mwenyezi Mungu, na mnadai kuwa ati ndio itakuombeeni hii leo? Je! Inakufaeni kitu kwa kukunusuruni, au hata inajifaa wenyewe kujisaidia? Hapana lolote. Kwani wao na miungu yao ni kuni za Moto.
Pale tulipo kufanyeni nyinyi tulio kuabuduni badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ati ni sawa sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote katika kustahiki kuabudiwa, juu ya kuwa hamjiwezi wala hamfai kwa lolote.
Na hakika katika khabari za Ibrahim zilizo tajwa yapo mawaidha na mazingatio kwa mwenye kutaka mawaidha na akazingatia. Na wala si wengi katika watu wako wanao somewa khabari hizi wenye kuitikia wito wako.
Na Mwenyezi Mungu ametaja khabari za Nuhu kwa kauli yake: Kaumu ya Nuhu iliukanusha Utume wake, wakamrudishia mwenyewe. Kwa kitendo hicho ikawa wamewakadhibisha Mitume wote wa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa wito wao ni mmoja katika asli yake na lengo lake.
Na wala sitaki kwenu ujira kwa ajili ya ninayo kupeni ya nasaha na wito. Na sina malipo ila kwa Mwenye kuwaumba viumbe wote, Aliye miliki mambo yao.