ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس

شماره صفحه:close

external-link copy
62 : 8

وَإِن يُرِيدُوٓاْ أَن يَخۡدَعُوكَ فَإِنَّ حَسۡبَكَ ٱللَّهُۚ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَيَّدَكَ بِنَصۡرِهِۦ وَبِٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na pindi wakitaka kukufanyia njama, Mwenyezi Mungu Atakukinga na udanganyifu wao. Yeye Ndiye Aliyekuteremshia ushindi na Akakutia nguvu kwa Waumini miongoni mwa Muhājirūn (waliohamia Madina kutoka Maka) na Anṣār (wenyeji wa Madina) info
التفاسير:

external-link copy
63 : 8

وَأَلَّفَ بَيۡنَ قُلُوبِهِمۡۚ لَوۡ أَنفَقۡتَ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا مَّآ أَلَّفۡتَ بَيۡنَ قُلُوبِهِمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ أَلَّفَ بَيۡنَهُمۡۚ إِنَّهُۥ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

na Akaziweka pamoja nyoyo zao baada ya utengano, lau ungalitoa mali yaliyoko duniani kote hungaliweza kuziweka pamoja, lakini Mwenyezi Mungu Aliziweka pamoja juu ya Imani wakawa ni ndugu wanaopendana. Hakika Yeye ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwenye hekima katika mambo Yake na uendeshaji Wake. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ حَسۡبُكَ ٱللَّهُ وَمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Ewe Nabii, hakika Mwenyezi Mungu Atakukinga wewe na Atawakinga wale walio pamoja na wewe shari ya maadui wenu. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ حَرِّضِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ عَلَى ٱلۡقِتَالِۚ إِن يَكُن مِّنكُمۡ عِشۡرُونَ صَٰبِرُونَ يَغۡلِبُواْ مِاْئَتَيۡنِۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّاْئَةٞ يَغۡلِبُوٓاْ أَلۡفٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ

Ewe Nabii, wahimize wanaokuamini kupigana vita. Iwapo watapatikana kati yenu watu ishirini wenye kusubiri kwenye kipindi cha kupambana na adui, watawashinda watu mia mbili kati yao. Na iwapo watapatikana kati yenu wapiganaji jihadi mia moja wenye subira, watawashinda Makahri elfu moja, kwa kuwa wao ni watu wasiokuwa na ujuzi na ufahamu wa yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewaandalia wapiganaji jihadi katika njia Yake; kwani wao wapigania utukufu katika ardhi na kufanya uharibifu ndani yake. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 8

ٱلۡـَٰٔنَ خَفَّفَ ٱللَّهُ عَنكُمۡ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمۡ ضَعۡفٗاۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّاْئَةٞ صَابِرَةٞ يَغۡلِبُواْ مِاْئَتَيۡنِۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمۡ أَلۡفٞ يَغۡلِبُوٓاْ أَلۡفَيۡنِ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Sasa hivi Mwenyezi Mungu Amewapunguzia, enyi Waumini, kwa udhaifu mlio nao. Basi ikiwa watakuwako miongoni mwenu watu mia moja wenye subira, watawashinda Makafiri mia mbili. Na iwapo watakuwako kati yenu watu elfu moja, watawashinda watu elfu mbili kati yao kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Na Mwenyezi Mungu Yuko pamoja na wenye subira kwa msaada Wake na nusura Yake. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 8

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُۥٓ أَسۡرَىٰ حَتَّىٰ يُثۡخِنَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ ٱلدُّنۡيَا وَٱللَّهُ يُرِيدُ ٱلۡأٓخِرَةَۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Haifai kwa Nabii awe na mateka miongoni mwa maadui wake mpaka aue kwa wingi, ili kutia kicho ndani ya nyoyo zao na aimarishe misingi ya Dini. Mnataka, enyi mkusanyiko wa Waislamu, kwa kuchukuwa kwenu fidia kutoka kwa mateka wa vita vya Badr, starehe ya ulimwenguni, na Mwenyezi Mungu Anataka kuikuza dini Yake ambayo kwayo hupatikana Akhera. Mwenyezi Mungu ni Mshindi Asiyeshindwa, ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake. info
التفاسير:

external-link copy
68 : 8

لَّوۡلَا كِتَٰبٞ مِّنَ ٱللَّهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمۡ فِيمَآ أَخَذۡتُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Lau si Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu chenye mapitisho na Makadirio yaliyotangulia ya kuhalalisha ngawira na kukomboa mateka kwa umma huu, basi ingaliwapata adhabu kubwa kwa kuchukuwa kwenu ngawira na fidia kabla ya kuletwa sheria kuhusu mambo mawili hayo. info
التفاسير:

external-link copy
69 : 8

فَكُلُواْ مِمَّا غَنِمۡتُمۡ حَلَٰلٗا طَيِّبٗاۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Basi kuleni mlichokipata katika ngawira na fidia ya mateka, kwani hiyo ni halali nzuri. Na jilazimisheni na hukumu za Mwenyezi Mungu na sheria Zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwenye huruma nao. info
التفاسير: