ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس

شماره صفحه:close

external-link copy
41 : 8

۞ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا غَنِمۡتُم مِّن شَيۡءٖ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُۥ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ إِن كُنتُمۡ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا يَوۡمَ ٱلۡفُرۡقَانِ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Na jueni, enyi Waumini, kwamba kile mlichokipata kutoka kwa adui yenu kupitia jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi mafungu manne kati ya mafungu yake matano yapewe wapiganaji ambao walishiriki vitani, na fungu moja lililosalia kati ya yale mafungu matano litagawanywa sehemu tano: ya kwanza ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume, iwekwe kwenye manufaa ya Waislamu wote; ya pili ni ya jamaa wa karibu na Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, nao ni waliozalikana na Hashim na waliozalikana na Muttalib. Wamwekewa sehemu hiyo ya tano mahali pa sadaka, kwani sadaka si halali kwao. Ya tatu ni ya mayatima; ya nne ni ya masikini, na ya tano ni ya msafiri aliyemalizikiwa na matumizi, iwapo nyinyi mnaukubali upweke wa Mwenyezi Mungu, mnamtii Yeye, ni wenye kuyaamini yale Aliyomteremshia mja Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, miongoni mwa aya, usaidizi na ushindi katika siku Aliyopambanua baina ya haki na upotofu hapo Badr, siku lilipokutana kundi la Waumini na kundi la washirikina. Na Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni Mwenye uwezo, Hashindwi na chochote. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 8

إِذۡ أَنتُم بِٱلۡعُدۡوَةِ ٱلدُّنۡيَا وَهُم بِٱلۡعُدۡوَةِ ٱلۡقُصۡوَىٰ وَٱلرَّكۡبُ أَسۡفَلَ مِنكُمۡۚ وَلَوۡ تَوَاعَدتُّمۡ لَٱخۡتَلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡمِيعَٰدِ وَلَٰكِن لِّيَقۡضِيَ ٱللَّهُ أَمۡرٗا كَانَ مَفۡعُولٗا لِّيَهۡلِكَ مَنۡ هَلَكَ عَنۢ بَيِّنَةٖ وَيَحۡيَىٰ مَنۡ حَيَّ عَنۢ بَيِّنَةٖۗ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ

Na kumbukeni pindi mlipokuwa kwenye upande wa bonde lililokuwa karibu sana na mji wa Madina na maadui zenu wameshukia kwenye upande wa bonde la mbali, na msafara wa biashara upande wenu wa chini unaelekea kwenye ufuo wa Bahari Nyekundu. Na lau kama mungalijaribu kuweka maelewano ya makutano hayo mungalitafautiana, lakini Mwenyezi Mungu Aliwakusanya bila kuagana ili Alipitishe jambo ambalo ililazimu lifanyike kwa kuwaokoa vipenzi Vyake na kuwadhalilisha maadui Wake kwa kuuawa na kushikwa mateka. Na hili lilifanyika ili apate kuangamia mwenye kuangamia kati yao kutokamana na hoja ya Mwenyezi Mungu iliyomthibitikia akaiyona na ikaondoa udhuru wake, na apate kuishi mwenye kuishi kutokamana na hoja ya Mwenyezi Mungu iliyomthibitikia na kujitokeza wazi kwake. Na kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia maneno ya makundi mawili hayo, hakifichiki Kwake chochote, ni Menye kuzijua nia zao. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 8

إِذۡ يُرِيكَهُمُ ٱللَّهُ فِي مَنَامِكَ قَلِيلٗاۖ وَلَوۡ أَرَىٰكَهُمۡ كَثِيرٗا لَّفَشِلۡتُمۡ وَلَتَنَٰزَعۡتُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ سَلَّمَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Na kumbuka, ewe Nabii, pindi Mwenyezi Mungu Alipokuonyesha uchache wa maadui zako ukiwa usingizini na ukawajulisha Waumini kuhusu hilo, ndipo nyoyo zao zikapata nguvu na wakawa na ujasiri wa kupigana nao. Na kama Anagalikuonyesha Mola wako wingi wa maadui zako, basi wangalisita Maswahaba wako kupambana nao, na mungalipatwa na uoga na mkatafautiana kuhusu kupigana, lakini Mwenyezi Mungu Aliepusha jambo la nyinyi kushindwa na Akaokoa na mwisho mbaya wa hilo. Hakika Yeye ni Mjuzi mno wa yaliyofichika nyoyoni na maumbile ya nafsi. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 8

وَإِذۡ يُرِيكُمُوهُمۡ إِذِ ٱلۡتَقَيۡتُمۡ فِيٓ أَعۡيُنِكُمۡ قَلِيلٗا وَيُقَلِّلُكُمۡ فِيٓ أَعۡيُنِهِمۡ لِيَقۡضِيَ ٱللَّهُ أَمۡرٗا كَانَ مَفۡعُولٗاۗ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ

Na kumbuka pia pindi walipojitokeza maadui kwenye ardhi ya mapigano mkawaona kuwa ni wachache mkawa na ujasiri juu yao, na Akawafanya nyinyi ni wachache kwenye macho yao, ili waache kujiandaa kupigana na nyinyi, ili Mwenyezi Mungu Alipitishe jambo ambalo hapana budi lifanyike, ili itimie ahadi ya Mwenyezi Mungu kwenu ya himaya na ushindi. Hapo likawa neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu, na neno la wale waliokanusha ndilo la chini, Na kwa Mwenyezi Mungu ndiko marudio ya mambo yote, Apate kumlipa kila mmoja kwa anachostahili kulipwa. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا لَقِيتُمۡ فِئَةٗ فَٱثۡبُتُواْ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا لَّعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, mkutanapo na kundi la watu wa ukafiri wakawa wamejitayarisha kupigana na nyinyi, basi thibitini na msishindwe na wao na mumtaje Mwenyezi Mungu kwa wingi, hali ya kuomba na kunyenyekea, Awateremshie ushindi na uwezo wa kumshinda adui yenu, ili mufaulu. info
التفاسير: