ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس

شماره صفحه:close

external-link copy
150 : 7

وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗا قَالَ بِئۡسَمَا خَلَفۡتُمُونِي مِنۢ بَعۡدِيٓۖ أَعَجِلۡتُمۡ أَمۡرَ رَبِّكُمۡۖ وَأَلۡقَى ٱلۡأَلۡوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأۡسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُۥٓ إِلَيۡهِۚ قَالَ ٱبۡنَ أُمَّ إِنَّ ٱلۡقَوۡمَ ٱسۡتَضۡعَفُونِي وَكَادُواْ يَقۡتُلُونَنِي فَلَا تُشۡمِتۡ بِيَ ٱلۡأَعۡدَآءَ وَلَا تَجۡعَلۡنِي مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Aliporejea Mūsā kwa watu wake akiwa na hasira na huzuni, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimpa habari kwamba watu wake wamepatikana na mtihani na kwamba Sāmirīy amewapoteza. Mūsā alisema, «Ni ubaya ulioje mlioufanya nyuma yangu baada ya mimi kuondoka! Je mumeitangulia amri ya Mola wenu?» Yaani, mulikufanyia haraka kuja kwangu kwenu, na hali ni jambo lililopangwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka?. Mūsā alizitupa mbao za Taurati kwa kuwakasirikia watu wake walioabudu kigombe na kwa kumkasirikia ndugu yake Hārūn. Akakishika kichwa cha Hārūn na akakivuta upande wake. Hārūn alisema kwa kubembeleza, «Ewe mwana wa mamangu, ‘Hakika hawa watu walinidharau, waliniona ni mnyonge na walikaribia kuniua, kwa hivyo usiwafurahishe maadui kwa unayonifanya na usiniingize katika hasira zako ukanifanya ni pamoja na wale walioenda kinyume na amri yako na wakaabudu kigombe.’» info
التفاسير:

external-link copy
151 : 7

قَالَ رَبِّ ٱغۡفِرۡ لِي وَلِأَخِي وَأَدۡخِلۡنَا فِي رَحۡمَتِكَۖ وَأَنتَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ

Mūsā Alisema, ulipomfunukia udhuru wa ndugu yake na kujua kuwa yeye hakufanya uzembe katika kusimama imara juu ya amri ya Mwenyezi Mungu, «Mola wangu nisamehe ghadhabu zangu na umsamehe ndugu yangu yaliyopita kati yake na Wana wa Isrāīl, na ututie ndani ya rehema yako kunjufu, kwani wewe una huruma na sisi zaidi kuliko kila mwenye huruma.» info
التفاسير:

external-link copy
152 : 7

إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ ٱلۡعِجۡلَ سَيَنَالُهُمۡ غَضَبٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَذِلَّةٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُفۡتَرِينَ

Hakika wale waliomfanya kigombe ni mungu itawapata wao ghadhabu kali kutoka kwa mola wao na unyonge katika uhai wa kilimwengu, kwa sababu ya kumkanusha kwao Mola wao. Na kama tulivyofanyia hawa, tutawafanyia wazushi wenye kuleta uzushi katika Dini ya Mwenyezi Mungu; na kila mwenye uzushi katika Dini ni mnyonge. info
التفاسير:

external-link copy
153 : 7

وَٱلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِهَا وَءَامَنُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na wale waliofanya maovu ya ukafiri na maasia kisha wakarejea, baada ya kuyafanya, kwenye Imani na matendo mema, hakika Mola wako baada ya toba ya kidhati ni Msamehefu mno wa vitendo vyao viovu si Mwenye kuwafedhehi kwavyo, ni Mwenye kuwarehemu wao na kila aliye mfano wao miongoni mwa wenye kutubia. info
التفاسير:

external-link copy
154 : 7

وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى ٱلۡغَضَبُ أَخَذَ ٱلۡأَلۡوَاحَۖ وَفِي نُسۡخَتِهَا هُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلَّذِينَ هُمۡ لِرَبِّهِمۡ يَرۡهَبُونَ

Zilipotulia hasira za Mūsā alizichukua mbao baada ya kuwa alizitupa chini, na ndani yake mlikuwa na maelezo ya haki na rehema kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu na kuogopa mateso Yake. info
التفاسير:

external-link copy
155 : 7

وَٱخۡتَارَ مُوسَىٰ قَوۡمَهُۥ سَبۡعِينَ رَجُلٗا لِّمِيقَٰتِنَاۖ فَلَمَّآ أَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ قَالَ رَبِّ لَوۡ شِئۡتَ أَهۡلَكۡتَهُم مِّن قَبۡلُ وَإِيَّٰيَۖ أَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَّآۖ إِنۡ هِيَ إِلَّا فِتۡنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَآءُ وَتَهۡدِي مَن تَشَآءُۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَاۖ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡغَٰفِرِينَ

Na Mūsā alichagua miongoni mwa watu wake wanaume sabiini walio bora kati yao, akatoka na wao akaenda hadi Tū,r Sīnā’ kwa wakati na muda ambao Mwenyezi Mungu Alimuagizia akutane na Yeye pamoja nao ili watubie kwa yale yaliyokuwa kwa wahuni wa Wana wa Isrāīl ya kuabudu kigombe. Walipokuja mahala hapo walisema, «Hatutakuamini, ewe Mūsā mpaka tumuone Mwenyezi Mungu waziwazi, basi utakaposema na Yeye tuoneshe.» Papo hapo walishikwa na mtetemeko mkali wakafa. Akasimama Mūsā akimnyenyekea Mwenyezi Mungu na akasema, «Ewe Mola wangu, niwaambie nini Wana wa Isrāīl nikiwajia na hali wewe umewaangamiza wabora wao? Lau unataka ungaliwaangamiza wote kabla ya hali hii ya kuwa mimi niko na wao. Hilo lingalikuwa sahali zaidi kwangu. Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wachache wa akili miongoni mwetu? Kitendo hiki ambacho watu wangu wamekifanya cha kuabudu kigombe, hakikuwa isipokuwa ni majaribu na mtihani, unampoteza kwayo unayemtaka miongoni mwa viumbe wako na unamuongoza kwayo unayemtaka kumuongoza. Ni wewe mtegemewa wetu na mwenye kutunusuru, tughufirie dhambi zetu na uturehemu kwa rehema zako; na wewe ndiye bora wa wenye kusamehe makosa na kusitiri dhambi. info
التفاسير: