ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس

شماره صفحه:close

external-link copy
105 : 7

حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ قَدۡ جِئۡتُكُم بِبَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَرۡسِلۡ مَعِيَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ

«Nastahili nisiseme kuhusu Mwenyezi Mungu isipokuwa ukweli na inapasa kwangu nijilazimishe nayo. Nimewajia na dalili na hoja zenye ushindi kutoka kwa Mola wenu juu ya ukweli wa yale ninayowatajia. Basi waachilie, ewe Fir'awn, Wana wa Isrāīl pamoja na mimi kutoka kwenye kifungo chako na ukandamizaji wako, na wape uhuru wa kumuabudu Mwenyezi Mungu.» info
التفاسير:

external-link copy
106 : 7

قَالَ إِن كُنتَ جِئۡتَ بِـَٔايَةٖ فَأۡتِ بِهَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Fir'awn alisema kumwambia Mūsā, «Ukiwa umekuja na alama, kama unavyodai, basi niletee na uihudhurishe mbele yangu, ili madai yako yawe ya sawa na ukweli wako uthibiti, iwapo wewe ni mkweli katika madai yako kuwa wewe ni mjumbe wa Mola wa viumbe.» info
التفاسير:

external-link copy
107 : 7

فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٞ مُّبِينٞ

Hapo Mūsā aliitupa fimbo yake na ikageuka nyoka mkubwa anayeonekana waziwazi. info
التفاسير:

external-link copy
108 : 7

وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّٰظِرِينَ

Na akauvuta mkono wake kutoka kwenye uwazi wa kanzu iliyofunguliwa kifuani au chini ya kapwa lake, na papo hapo ukawa mweupe kama maziwa usio na mbalanga, ukiwa ni alama kwa Fir'awn; akiurejesha unarudi rangi yake ya mwanzo, kama ulivyo mwili wake. info
التفاسير:

external-link copy
109 : 7

قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ

Watukufu wa watu wa Fir'awn walisema, «Hakika Mūsā ni mchawi, anayatawala macho ya watu kwa kuwadanganya mpaka ikawaingia kwenye fikira zao kuwa fimbo ni nyoka, na kukiona kitu kinyume na vile kilivyo, na yeye ana ujuzi mwingi wa uchawi na ana uhodari nao. info
التفاسير:

external-link copy
110 : 7

يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُمۡۖ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ

«Yuwataka kuwatoa nyinyi nyote kwenye nchi yenu.» Fir'awn akasema, «Mnanipa shauri gani, enyi watu watukufu, juu ya mambo ya Mūsā?» info
التفاسير:

external-link copy
111 : 7

قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَأَرۡسِلۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ

Wakasema waliohudhuria mjadala wa Mūsā miongoni mwa mabwana wa watu wa Fir’awn na wakubwa wao, «Mfanye Mūsā na Hārūn wangojee, na upeleke askari kwenye miji ya Misri na majimbo yake. info
التفاسير:

external-link copy
112 : 7

يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ

«Ili wakukusanyie kila mchawi mwenye ujuzi mwingi wa uchawi. info
التفاسير:

external-link copy
113 : 7

وَجَآءَ ٱلسَّحَرَةُ فِرۡعَوۡنَ قَالُوٓاْ إِنَّ لَنَا لَأَجۡرًا إِن كُنَّا نَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبِينَ

Wachawi wakamjia Fir'awn wakasema, «Je, tutakuwa na zawadi na mali tukimshinda Mūsā?» info
التفاسير:

external-link copy
114 : 7

قَالَ نَعَمۡ وَإِنَّكُمۡ لَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ

Fir'awn akasema, «Ndio, mtakuwa na malipo na ukaribu na mimi mkimshinda.» info
التفاسير:

external-link copy
115 : 7

قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ نَحۡنُ ٱلۡمُلۡقِينَ

Wakasema wachawi wa Fir'awn kumwambia Mūsā, kwa njia ya kujiona na kutojali. «Ewe Mūsā, chaguwa uwe ni wa mwanzo kutupa fimbo yako au tuwe sisi ni wa mwanzo kutupa.» info
التفاسير:

external-link copy
116 : 7

قَالَ أَلۡقُواْۖ فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ سَحَرُوٓاْ أَعۡيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسۡتَرۡهَبُوهُمۡ وَجَآءُو بِسِحۡرٍ عَظِيمٖ

Akasema Mūsā kuwaambia wachawi, «Tupeni nyinyi.» Walipotupa kamba na fimbo, waliyaroga macho ya watu yakaona kwamba yale waliyoyafanya ni ya kweli, na hali yalikuwa ni kiinimacho na vitu vya kudhania, na waliwatisha watu vitisho vikali na walikuja na uchawi wa nguvu ulio mwingi. info
التفاسير:

external-link copy
117 : 7

۞ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۖ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ

Hapo Mwenyezi Mungu Alimletea wahyi mja Wake na Mtume Wake Mūsā, amani imshukiye, katika kisimamo hicho kikubwa ambacho hapo Mwenyezi Mungu Alipambanua baina ya ukweli na urongo, akimuamuru akitupe kilichoko kwenye mkono wake wa kulia, nacho ni fimbo yake. Akaitupa na papo hapo ikawa inavimeza vile wanavyovitupa na kuwafanya watu wadhanie kuwa ni vya kweli na ilhali ni vya urongo. info
التفاسير:

external-link copy
118 : 7

فَوَقَعَ ٱلۡحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hapo haki ikajitokeza na ikafunuka kwa aliyehudhuria na kuiona kuhusu mambo ya Mūsā, amani imshukie, na kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, analingania haki, na ukabatilika urongo waliokuwa wakiufanya. info
التفاسير:

external-link copy
119 : 7

فَغُلِبُواْ هُنَالِكَ وَٱنقَلَبُواْ صَٰغِرِينَ

Wakashindwa wachawi wote katika mahala walipokusanyika, na akaondoka Fir'awn na watu wake wakiwa wanyonge, waliozidiwa nguvu na kushindwa. info
التفاسير:

external-link copy
120 : 7

وَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ

Wakapomoka wachawi kwa nyuso zao kwa kumsujudia Mola wa viumbe wote, kwa uwezo mkubwa wa Mwenyezi Mungu waliouona. info
التفاسير: