Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al suajili - Ali Muhsen Alberwany

external-link copy
69 : 11

وَلَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجۡلٍ حَنِيذٖ

Na wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema: Salama! Naye akasema: Salama! Hakukaa ila mara akaleta ndama wa kuchoma. info

Na Sisi tuliwatuma Malaika kwa Ibrahim wampe bishara njema yeye na mkewe kuwa watapata mwana. Waliwasalimu kwa kauli ya: Salama! Naye akarejesha amkio lao kwa kusema: Salama! Upesi upesi akenda kuwatengezea ndama aliye nona wa kuchoma ili wale.

التفاسير: