Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

external-link copy
3 : 7

ٱتَّبِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ وَلَا تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۗ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Yafuateni, enyi watu, hayo yaliyoteremshwa kutoka kwa Mola wenu miongoni mwa Qur’ani na Sunnah(mafundisho ya Mtume) kwa kufuata maamrisho na kuepuka makatazo Na wala msiwafuate wategemewa badala ya Mwenyezi Mungu, kama mashetani na wasomi wa Kiyahudi na watawa wa Kinaswara. Hakika nyinyi ni mara chache mnapowaidhika na kuzingatia na mkarudi kwenye haki. info
التفاسير: